MAKALA: Zifahamu Sheria 17 za Mpira wa Miguu.
MAKALA: Zifahamu Sheria 17 za Mpira wa Miguu, Mpira wa Miguu (pia Soka au Kandanda) ni mchezo unaochezwa na jumla ya wachezaji ishirini na wawili katika timu mbili, kila timu ikiwa na wachezaji kumi na mmoja.
- NECTA Matokeo ya Darasa la Saba 2022/2023
- MAJINA ya Wanafunzi na Shule walizochaguliwa form one 2023
- KOMBE la Dunia LIVE Kwenye Nijuze Habari APP
Lengo hasa la mchezo huu ni wachezaji kuumiliki mpira kwa kutumia miguu na kufunga goli, yaani kuuingiza mpira katika wavu wa wapinzani mara nyingi zaidi.
Matumizi ya mikono ni marufuku isipokuwa kwa mlinda mlango katika eneo maalumu na wakati wa kurudisha mpira baada ya kutoka nje ya uwanja.
Soka ndiyo mchezo unaopendwa zaidi Duniani, na unachezwa kwa kufuata kanuni kadhaa maarufu kama sheria za mchezo.
Mchezo wa soka unasimamiwa kimataifa na shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA, linaloandaa Kombe la Dunia kwa wanaume na wanawake kila baada ya miaka minne.
Kombe la Dunia la FIFA limefanyika kila baada ya miaka minne tangu mwaka 1930 ukiacha mashindano ya 1942, na 1946, yaliofutwa kwa sababu ya vita vikuu vya dunia.
- Msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- Simba yapangwa kundi C CAF Champions League 2022/2023 tazama droo kamili hapa
- Mstari mrefu pembeni mwa Uwanja Unaoashiria mwisho Wa Uwanja .
- Mstari mrefu wa Katikati Unaogawa Uwanja katika pande 2 Zilizolingana katikati ya Uwanja kuna mduara wenye nusu kipenyo cha mita 9.15.
- Mstari mrefu Upande wa goli Unaoashiria mwisho Wa Uwanja upande Wa goli .
- Pia kuna nusu duara katika makutanio ya Mstari Wa pembeni na Mstari Wa goli ambapo huitwa Kona .
- Utofauti Wa Kipenyo na Uzito Wa mpira Wa miguu hutegemea Uwezo ama rika la Mchezaji au watumiaji .
- Mwamuzi ndiye anayeongoza mchezo na Kutafsiri sheria wakati wa mchezo, hutoa maamuzi ndani ya Kipindi cha mchezo na kutoa taarifa ya mchezo husika .
- Ndiye msemaji au mwamuzi wa mwisho pale inapobainika kwamba Sheria ya mchezo imekiukwa kwa namna yeyote ili ikiwa ni pamoja na kutoa adhabu pindi mchezaji anapofanya Kosa ndani ya Uwanja .
- Humsaidia mwamuzi mkuu kuhusu matukio yanayotendeka nje na ndani ya Uwanja.
- Idadi ya waamuzi wasaidizi hutegemea mashindano au mchezo husika, waamuzi hao hutambulika kama washika vibendera namba 1&2 na Kamisaa wa mchezo anayetunza kumbukumbu.
- Pia mashindano mengine huruhusu waamuzi wakae nyuma ya goli mfano UEFA Champions League .
Kwa kawaida Mpira wa Miguu huchezwa kwa dakika 90, katika vipindi viwili yaani dakika 45 kwa kila kipindi, baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza cha mchezo, mchezo husimama (mapumziko) kwa muda usiopungua dakika 10 na
Usiozidi 15.
- Pia Kama muda Wa nyongeza dk 30′ utaongezwa kwa lengo la kumpata mshindi, timu zitapumzika kwa dakika 5, tu baada ya dakika 15 za kipindi cha kwanza katika dakika 30 za nyongeza (Extra time ) na kipenyo kisha kubadilishana magoli tayari kwa kumalizia kipindi cha 2 Ila muda waweza kupunguzwa kwa makubaliano ya timu husika .
- Mchezo huanzishwa tena baada ya goli kufungwa na baada ya kosa kutendeka na mwamuzi akapuliza Filimbi au kama mpira ukatoka nje au mchezaji kuumia n.k.
- Yanga yapangwa kundi D CAF Confederation Cup 2022/2023 tazama droo kamili hapa
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- Pia mpira Utakuwa ndani ya mchezo kama uko ndani ya Uwanja na Unaendelea Kuchezwa .
- Pia goli litahesabiwa kama mpira utavuka mstari chini ya uwanja au ukiwa hewani na likaonekana ukavuka mstari wa goli .
- Mchezaji anaweza akawa katika nafasi ya kuotea lakini asitafsiriwe kama ameotea kama hajajishughulisha kabisa na mpira.
- Dhana ya kuotea hutegemea mambo matatu muhimu ambayo ni nafasi, kucheza na kutoa .
