Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Katika kuonyesha kuwa Yanga 'inautaka' kwelikweli mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa Jumapili, April 02, msafara ulioondoka mapema leo umewajumuishwa vongozi waandamizi wa Yanga na GSM
Wajumbe wawili wa Baraza la Wadhamini Abbas Tarimba na Geofrey Mwambe wako katika msafara huo ambao pia yumo 'bosi kubwa' Ghalib Said Mohamed (GSM)
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said yeye ameongoza safu ya uongozi, msafara mzima ukiwa na takribani watu 44
Ni mara chache sana kumuona GSM akisafiri na timu, unapoona kafanya hivyo basi fahamu huko aendako kuna jambo kubwa!
Yanga imedhamiria kuweka rekodi ya kuvuka hatua ya robo fainali ambayo tangu mfumo mpya wa mashindano ta CAF ulipoanza kutumika mwaka 2016, hakuna timu ya Tanzania ambayo imewahi kuvuka hatua hiyo iwe ligi ya mabingwa au kombe la Shirikisho
Hesabu za Yanga ni kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi D nafasi ambayo mpaka sasa bado wanaishikilia
Wananchi wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya TP Mazembe ili kujiweka katika nafasi nzuri huku wakisubiri matokeo ya mchezo kati ya US Monastir dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa saa 4 usiku. Mechi ya TP Mazembe dhidi ya Yanga itapigwa saa 10 jioni
Yanga imefunga mabao mengi kuliko Monastir na pia wana uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa wakiizidi Monastir GD 1
Kama Yanga watashinda hata bao moja dhidi ya TP Mazembe, basi US Monastir watahitaji kushinda angalau mabao matatu kuipiku Yanga kileleni
Hivyo Wananchi watahitaji kupata ushindi wowote ingawa wakifunga zaidi ya mabao mawili itawaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kumaliza kileleni
Post a Comment