YANGA yafunguka ishu ya Nabi kuondoka

YANGA yafunguka ishu ya Nabi kuondoka

YANGA yafunguka ishu ya Nabi kuondoka

YANGA yafunguka ishu ya Nabi kuondoka

YANGA yafunguka ishu ya Nabi kuondoka

UONGOZI wa Klabu ya Young Africans SC umetoa taarifa njema kwa Mashabiki na Wanachama wake kuwa Nasreddin Nabi, bado ni kocha Mkuu wa Klabu hiyo yenye makazi yake Mtaa wa Jangwani Jijini Dar es Salaam.

Nabi alijiunga na Yanga SC April, 2021 na amekuwa na rekodi nzuri ya kuiongoza timu hiyo kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita wa 2021/2022 bila kupoteza.

Akizungumza Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine amewaomba Mashabiki na Wanachama wa Yanga kufatilia taarifa za uhakika za timu yao kupitia vyanzo rasmi vya habari vya klabu.

“Niwaombe mashabiki na wanachama wetu kuwa na utaratibu wa kufatilia taarifa za klabu yetu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari”.

Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba SC juzi October 24, 2022 Wananchi walofikisha mechi 43 za Ligi Kuu ya NBC bila kupoteza, sawa na siku 546 za mechi za Ligi Kuu ya NBC bila wapinzani wao kuondoka na ushindi mbele yao.

Mara ya mwisho Yanga SC kupoteza mchezo wa Ligi ilikuwa dhidi ya Azam FC kwa bao la Prince Dube, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam April 25, 2020.

Kwenye mechi hizo 43 za Ligi Kuu Yanga imefanikiwa kufunga mabao 72, ikiruhusu mabao 15 tu na kutoka bila kuruhusu bao lolote kwenye michezo 29, ushindi mara 33 na kutoka sare michezo 10.

Miongoni mwa vigogo wa Afrika ambao wanashikilia rekodi ya kucheza michezo mingi bila kupoteza ni pamoja na ASEC Mimosas ambayo ni klabu ya zamani ya Aziz Ki iliyocheza michezo 108 bila kupoteza tokea mwaka 1989 mpaka 1994.

Wengine ni Esperance de Tunis waliocheza michezo 85 bila kupoteza kwenye Ligi Kuu ya Tunisia tokea mwaka 1997 mpaka mwaka 2001 ambapo walipokonywa ushindi mechi ya 86 baada ya kuvunja kanuni ya kumchezesha mchezaji asiyeruhusiwa kwenye ushindi wao wa magoli 6 dhidi ya Dejrba.

Al Ahly wao pia wanashikilia rekodi ya kucheza michezo 45 ya Ligi Kuu ya nchini Misri ambapo, rekodi ilivunjwa na mchezaji wao wa zamani John Antwi ambapo wakati huo alikuwa anaitumikia Misr El Maqsa.

Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Tunashikilia nafasi ya tatu kwa kucheza Michezo Mingi bila kupoteza, Michezo 43, ikisalia michezo mitatu tu kufiki rekodi ya Al Ahly.

The post YANGA yafunguka ishu ya Nabi kuondoka appeared first on Nijuze Mpya.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post