Arsenal yapata pigo Tena

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA

Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
 
Beki wa Arsenal Takehiro Tomiyasu atakosa mechi zilizosalia msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa jeraha la goti, klabu hiyo ya Ligi ya Premia imethibitisha.


Beki wa kulia wa Japan, Tomiyasu alitoka nje dakika tisa katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Europa kwa Arsenal dhidi ya Sporting ya Ureno baada ya kuteleza vibaya na kuumia goti


Arteta alionyesha wasiwasi wake punde tu baada yabeki huyo kuumia kwani mchezaji huyo wa kimataifa wa Japan mwenye umri wa miaka 24 'si mtu wa kutia chumvi mambo'


"Kufuatia kubadilishwa kwake wakati wa mechi ya Ligi ya Europa Alhamisi iliyopita, tathmini zilizofuata zimethibitisha kwamba Takehiro Tomiyasu alipata jeraha kubwa kwenye goti lake la kulia," Arsenal ilisema katika taarifa


"Tomi amefanyiwa upasuaji wa mafanikio London siku ya Jumanne na ataondolewa kwa muda uliosalia wa msimu huu."


Arsenal ilitupwa nje ya Ligi ya Europa kwa mikwaju ya penalti lakini bado ipo kileleni mwa Ligi Kuu ya England ikiwa na pointi nane mbele ya Manchester City, ambayo ina mechi moja mkononi.


Klabu hiyo ya London kaskazini pia ilimpoteza mlinzi William Saliba kutokana na jeraha la mgongo katika mchezo huo

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post