- Pia mchezaji hatakuwa ameotea ikiwa walinzi wa timu pinzani watamkimbia au kutojishughulisha kabisa pale mchezaji wa timu pinzani atakapo pokea mpira na kufunga goli .
- Mchezaji hatatafsiriwa kama ameotea akiwa amepasiwa na mchezaji wa timu pinzani kwa kujua au kutokujua .
- Pia ikiwa mchezaji yuko katika nafasi ya kuotea na mwenzake mwenye mpira akapiga mpira golini moja kwa moja bila kumpasia mpira huyo aliyeko katika nafasi ya kuotoe na kufunga goli hapo mwamuzi ataruhusu goli bila kutafsiri Kuotea.
- Mchezaji atakuwa ameotea iwapo mpira utapigwa golini ukagonga mlingoti mojawapo wa goli au mlinda mlango na kurudi ndani ya Uwanja na kuguswa na mchezaji aliyekuwa katika nafasi ya kuotea.
- Aidha hakutakuwa na dhana ya kuotea pale mchezaji atakapokutana na mpira uliochezwa na mlinda mlango .
- Mpira wa kurushwa hauna kuotea, pia mchezaji hatakuwa ameotea endapo atapokea mpira katika eneo lake kabla hajavuka mstari wa katikati ya Uwanja .
- Makosa atendayo mchezaji anaweza kuonywa kwa kadi ya njano au nyekundu na kutolewa nje ya Uwanja .
- kwa kawaida makosa yanayoonywa kwa kadi ya manjano ni kama Vile kushika na kuunawa mpira bila kukusudia, Kumsukuma mchezaji wa timu pinzani katika hali ya kutaka kuchukua mpira.
- Kupoteza muda, kumvuta au kumshika mchezaji wa timu pinzani wakiwa katika hali ya kucheza mpira.
- Makosa ya kadi nyekundu ni kama vile , kutukana, kupigana, kucheza rafu kwa nyuma, kukaba kwa nguvu kwa kunyoosha miguu mmoja au yote miwili mbele wakati mchezaji mwingine anataka kupokea mpira au kucheza N.K
KWA MUJIBU WA SHERIA HII
- Mchezaji atakayeonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja atakosa mechi 3.
- Mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano 2 katika mchezo mmoja atatolewa kwa kadi nyekundu na kukosa mchezo mmoja.
- Mchezaji akionyeshwa kadi za njano katika michezo 5 ndani la Ligi moja au mashindano atakosa mechi 1, kadi 10 atakosa michezo miwili na kadi 15 atakosa michezo mitatu.
- Endapo mchezaji atafikisha kadi za njano 20 katika msimu mmoja, basi kamati ya maadili ya wachezaji itakaa na kuamua adhabu kwa mchezaji huyo .
- Wakati mpira unapigwa golini, wachezaji wengine wanatakiwa kuwa katika umbali jsiopungua mita 9.15 au hatua zisizopungua 10 kutoka pale mpira ulipo .
Ni kitendo cha mpira kutengwa kwenye kisanduku cha meta 12 kutoka goli, pigo la penati linawahusisha wachezaji wawili tu, mpigaji na mlinda mlango na wachezaji wengine wrote wanatakiwa kuwa nje ya 18.
- Kuna aina 2 za pigo la penati ambazo ni penati ndani ya muda wa mchezo yaani ndani ya dakika 90, na pigo la penati baada ya muda wa mchezo ambalo linalenga kutafuta mshindi Wa mchezo mara baada ya timu zote kutoshana nguvu ndani ya dakika za mchezo.
- Mpiga penati ndani ya muda Wa mchezo hufanya mambo mawili ambayo ni Kupiga mpira golini moja kwa moja au kumtengea mwenzake aliye nje ya 18.
- Mpigaji wa penati anaruhusiwa kuucheza tena mpira uliorudi ndani ya hwanja baada ya mlinda mlango kuucheza na hatoruhusiwa kuucheza endapo utagonga mlingoti na kurudi uwanjani.
- Hauhusiani na GoaL Kick na utarushwa kuelekea lango la aliyeutoa.
- Katika upigaji wa kona mchezaji anaweza kupiga moja kwa moja au kuanza kwa kupasia mwenzie.
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
- PATA bonasi hadi 230000 na Helabet Tanzania
- JINSI ya kuweka Pesa Helabet Tanzania
- Jinsi ya kujisajili na HELABET Tanzania
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Donwlod HAPA SISI kwetu Michezo ndo Furaha yetu.
Nipashe Michezo, Nijuze Michezo, Simba sc leo, Global Publishers michezo, saleh jembe michezo, Yanga leo, Shaffih dauda michezo, michezo, Magazeti, Usajili, Habari.
MAKALA: Zifahamu Sheria 17 za Mpira wa Miguu
The post MAKALA: Zifahamu Sheria 17 za Mpira wa Miguu appeared first on Nijuze Mpya.
Post a Comment