RATIBA ya Safari ya Yanga Kuelekea Sudan

RATIBA ya Safari ya Yanga Kuelekea Sudan

RATIBA ya Safari ya Yanga Kuelekea Sudan

Yanga vs Al Hilal October 16 2022 CAF Champions League 2022/2023, Young Africans vs Al Hilal Omduraman October 16 2022, Young Africans vs AL-Hilal Omduraman, Yanga vs Al-Hilal CAF Champions League.

RATIBA ya Safari ya Yanga Kuelekea Sudan

RATIBA ya Safari ya Yanga Kuelekea Sudan

MSAFARA wa Wachezaji 25, Benchi la Ufundi 11, Viongozi na Mashabiki 15 wa Yanga SC wanatarajia kusafiri Jumamosi ya October 15, 2022 kuelekea Sudan kwaajili ya Mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal Omduraman.

Klabu hiyo itaondoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar Es Salaam, Majira ya saa 10:00 Alfajiri kwa Shirika la ndege ya Ethiopia na itatua Sudan, saa 6:40 mchana kwa saa hapa Tanzania (Sudan itakuwa ni saa 11:40 asubuhi).

“Tumepishana muda na Sudan, sisi tuko mbele kwa saa moja, hivyo tutatua Sudan asubuhi lakini kwa saa za hapa Tanzania itakuwa mchana. Kila kitu kipo sawa mpaka sasa kwa upande wa maandalizi,” amesema Mkurugenzi wa mashindano wa Yanga, Saad Kawemba.

Baada ya Mapumziko, Kikosi Cha Kitafanya Mazoezi saa 2:00 usiku kwa saa za Sudan, sawa na saa 3:00 usiku kwa saa za Tanzania, kwenye uwanja wa Al Hilal utakaotumika siku ya Mchezo October 16,2022.

“Tutafanya mazoezi kwenye Uwanja tutakaotumia kwaajili ya mechi na tutatumia muda ule ule wa saa 2:00 usiku kwa saa za Sudan, ambao ni ndio muda mechi itachezwa,” aliongeza Kawemba.

Baada ya mchezo, timu itarejea nchini Tanzania October 17, 2022 kwa Shirika la Ndege la Ethiopia, Majira ya saa 9:30 usiku kwa saa za Sudan na kutua nchini Tanzania saa 6:45 mchana kwa saa za Tanzania.

Nijuze Habari kupitia nijuzehabari.co.tz tutakuletea moja kwa moja Matokeo ya mchezo huo (Live Updates) pamoja na Kikosi kitakachoanza mapema iwezekanavyo.

The post RATIBA ya Safari ya Yanga Kuelekea Sudan appeared first on Nijuze Mpya.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post