Simba kuifuata Horoya kesho – CAF Champions League

Simba kuifuata Horoya kesho – CAF Champions League

Simba vs Horoya, Simba SC vs Horoya Athletic Club, Simba vs Horoya CAF Champions League, Horoya vs Simba, Horoya Athletic Club vs Simba Sports Club, Horoya AC vs Simba SC.

Simba kuifuata Horoya kesho - CAF Champions League

Simba kuifuata Horoya kesho – CAF Champions League

 

KIKOSI Cha Simba Sports Club kinatarajia kuondoka nchini kesho saa 10 alfajiri kuelekea Guinea kwaajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya Athletic Club.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii ya February 11, 2023 kwenye Uwanja wa General Lansana Conte nchini Guinea kuanzia saa 19:00 Usiku.

Kikosi hicho kitaondoka na msafara wa watu 45 ambapo wachezaji watakuwa 25 benchi la ufundi pamoja na viongozi wa timu.

Simba itasafiri na ndege ya Shirika la Ndege ya Ethiopia (Ethiopia Airlines) ambapo msafara huo utapitia nchini Ethiopia na kubadili ndege ambayo itawapeleka hadi Guinea ambapo watafika kesho jioni.

Baada ya kuwasili salama nchini Guinea Wachezaji watafanya mazoezi ya utimamu wa mwili ili kuondoa uchovu wa safari.

Aidha Kikosi hicho kimekamilisha maandalizi yake kabla ya kuanza safari ya kuelekea Guinea.

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.

The post Simba kuifuata Horoya kesho – CAF Champions League appeared first on Nijuze Mpya.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post