Kaze tuko tayari, watatu kuikosa KMC FC 22 February 2023
KOCHA Msaidizi wa Klabu ya Yanga SC, Cedric Kaze amesema kuwa wameelekeza nguvu zozte kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC FC ambao utapigwa kesho Jumatano ya February 22 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari Leo, Kaze amesema kuwa hawakupata muda wa kufanya mazoezi baada ya mchezo dhidi ya TP Mazembe lakini wamefanya ‘recovery’, ari na morali za wachezaji ziko juu kuelekea mchezo dhidi ya KMC.
“Tumefanya recovery nzuri baada ya mchezo dhidi ya TP Mazembe. Mechi mbili za CAF Confederation Cup zimetusaidia kuimarika, ari na morali ya wachezaji iko juu naamini watapambana ili kuweza kupata alama tatu”
“Tumekuwa na mwenendo mzuri katika mechi za ligi kuu zilizopita lakini hizo ni takwimu tu ambazo zinatupa heshima, kikubwa tunaangalia mechi iliyo mbele dhidi ya KMC”
“Mechi hii tunacheza katika nyakati ngumu kwa sababu mbele tunakabiliwa na mchezo wa kombe la Shirikisho lakini wakati huohuo tuko kwenye nyakati ambazo hatupaswi kupoteza alama kwenye Ligi”
“Tumezungumza na wachezaji wasahau furaha ya Matokeo ya Mechi iliyopita na waelekeze nguvu kwenye mchezo muhimu dhidi ya KMC ambao tunapaswa kushinda,” amesema Kaze
Akizungumzia hali ya kikosi, Kaze amesema hakuna majeruhi wapya, Wachezaji watakaokosekana ni walewale ambao bado wako nje wakiendelea na matibabu ambaobni Benard Morrison, Denis Nkane na Aboutwalib Mshery.
Aidha KMC imetangaza Viingilio vya mchezo huo, ambapo kwa VIP A itakuwa Tsh 15,000, VIP B itakuwa Tsh 10,000 na Mzunguuko itakuwa Tsh 5,000 tu.
Mchezo huo wa raundi ya 24 Ligi Kuu ya NBC utapigwa kuanzia saa 10:00 Jioni.
The post Kaze tuko tayari, watatu kuikosa KMC FC 22 February 2023 appeared first on Nijuze Mpya.
from Michezo – Nijuze Mpya https://ift.tt/wgsaEjo
via IFTTT
Post a Comment