Singida Big Stars yatoa ufafanuzi Usajili wa Kazadi Kasengu
Francis Kazadi Kasengu Singida Big Stars FC, Francis Kazadi Kasengu Singida Big Stars, Kazadi Kasengu Singida Big Stars, Kazadi Kasengu Singida Bs, Singida Big Stars DR Congo, Usajili wa Kazadi Kasengu Singida Big Stars, Usajili Singida Big Stars, Kazadi Kasengu Mshambuliaji wa Singida Big Stars.
- FAHAMU Jinsi ya kupata namba ya NIDA (NIN)
- MATOKEO ya Marudio Mtihani darasa la saba 2022
- NECTA: Matokeo ya Darasa la nne 2022/2023
UONGOZI wa Klabu ya Singida Big Stars FC umewatoa hofu Mashabiki na Wanachama wake kwa kusisitiza kuwa Mshambuliaji Francis Kazadi Kasengu ni mali halali ya klabu hiyo, kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa mapema mwaka huu.
Kazadi amesajiliwa Singida Big Stars katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili akitokea Al Masry SC ya Misri, ambako hakuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara tangu aliposajiliwa mwaka 2020 akitokea Wydad Casablanca alikocheza jumla ya mechi 14 na kufunga mabao 9.
Uongozi wa Singida Big Stars Football Club umetoa taarifa za Mkataba kati yao na Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, kufuatia kuibuka kwa tetesi zilizodai kuwa Kazadi bado hajasaini mkataba na klabu hiyo, na yupo klabuni hapo kufanya majaribio.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Singida Big Stars Dismas Ten amesema kuwa taarifa zinazosambaa kuhusu Mkataba wa Kazadi na Klabu yao sio za kweli, na kilichopo ni kwamba Mshambuliaji huyo ni mali yao halali.
- NECTA: Matokeo ya Kidato cha Pili 2022/2023
- MATOKEO | Tazama Hapa Matokeo ya Darasa la Nne, Kidato Cha Pili na Cha Nne 2022/2023
- MATOKEO Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2023
“Kazadi ni mchezaji wetu halali tena ameshasaini mkataba na Klabu yetu, hizo taarifa sio sahihi kwa sababu zipo tofauti na kilichopo kisheria.”
“Katika hali ya kawaida huwezi kuwazuia watu kusema na kusema kwao kunakuja kwa hali nyingi, ninachokuhakikishia ni kwamba huyu ni mchezaji wetu wa halali na huko anapotajwa sio sahihi.”
“Watu wanapaswa kufahamu kwamba Singida Big Stars Football Club ni Taasisi inayofanya kazi zake kiutaratibu, kwa hiyo hili suala la usajili wa Kazadi lipo kiutaratibu, kwa hiyo ninataka kuweka wazi kuwa tunafanya kazi kwa kufuata weledi na hatubahatishi.” amesema Ten
Kazadi amekua gumzo kwenye Soka la bongo tangu usiku wa kuamkia leo, kufuatia kufunga mabao manne ya ushindi wa Singida Big Stars dhidi ya Azam FC, katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kwanza Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar 2023.
Mabao hayo manne yanamfanya Mshambuliaji huyo maarufu Zadio kufikisha jumla ya mabao matano (5) kwenye Michuano hiyo huku bao lake la kwanza akilifunga kwenye mchezo wa hatua ya Makundi dhidi ya Young Africans uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Kazadi ana uzoefu wa kucheza Fainali ya ligi ya Mabingwa Barani Afrika mwaka 2014 na Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2018 akiwa na AS Vita Club ya kwao DR Congo.
Matatizo yake ya hivi karibuni dhidi ya klabu yake ya Al Masry ya Misri yalimfanya awe nje ya dimba tangu August 2022.
- MSIMAMO wa Makundi Kombe la Mapinduzi 2023
- MAKUNDI na Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2023
- TETESI Usajili Ligi Kuu dirisha dogo la usajili 2022/2023
- MAJINA ya waliochaguliwa Kujiunga na VETA Tanzania 2023
- NECTA Matokeo ya Darasa la Saba 2022/2023
- MAJINA ya Wanafunzi na Shule walizochaguliwa form one 2023
- Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- Simba yapangwa kundi C CAF Champions League 2022/2023
- Yanga yapangwa kundi D CAF Confederation Cup 2022/2023
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.
Nipashe Michezo, Nijuze Michezo, Simba sc leo, Global Publishers michezo, saleh jembe michezo, Yanga leo, Shaffih dauda michezo, michezo, Magazeti, Usajili, Habari za Michezo, Nijuze Habari, Nijuze Michezo, Nijuze TV App, Nijuze TV LIVE, Nijuze Habari Michezo, Nijuze Habari Magazeti, Nijuze Habari Ajira, Nijuze Habari Usajili, Nijuze Habari Matokeo, Nijuze Habari Usajili, saleh jembe michezo leo,habari za michezo
leo 2023, habari za yanga za leo, habari za simba za leo, Habari za Michezo leo 2023.
The post Singida Big Stars yatoa ufafanuzi Usajili wa Kazadi Kasengu appeared first on Nijuze Mpya.
Post a Comment