SAMATTA Kurejea Ligi Kuu Bara
Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Ally Samatta ameweka wazi mpango wake wa kurejea kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara, kabla ya kustaafu Soka.
Samatta amesema kuwa katika maisha yake ya Soka hakupata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu nchini Tanzania, hivyo anatamani kutumia nafasi hiyo kulijua vizuri Soka la Bongo.
Akizungumza na Salama Jabir kwenye kipindi cha Salama Na, Samatta amesema kuwa anataka kujenga mahusiano na ukaribu na watu wa nyumbani kwa kuwa muda mwingi amekua akicheza Soka lake nje ya nchi.
“Mipango yangu ni kuja kumalizia mpira wangu hapa nyumbani, kama ambavyo watu wanajua kuwa sijacheza kwa muda mrefu soka la nyumbani.”
“Nitarudi kucheza ili kujenga mahusiano na watu pamoja na kulijua vizuri soka la nyumbani, na hii ninataka kuwaambia watu wasifikirie kuwa nitarudi kwenye timu yangu ya zamani, hapana, ninaweza kucheza timu yoyote.”
“Siyo lazima ziwe timu hizo kubwa (Young Africans na Simba SC) nitacheza timu yoyote, ili mradi niwe nimerudi nyumbani na kutimiza dhamira yangu ya kujua vizuri ladha ya soka letu la Tanzania.” amesema Samatta
Kabla ya kutimkia TP Mazembe Samatta aliichezea Simba SC iliyomsajili kutoka African Lyon iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kipindi hicho.
Mbali na TP Mazembe aliyoichezea kwa mafanikio makubwa Barani Afrika, Samatta amecheza soka Barani Ulaya akiwa na Klabu za KRC Genk (2016–2020) na kufanikiwa kufunga mabao 43 katika michezo 101 aliyocheza.
Msimu wa 2020–2021 alisajiliwa na Aston Villa ya England aliyoitumikia katika michezo 14 na baadae alitimkia Uturuki kujiunga na Fenerbahçe (2020–2021).
2021–2022 alitolewa kwa mkopo Antwerp ya Ubelgiji akicheza michezo 27 na kufunga mabao 5 tu kabla ya kurejea KRC Genk mapema mwaka huu.
- MATOKEO | Tazama Hapa Matokeo ya Darasa la Nne, Kidato Cha Pili na Cha Nne 2022/2023
- MAKUNDI na Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2023
- TETESI Usajili Ligi Kuu dirisha dogo la usajili 2022/2023
- MAJINA ya waliochaguliwa Kujiunga na VETA Tanzania 2023
- NECTA Matokeo ya Darasa la Saba 2022/2023
- MAJINA ya Wanafunzi na Shule walizochaguliwa form one 2023
- Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- Simba yapangwa kundi C CAF Champions League 2022/2023
- Yanga yapangwa kundi D CAF Confederation Cup 2022/2023
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.
Nipashe Michezo, Nijuze Michezo, Simba sc leo, Global Publishers michezo, saleh jembe michezo, Yanga leo, Shaffih dauda michezo, michezo, Magazeti, Usajili, Habari za Michezo, Nijuze Habari, Nijuze Michezo, Nijuze TV App, Nijuze TV LIVE, Nijuze Habari Michezo, Nijuze Habari Magazeti, Nijuze Habari Ajira, Nijuze Habari Usajili, Nijuze Habari Matokeo, Nijuze Habari Usajili, saleh jembe michezo leo,habari za michezo
leo 2023, habari za yanga za leo, habari za simba za leo, Habari za Michezo leo 2023.
The post SAMATTA Kurejea Ligi Kuu Bara appeared first on Nijuze Mpya.
Post a Comment