YANGA yaingia Mkataba na UNICEF October 18 2022
KLABU ya Young Africans SC imeingia mkataba wa miezi sita na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto – UNICEF unaolenga kuongeza uelewa kwa Umma kuhusu Chanjo ya UVIKO-19 na kutoa Elimu kuhusu virusi vya EBOLA.
Yanga na UNICEF zimeingia mkataba huo Leo Jumanne October 18 2022, ambapo September 20, 2022 serikali ya Uganda ilitangaza rasmi mlipuko wa virusi vya Ebola katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo.
Ni heshima kubwa kuingia mkataba na UMOJA WA MATAIFA. Ni kwa mara ya kwanza katika historia kwa Vilabu vya hapa Afrika Mashariki.
Ushirikiano na UNICEF umejengwa katika falsafa ya Klabu yetu ya kusaidia jamii.
“Tunajulikana kama timu ya Wananchi. Falsafa yetu ni kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili Wananchi,” amesema Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said baada ya kusaini mkataba huo.
Naye Mtendaji Mkuu wa Young Africans SC, Andre Mtine amesema kuwa Leo ni Siku ya Kihistoria kwa Klabu hiyo kuingia Mkataba Mkubwa na Shirika Kubwa Duniani la UNICEF.
Yanga imesema kuwa itashirikia na UNICEF ili kila Mwanachama, Mpenzi na Shabiki wa Young Africans SC pamoja na Vilabu vingine apate/wapate maarifa na uelewa kuhusu chanjo ya UVIKO-19.
“Ni jukumu letu kama Klabu kuunga mkono juhudi zitakazotuwezesha kushinda UVIKO-19 na EBOLA,” amesema Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said alisisitiza.
The post YANGA yaingia Mkataba na UNICEF October 18 2022 appeared first on Nijuze Mpya.
Post a Comment