Bayern Munich yamfungashia virago kocha wake


 Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamemfuta kazi Kocha wao Mkuu Julian Nagelsmann


Uamuzi huo umechukuliwa mara moja huku ikibainishwa kuwa wakati wowote watamtangaza kocha wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel kuwa mrithi wake


Tuchel anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuwanoa matajiri hao wa Ujerumani


Msimu huu Bayern wamekuwa na mwenendo wa kusuasua kwenye ligi wakishika nafasi ya pili nyuma ya Borussia Dortmund wakizidiwa alama moja


Hata hivyo Nagelsmann aliiwezesha Bayern kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kuwaondosha PSG kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-0


Baada ya kutimuliwa na Beyern, Nagelsmann anaweza kuibukia Uingereza kunako klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo inatarajiwa kumfuta kazi Antonio Conte

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post