Serikali yatangaza tarehe ya kuzima laini ambazo hazijahakikiwa

Serikali yatangaza tarehe ya kuzima laini ambazo hazijahakikiwa

Serikali yatangaza tarehe ya kuzima laini ambazo hazijahakikiwa

Serikali yatangaza tarehe ya kuzima laini ambazo hazijahakikiwa

Serikali yatangaza tarehe ya kuzima laini ambazo hazijahakikiwa

SERIKALI imetangaza kuzima laini zote zisizo hakikiwa itakapofika Februari 13, 2023. Siku moja kabla ya Valentine’s Day.Valentine’s Day ni siku maarufu ya wapendao duniani ambayo husherehekewa Februari 14 ya kila mwaka.

Ni sherehe inayotumiwa kuimarisha upendo kwa watu mbalimbali pia wandoa au wachumba.

Hayo yamesema leo Jumanne, Januari 24, 2023 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Amesema takwimu zilizopo hadi Januari 19, 2023 laini za simu zilizosajiliwa ni zaidi ya 60.7 milioni.

Laini hizi ndio zinatumika mitaani na zingine kutapeli watu kwa kutumiwa ujumbe wa ‘tuma kwenye namba hii.’

Nape amesema Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ilitoa taarifa ya kuwataka wananchi wote kuhakiki namba zao.

Kwa mujibu wa Nape tarehe ya mwisho ya uhakiki wa namba imeahirishwa mara kadhaa na leo ameahirisha badala ya kuzimwa Januari 31, 2023, lakini amesogeza hadi Februrai 13, 2023, siku moja kabla ya Siku ya Wapendanao Duniani.

“Tumeweka hivyo ili siku ya Wapendao ‘Valentine’s Day’ kusiwe na utapeli wa ‘tuma nauli kwenye namba hii,” amesema Nape.

Nape amesema tangu kuanza kampeni ya uhakiki wa namba za simu kutokana na wingi wa matukio ya utapeli ni namba zaidi 58.4 milioni ndio zimehakikiwa huku zaidi ya namba 2.3 milioni hazijahakikiwa hadi sasa.

“Tunazitafuta hizi milioni mbili ziko wapi, ndio zinazofanya utapeli mitaani. Ni namba ambazo zimesajiliwa, lakini hazijahakikiwa,” amesema.

Nape amesema Serikali ilipoanza kampeni ya kusajili namba zote za simu kwa teknolojia ya alama za vidole, lengo lilikuwa kupambana na utapeli.

Amesema kampeni hiyo ilianza Mei Mosi, 2019 na kumalizika Desemba 2021, na zile zilizokuwa hazijasajiliwa zilizimwa.

Hata hivyo, amesema kulikuwa na ujanja unaofanywa na wanaosajili laini za simu kutumia kitambulisho cha Taifa cha mtu mwingine kusajili namba zingine za simu na hizo ndio wanazitafuta.

“Kuna wale ambao hawajapata vitambulisho vya Nida na wametumia vitambulisho vya jamaa zao kusajili laini zao, waende kwa waliotumia vitambulisho vyao kuhakiki namba zao.

“Waende wakaongee nao, wakubaliane, kama atakubali atoe hizo taarifa zinazotakiwa kwenye kuhakiki laini, kwa kuwa ikitumika kufanya uhalifu atakaekamatwa ni mwenye kitambulisho,” amesema Nape.

Katika hatua nyingine Waziri huyo ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan haridhishwi na hali ya Waandishi wa habari nchini hivyo kutaka tathimini ya kina kufanyika kuhufu namna ya kuondoa changamoto zilizopo.

Kutokana na hayo amesema Wizara yake imefanya mazungumzo na kuunda Kamati ya watu tisa kutathmini
hali ya vyombo vya habari kiuchumi na kiutendaji.

Amewataja wanakamati hao kuwa “Mwenyekiti wa Kamati Tido Mhando ambaye ni Mtendaji Mkuu Azam Media Group,Katibu wa Kamati Gerson Msigwa Mkurugenzi idara ya habari Maelezo na msemaji wa Serikali huku wajumbe wakiwa ni Bakari Machumu, Joyce Mhavile, Richard Mwaikenda, Dk.Rose Rueben, Kenneth Simbaya , Sebastian Maganga na Jackline Woiso”.

Waziri Nape amefafanua kuwa Kamati hiyo itafanya kazi ya kuchakata taarifa kwa kina na kutumia nafasi hiyo kuwaomba Waandishi wa habari kutoa ushirikiano na kutoa maoni Kwa njia ya mtandao bila kulazimu mtu kusafiri na kwamba itafanya kazi ndani ya muda wa miezi mitatu ili kukwamua tasnia ya habari.

“Vile vile Kamati itafanya kazi ya kukusanya taarifa za waandishi wa habari walioajiriwa,Wenye mikataba ,vipato vyao ,wawakikishi mikoani ikiwa ni pamoja na kupendekeza njia bora za kukabiliana na changamogo hizo,”amesisitiza.

Kwa upande wake Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wanahabari kwa kufanya kazi kwa bidii kipindi chote cha mwaka uliopita huku akiwata kuendelea kuchapa kazi kwa uzalendo na kujitolea kwa manufaa ya Taifa.

“Mwaka jana tulishuhudia uzalendo wa hali ya juu,hakukuwa na habari zinazotugawa wala chuki na huu ndiyo uzalendo tunaoutaka,nichukue fursa hii kuwataka Waandishi wa habari kuendelea kufanya kazi kwa kufuata misingi na maadili ya uandishi wa habari,”amesema.

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.

Nipashe Michezo, Nijuze Michezo, Simba sc leo, Global Publishers michezo, saleh jembe michezo, Yanga leo, Shaffih dauda michezo, michezo, Magazeti, Usajili, Habari za Michezo, Nijuze Habari, Nijuze Michezo, Nijuze TV App, Nijuze TV LIVE, Nijuze Habari Michezo, Nijuze Habari Magazeti, Nijuze Habari Ajira, Nijuze Habari Usajili, Nijuze Habari Matokeo, Nijuze Habari Usajili, saleh jembe michezo leo,habari za michezo
leo 2023, habari za yanga za leo, habari za simba za leo, Habari za Michezo leo 2023.

The post Serikali yatangaza tarehe ya kuzima laini ambazo hazijahakikiwa appeared first on Nijuze Mpya.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post