Metacha arejea Yanga, aomba radhi
KLABU ya Yanga imethibitisha kumsajili mlinda lango wao wa zamani Metacha Boniface Mnata ambaye ametua kwa mkopo hadi mwisho wa msimu kutoka klabu ya Singida Big Stars.
Metacha anajiunga na Yanga kuongeza nguvu langoni baada ya golikipa nambari mbili wa Klabu hiyo, Aboutwalib Mshery kupata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu.
Kuelekea Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya Makundi Klabu ya Young Africans inahitaji kuwa imara katika kila eneo ndiyo sababu ya kumsajili Mnata ambaye atasaidizana na Djigui Diarra kuhakikisha lango la Yanga linakuwa imara.
Baada ya kutambulishwa Metacha Mnata amewaomba radhi Mashabiki na Wanachama wa Young Africans.
Kabla ya kurejea Yanga Metacha alisajiliwa na Singida Big Stars mwanzoni mwa msimu huu kutoka Polisi Tanzania alikosajiliwa kutoka Yanga.
Metacha amelazimika kuomba radhi kufuatia utovu wa nidhamu alioufanya kabla ya kuondoka Yanga misimu miwili iliyopita.
Metacha ameomba radhi dakika chache baada ya kukamilisha uhamisho wake usiku wa kuamkia leo na kusema: “Ninayofuraha kubwa ya kuwajulisha nimepata nafasi ya kurudi tena kwenye klabu niipendayo ya Young Africans, nikiwa kama mpambanaji hapo nyuma lakini nilifanya makosa kwa hiyo ninaomba mnisamehe na mnipokee.”
“Ninaahidi kuwa Metacha wa sasa sio yule aliyekuwepo hapo nyuma, ninaahidi nitapambana kwa moyo mmoja na kwa ari kubwa, ili nihakikishe timu inapata matokeo, ninawaahidi nitafanya vizuri na nitakuwa bora zaidi.”
Metacha Mnata alionesha utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu msimu wa 2020/2021 dhidi ya Ruvu Shooting, Baada kwa kuwaonesha ishara ya Kidole cha Kati Mashabiki wa Young Africans, ambao walimbeza kwa kiwango chake kwenye mchezo huo.
Kufuatia kosa hilo, Kamati ya Saa 72 ya Ligi Kuu Tanzania Bara ilitangaza kumfungia Metacha, michezo mitatu na kutozwa faini ya Shilingi laki tano (500,000).
- YANGA yamtambulisha Kennedy Musonda
- MATOKEO ya droo raundi ya 32 na 16 Bora ASFC 2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- NECTA: Matokeo ya Darasa la nne 2022/2023
- NECTA: Matokeo ya Kidato cha Pili 2022/2023
- TETESI Usajili Ligi Kuu dirisha dogo la usajili 2022/2023
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- Simba yapangwa kundi C CAF Champions League 2022/2023
- Yanga yapangwa kundi D CAF Confederation Cup 2022/2023
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
DONWLOAD NIJUZE TV HAPA SISI kwetu Michezo ndiyo Furaha YETU.
Nipashe Michezo, Nijuze Michezo, Simba sc leo, Global Publishers michezo, saleh jembe michezo, Yanga leo, Shaffih dauda michezo, michezo, Magazeti, Usajili, Habari za Michezo, Nijuze Habari, Nijuze Michezo, Nijuze TV App, Nijuze TV LIVE, Nijuze Habari Michezo, Nijuze Habari Magazeti, Nijuze Habari Ajira, Nijuze Habari Usajili, Nijuze Habari Matokeo, Nijuze Habari Usajili, saleh jembe michezo leo,habari za michezo
leo 2023, habari za yanga za leo, habari za simba za leo, Habari za Michezo leo 2023.
The post Metacha arejea Yanga, aomba radhi appeared first on Nijuze Mpya.
Post a Comment