Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Musonda aliondoka Power Dynomos kuijunga na Yanga akiwa kinara wa mabao huko Zambia akifunga mabao 11
Mifumo yote anayopenda kutumia Nabi ni kuweka mshambuliaji mmoja mbele. Changamoto ilionekana katika mechi za mwanzo.
Lakini sasa Nabi amepata mfumo sahihi wa kuwatumia Musonda na Mayele na unaweza kusema pacha yao imewaka!
Nabi anamtumia Musonda kama wingi anayetokea upande wa kushoto lakini mara nyingi huingia ndani kuungana na Mayele wakati Joyce Lomalisa akipanda
Tayari Musonda amefunga mabao matano katika mashindano yote, mabao mawili amefunga kombe la FA, bao moja amefunga kwenye ligi na mabao mawili amefunga kwenye kombe la Shirikisho
Katika michuano ya kombe la Shirikisho Musonda ndio kinara wa kutengeneza mabao akiwa na assist tatu, mbili akiwa amemtengenezea Mayele
Mayele ndiye kinara wa mabao kombe la Shirikisho akiwa ameweka kambani mabao matatu
Post a Comment