Tetesi za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa December 23 2022
Tetesi za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa December 23 2022, Kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham anapendelea kujiunga na Real Madrid kutoka Borussia Dortmund, licha ya Liverpool, Manchester City na Manchester United kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.(AS – kwa Kihispania)
Benfica imekataa ofa ya euro milioni100 (£88m) kutoka kwa klabu ambayo haijatajwa jina kwa ajili ya kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool na Real Madrid, na haitamuuza kwa chini ya euro milioni 120 mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 (£106m). (Record – kwa Kireno)
Real Madrid wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Italia Manuel Locatelli, 24, ambaye yuko kwa mkopo Juventus kutoka Sassuolo, ikiwa watamkosa Bellingham au Fernandez. (AS – kwa Kihispania)
Chelsea wamefikia mkataba wa euro milioni12 (£10.5m) na Molde ili kumsaini mshambuliaji wa Ivory Coast David Datro Fofana, 20. (Fabrizio Romano).
Mlinda mlango wa Chelsea na Senegal Edouard Mendy, 30, amepuuzilia mbali mkataba mpya wa miaka sita Stamford Bridge kwa sababu anaamini kuwa klabu hiyo haimuonyeshi “heshima” ya kutosha linapokuja suala la mshahara. (Sun)
Afisa mkuu mtendaji wa Shakhtar Donetsk Carlo Nicolini amethibitisha kuwa Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ukraine Mykhailo Mudryk, 21. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)
Arsenal wanajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 27, ambaye kandarasi yake itamalizika Juventus msimu wa joto. (Repubblica, via Mail)
Arsenal bado hawajaamua iwapo watamruhusu mlinzi wa Ureno Cedric Soares kuondoka mwezi Januari, huku Fulham wakiongoza mbio za kumsaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye pia anawavutia Bayer Leverkusen na Villarreal. (Evening Standard)
Mshahara wa kila wiki wa Soares wa karibu £75,000 umekuwa kizingiti. (Sun)
Tetesi za Usajili Barani Ulaya Jana Alhamisi December 22 2022.
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi amekubali mkataba wake na klabu ya Paris St-Germain kuongezwa kwa mwaka mmoja katika hatua mbayo itamfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 kusalia na mabingwa hao wa Ufaransa hadi majira ya joto 2024. (Le Parisien – kwa Kifaransa).
PSG haitamruhusu mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, kuondoka mwezi Januari kwani inapania kumuuza msimu wa joto kwa bei inayofaa. (Ben Jacobs, Twitter)
Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone amechochea mazungumzo kwamba mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 23, anauzwa kwa kusema “hakuna mtu wa muhimu” katika klabu hiyo. (Goal)
Arsenal ilimtaka mlinzi wa Argentina Lisandro Martinez msimu wa joto lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliamua kuungana na mkufunzi wa zamani wa Ajax Erik ten Hag katika klabu ya Manchester United. (VI via Manchester Evening News)
Chelsea wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua kiungo wa kati wa Vasco da Gama raia wa Brazil Andrey Santos, 18. (Fabrizio Romano).
Manchester United wana nia ya kumsajili mlinda mlango wa Aston Villa Emiliano Martinez, 30, ambaye alichangia pakubwa kuisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia. (Football Insider)
Ofa ya Al-Nassr ya kandarasi ya pauni milioni 160 kwa mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, inaungwa mkono na serikali ya Saudi Arabia. (Ben Jacobs via Express)
Klabu ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani imedai kuwa ilipewa nafasi ya kumsajili Ronaldo na Manchester United kabla ya kuondoka Old Trafford. (DAZN, via Mail)
Meneja wa Barcelona Xavi amemshawishi nahodha wake, kiungo wa kati wa Uhispania Sergio Busquets, 34, kusalia katika klabu hiyo hadi msimu wa joto, badala ya kushinikiza kuhamia Ligi Kuu ya Soka mwezi Januari. (Sport – kwa Kihispania)
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- Simba yapangwa kundi C CAF Champions League 2022/2023
- Yanga yapangwa kundi D CAF Confederation Cup 2022/2023
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
- PATA bonasi hadi 230000 na Helabet Tanzania
- JINSI ya kuweka Pesa Helabet Tanzania
- Jinsi ya kujisajili na HELABET Tanzania
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Donwlod HAPA SISI kwetu Michezo ndo Furaha yetu.
Nipashe Michezo, Nijuze Michezo, Simba sc leo, Global Publishers michezo, saleh jembe michezo, Yanga leo, Shaffih dauda michezo, michezo, Magazeti, Usajili, Habari.
The post Tetesi za Usajili Barani Ulaya Leo Ijumaa December 23 2022 appeared first on Nijuze Mpya.
Post a Comment