WAVAMIZI Mo Simba Arena wapewa siku 60
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala ameagiza watu waliovamia eneo la Uwanja wa Mo Simba Arena kuondoka ndani ya miezi miwili (siku 60) kuanzia jana September 14 2022.
Hatua hiyo ya uvamizi imesababisha kuchelewa kwa ujenzi wa uwanja huo kupitia fedha zilizochangwa na mashabiki wa Klabu hiyo.
Makala ametoa kauli hiyo ya kuwaondoa wavamizi hao na kuongeza kuwa eneo hilo ambalo Simba ilipewa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete chini ya Mwenyekiti wake wakati huo Hassan Dalali na hati zote halali za serikali.
Makala ameongeza kuwa mmiliki wa eneo lazima uwe na hati ili utambulike na serikali lakini watu wamevamia eneo bila woga na kujenga hivyo wanatakiwa kuondoka kwa muda niliopa.
“Kuvamia eneo ni uhalifu kama uhalifu mwingine, hili ni eneo la Simba na walipewa na Rais mstaafu Dk. Kikwete, kwa hiyo waliovamia nawapa siku 60 kuanzia leo (Jana September 14 2022) kuhakikisha wanaondoka.
“Leo ni Septemba 14 (Jana) nitakuja November 13 kuangalia zoezi hili limefikia wapi,” alisema Mh. Makala.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amesema fedha yote zaidi ya milioni 150 iliyochangwa kwenye zoezi la nani zaidi zitatumika kufanikisha ujenzi huo.
Mwakilishi wa Mkandarasi Mega Woodcraft (T) Ldt Jonathan Kibona amesema vifaa vya vipo tayari na ujenzi utakamilika ndani ya miezi ndani ya miezi miwili na nusu.
“Zoezi lilichelewa sababu kulikuwa na uvamizi lakini baada ya maelekezo ya Mkuu wa Mkoa na vifaa vipo tayari ndani ya miezi miwili na nusu uzio madhubuti utakuwa tayari,” alisema Kibona.
The post WAVAMIZI Mo Simba Arena wapewa siku 60 appeared first on Nijuze Mpya -| Pata Habari zote za Michezo kitaifa na Kimataifa, Tetesi na Usajili, Magazeti ya Michezo, Ratiba na Matokeo, Mahusiano Pamoja na Nafasi za Kazi.
Post a Comment