Kadi za njano zaiweka Simba ktk mtego huu ligi ya mabingwa

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa kukamilisha ratiba ligi ya mabingwa dhidi ya Raja Casablanca. Mchezo huo utapigwa April 01 huko Morocco 


Ni mchezo wa kukamilisha ratiba kwa sababu Raja na Simba zimefuzu hatua ya robo fainali kundi C, Raja ikimaliza nafasi ya kwanza na Simba ikishika nafasi ya pili


Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira anakiandaa kikosi chake bila ya nyota wake saba ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa


Aidha katika mchezo huo, Simba pia itawakosa wachezaji wake Mohammed Hussein 'Tshabalala' na Kibu Denis wanaotumikia adhabu ya kadi mbili za njano


Tshabalala alionyeshwa kadi za njano katika mechi zote mbili dhidi ya Horoya Ac, wakati Kibu alionyeshwa kadi za njano katika michezo dhidi ya Vipers Fc (Ugenini) na Horoya Ac


Huenda Gadiel Michael akapata nafasi ya kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi ya mabingwa msimu huu katika mchezo dhidi ya Raja wakati Robertinho ana wachezaji wengi ambao anaweza kuwatumia katika nafasi ya Kibu


Robertinho huenda akalazimika kufanya mabadiliko ya kikosi chake ili kuhakikisha anakuwa kikosi imara katika mchezo wa robo fainali


Baadhi ya nyota wana kadi za njano ambapo kama watapata kadi ya pili katika mchezo huo watakosa mechi ya kwanza ya robo fainali


Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Joash Onyango, Hennock Inonga, Mzamiru Yassin, Saido Ntibazonkiza, Pape Ousmane Sakho, John Bocco na Moses Phiri

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post