Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba ilitinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa kihistoria wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya Ac na kujihakikishia kumaliza katika nafasi ya pili kundi C huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi
Ahmed amesema wamezisikia kauli za baadhi ya wachambuzi kuhusu hatma yao katika hatua ya robo fainali
"Sisi malengo yetu msimu huu ni kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa. Hii robo fainali imekuwa kawaida kwetu sasa tunataka kwenda mbali zaidi"
"Hatutamuogopa yeyote ambaye tutapangwa nae kwenye robo fainali. Iwe ni Mamelodi, Wydad au Esperance hawa sisi tunawamudu na tutaruka nao vizuri tu," alitamba Ahmed
Katika hatua ya robo fainali, Simba itapangwa na timu iliyomaliza kinara wa kundi A, B au D
JS Kabylie na Wydady Athletic zimetinga robo fainali kutoka kundi A zote zikiwa na alama 10, kinara wa kundi atafahamika kwenye mechi za kuhitimisha hatua ya makundi timu hizo zikichuana nchini Morocco Wydad wakiwa nyumbani
Mamelodi Sundowns wana nafasi kubwa ya kumaliza vinara wa kundi B wakiwa tayari na wametinga robo fainali
Esperance ina nafasi kubwa ya kumaliza kinara wa kundi D ikiwa tayari imetinga robo fainali pamoja na CR Belouizdad ya Algeria
Esperance itacheza na CR Belouizdad mechi ya kuhitimisha makundi
Post a Comment