Emmanuel Okwi na Kocha wake waufungukia mchezo wa kesho


 Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Uganda Milutin Sredojevic 'Micho' amesema kikosi chake kipo katika kipindi cha mpito ambapo wanatengeneza timu imara kutoka kwa wachezaji wazoefu na kuwaingiza wachezaji vijana


Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Micho alisema kukutana na Tanzania yenye wachezaji kadhaa wanaocheza nje (Misri, Saudi Arabia, Ubelgiji) pamoja na wale wa Simba na Yanga kunafanya timu Taifa Stars kuwa timu imara.


"Lazima nikiri Tanzania na Uganda ziko mazingira tofauti kwa sasa. Tunacheza na timu ambayo ina wachezaji katika klabu ambazo zimefuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya nabingwa na kombe la Shirikisho. Tunacheza na timu ambayo imepeleka wachezaji nchi kama Morocco, Misri, Saudi Arabia na barani Ulaya"


"Sisi tuko katika kipindi cha mpito. Tunajaribu kuingia damu changa kwenye timu yetu baada ya wachezaji wetu wengi ambao muda wao wa kuitumikia timu ya Taifa unamalizika"


"Hautakuwa mchezo mwepesi hata kidogo lakini sisi tumekuja hapa kupambana kusaka matokeo muhimu kutuweka hai matumaini yetu kwenye michuano ya Afcon," aisema Michu


Nae nahodha wa Uganda Emmanuel Okwi amesema wamepata mapokezi mazuri Tanzania, wako tayari kwa mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Jumanne dhamira yao ikiwa kuibuka na ushindi


Okwi amesema walipoteza mchezo wao wa nyumbani hivyo nao watapambana ili kuhakikisha wanashinda na kufufua matumaini ya kushiriki fainali za Afcon 2023

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post