Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Leo majira ya saa nne usiku kwa saa za Morocco, Wekundu wa Msimbazi Simba watashuka uwanja wa Mohammed V kuwakabili Raja Casablanca katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Ni mchezo wa kukamilisha ratiba tu kwani Simba na Raja tayari zina tiketi ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa
Pamoja na mazingira hayo, bado ni mechi muhimu kwa kila timu kulinda heshima kwenye michuano hiyo
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema hawana presha yoyote kuelekea mchezo huo lakini watapambana ili kulinda heshima ya mpira na klabu ya Simba
Ahmed amesema hii sio mechi ya kuwaweka mashabiki katika presha kwani ni mechi ya kukamilisha ratiba tu ambayo Simba itaicheza kimkakati muhimu kwao ni kulinda heshima ya klabu tu
"Mechi hii haina presha yoyote upande wetu sababu tumeshafuzu robo fainali. Ni mechi ya kukamilisha ratiba tu"
"Ila kwa heshima ya klabu ya Simba, na kwa heshima ya mpira wa miguu ni mechi ambayo hatutaicheza kwa dharau kwani tunajua tukifanya hivyo tunaweza kupoteza pengine zaidi ya vile ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza Dar"
"Benchi la ufundi na wachezaji wataingia katika mchezo huu wakifahamu ni mechi ya kulinda heshima ya klabu yetu, pamoja na kuwa ni mechi ambayo matokeo yake hayana umuhimu, lengo letu ni kuona tunacheza vizuri na hatupotezi mchezo huo," alisema Ahmed
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam Raja waliibuka na ushindi wa mabao 3-0, shauku ya mashabiki wa Simba leo ni kuona ushindi unapatikana hukohuko kwao
Post a Comment