Yanga kuifuata US Monastir Leo, CAF Confederation Cup
Yanga vs US Monastir 12 February 2023, Yanga SC vs Monastir Kombe la Shirikisho Afrika, Young Africans vs US Monastir, Young Africans vs US Monastir, US Monastir vs Yanga SC CAF Confederation Cup, Yanga SC vs US Monastir.
KIKOSI cha Yanga kinatarajiwa kusafiri leo kuelekea nchini Tunisia kwaajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) dhidi ya US Monastir Jumapili hii ya February 12, 2023.
Afisa Habari wa Klabu hiyo Ali Kamwe amesena kuwa maandalizi yao ya hapa nyumbani na kule Tunisia wanapokwenda yapo sawa na wapo tayari kuishangaza Afrika kwa kufuzu hatua inayofuata wakiwa vinara wa Kundi D.
“Mpaka sasa hivi kila kitu kinakwenda sawa kwenye upande wa maandalizi, na tunaposema maandalizi kwenye hii michezo ya Afrika huwa tunamaanisha mambo makubwa mawili.”
“Jambo la kwanza ni maandalizi ya kiufundi, Kocha Nabi na wasaidizi wake mpaka sasa hivi kila kitu kinakwenda sawa kwa 95%. Kumekuwa na sessions tofauti za mazoezi.”
“Tutakuwa na session nyingine ya mwisho hapa Dar kabla ya timu kuondoka kuelekea Tunisia.”
“Upande wa pili wa maandalizi tunaouzungumzia ni mambo ya logistics, timu inasafiri lini, inasafiri kwa usafiri gani, itafikia hoteli gani, itafanyia mazoezi wapi n.k”
“Huku nako kwa zaidi ya 90% uongozi wa Yanga umefanya kila linalowezekana yote tuliyokuwa tumetapanga yamekwenda vizuri.”
Yanga itaondoka majira ya saa 9 kuelekea Tunisia ambapo itapitia Dubai, na inatarajiwa kuwasili Dubai majira ya saa ya 3:50 usiku.
Kesho asubuhi saa 2:40 Yanga itaondoka Dubai kuelekea Tunis tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir.
Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Stade Olympique Hammadi Agrebi kwa sababu Uwanja wa nyumbani wa Monastir haukukidhi vigezo vya CAF.
Katika safari hiyo Yanga itaondoka na Wachezaji 25 akiwemo Aboutwalib Mshery ambaye anakwenda nchini Tunisia kwaajili ya matibabu zaidi.
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.
The post Yanga kuifuata US Monastir Leo, CAF Confederation Cup appeared first on Nijuze Mpya.
Post a Comment