
Robertinho kuelekea mchezo vs Azam 21 February 2023

Robertinho kuelekea mchezo vs Azam 21 February 2023
Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kuwa anawaamini wachezaji wake kuelekea mchezo wa raundi ya 24 dhidi ya Azam FC kesho Jumanne ya tarehe 21 February 2023
Robertinho amekiri kuwa utakuwa mchezo mgumu wa Derby ya Mzizima dhidi ya Azam FC.
Robertinho ameongeza kuwa walipata matokeo mazuri kwenye mechi za Ligi zilizopita na wanajua umuhimu wake na wapo tayari kuhakikisha wanapata Ushindi.
Robertinho ameongeza kuwa amewasisitiza Wachezaji mazoezini kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi wanazo tengeneza na kuzuia pamoja wanaposhambuliwa.
“Tuna matokeo mazuri kwenye ligi, tunatakiwa kuongeza kupata matokeo bora, tumetoka kupoteza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa hatutaki kupoteza tena kwakuwa itashusha morali yetu.
“Itakuwa mechi ngumu sababu ni Derby, Azam ni timu nzuri na tunaiheshimu lakini nawaamini wachezaji wangu watafanya vizuri,” amesema Robertinho.
Akizungumzia uwepo wa kiungo mkabaji, Sadio Kanoute ambaye alikosekana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Raja Casablanca kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Robertinho amesema:
“Nimefurahi kwa Kanoute kurejea kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Azam kwakuwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza, uwepo wake unatupa machaguo mengi ya upangaji wa kikosi.”
“Pia Jonas Mkude ambaye alikuwa majeruhi nilimpa dakika 45 za mwisho kwenye mchezo uliopita na amefanya vizuri nimefurahi, anakuja kuongeza kitu kikosi,” amesema Robertinho.
The post Robertinho kuelekea mchezo vs Azam 21 February 2023 appeared first on Nijuze Mpya.
from Michezo – Nijuze Mpya https://ift.tt/3z8OrYi
via IFTTT
Post a Comment