Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mo amesema mchakato huo umechelewa kukamilika kwa sababu wapo watu ambao wanaukwamisha
Aidha Mo amesema anawafahamu wote wanaokwamisha mchakato huo na ipo siku atawataja wasipojirekebisha
"Nimefanya nao mkutano, nimewaambia kuwa wale ambao wanakwamisha hili jambo nawajua, kwa hivyo wakiendelea nitatoka hadharani nitawataja kwa majina na hatma yangu mimi na wao itabaki mikononi mwa Wanasimba," alisema Mo
Akizungumzia uwekezaji kwenye soka la vijana ambapo hivi karibuni Simba imeingia mkataba wa miaka miwili na MobiAd, Mo amesema mpango huo ni wa muda mrefu
"Kuwekeza kwenye vijana ni mpango wa muda mrefu, lakini kuna watu wanasema hapana tuwekeze kununua wachezaji ambao utapata mafanikio haraka lakini mara nyingine utafeli"
Aidha kutokana na changamoto zilizojitokeza kwenye usajili, Mo amesema msimu ujao watatumia utaratibu tofauti ambao utawahusisha wataalam wa ndani na nje
"Mimi nimeingia Simba tukiwa na Bajeti ya Bil. 2, leo bajeti yetu mwaka huu 2023/24 inaweza kufika Bil. 20 kwa hivyo Bajeti imezidi mara 10 kwenye miaka mitano haya ni mafanikio makubwa"
"Kuna tatizo, kuna makosa ambayo yamefanyika kwenye usajili, tumesajili wachezaji ambao hawa-perform kwa hivyo mara hii tunakuja na mfumo mpya, tunabadilisha system nzima ya scouting, tutakuwa na watu wa ndani watashirikiana na watu wa nje ambayo ni professional," alisema
Post a Comment