Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mbeya City inajiandaa na mechi yake ya robo fainali ya kombe la shirikisho, (ASFC) dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa Aprili 2, huku Ruvu Shooting wao wakijiwinda dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Aprili 9.
Maafande hao ambao wapo nafasi mbili za mkiani kwenye ligi kwa pointi 20 wameweka kambi yao jijini Mbeya
Mabao ya Mbeya City yamewekwa wavuni na Brown Mwankemwa dakika 16, Eliud Ambokile dakika ya 22, Richardson Ng'ondya dakika ya 77 na Baraka Mwalubanju dakika ya 88 huku la kujifariji kwa Ruvu likifungwa na Mgandila Shaban dakika ya 30.
Kocha mkuu wa Ruvu Shooting, Mbwana Makata amesema aliuhitaji mchezi huo ili kuangalia uimara wa kikosi chake kwa mchezaji mmoja mmoja na kwamba anaendelea kukisuka kabla ya mechi ijayo
"Makosa bado yapo tumekosa hadi penalti lakini pia tumefungwa, naendelea kupambana kuhakikisha nasahihisha upungufu ili mchezo ujao tuweze kushinda na kujiweka pazuri," amesema Makata.
Kocha msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amesema matokeo hayo yanawapa mzuka katika kujiwinda na mechi ijayo ya robo fainali dhidi ya Singida BS na kwamba msimu huu baada ya kukosa nafasi nne za juu kwenye ligi kuu, wanaelekeza nguvu kwenye ASFC.
"Malengo yetu ni kucheza kimataifa na inawezekana, japokuwa kwenye ligi kuu tumeshakwama hivyo tunaenda kupambania kwenye kombe la shirikisho kimsingi ni kufikia ndoto zetu," alisema Mwamlima.
Mwanaspoti
Post a Comment