RIWAYA:UKANDA WA GAZA
MWANDISHI :NELSON NTIMBA.
MTUNZI#2BETADAISOPIA.
Simu:0656353765.
UKANDA WA GAZA
TOLEO LA KWANZA.
*******CHUI MWEUSI*******
Risasi ya kwanza ilinikwaruza kwenye bega langu la kushoto lakini haikunizuia kuendelea kukimbia maana uhai wangu ulikuwa ni bora lakini kilicho kuwa bora kuliko yote ni kufikisha ripoti ya siri ikiwa salama.
Kadri nilivyo kuwa na kimbia ni kama nilikuwa napoteza muda tu maana na wao walizidi kunikimbiza bila hata kuchoka.Risasi nyingine mbili zilipita karibu na sikio langu la kashoto na kunifanya nihisi joto la haja.Lakini sikujaribu kujionea huruma maana katika muda nilio kuwa nimebaki nao haukuwa rafiki kwangu kuendelea kupambana na wasaka uhai.Kila mahali niliko pita kwenye msitu huu nyasi na miti zilibaki zinaskitika maana nilikuwa nimeloa damu na kuchafuka haswa kwa damu.
Kamwe sikuupa nafasi msemo usemao mbio za sakafuni uhishia ikingoni.Kichwani nilijipatia methali mwenyewe "Mbio ndefu uhitaji pumzi ya kutosha" nilianza kurejezea kumbukumbu nzuri na kuzifuta mbaya ambazo zilikuwa zimenichafulia jina langu.Sikufaha tena kuitwa jasusi maana dunia ilisha niona gaidi.Vyombo vya habari vya magharibi vilisha nizika katika kumbukumbu. Sikuwa na cha kujivunia tena kama shujaa zaidi ya akili yangu kuchagua mwenyewe nitakavyo kuwa.
Hatimaye nilipaswa kutetea uhai wangu na uhuru wangu kwa mara nyingine na nilipaswa kuua ama kukimbia mbio zisizo hishia sakafuni maana msemo huo kwangu kamwe sijawahi kuupa nafasi hata ya kuazima sembuse utokee mbele yangu lazima niusukume uende mbali nami.
Sauti ya bunduki aina ya IWI X95 TAVOR SMG ndiyo ilikuwa ikinipa wakati mgum maana ilikuwa na nguvu nyingi hata kukoswa koswa kwa risasi niliona nashambuliwa kizembe sana maana mi nikiwa na hata gobore lazima nipate shabaha lakini hawa askari tena walio kuwa na vyeo vya ukomandoo wananikosa kwa mara nyingi hili hali wana siraha hatari. Niliwaona ni wazembe wa kazi maana kama niliweza kuwatoroka kwa wepesi vile sasa nikiwa mtaani wataniweza?
Hatimaye mbio zangu ambazo kamwe sikupenda zihitwe mbio za sakafuni zilifika karibu na mto mkubwa ambao hadi leo sikupata kujua jina lake lilimaanisha kitu gani zaidi ya kuwa mto maarufu ambao umebeba historia ya nchi ya Israel mto Efrati.
Lakini kwangu huo ulikuwa umebeba historia tofauti kidogo kwangu kuona maji nilijua nimepata njia bora na rahisi katika kutimiza mipango yangu ya kuwa mbali na kambi ya kifo. Maana nilikuwa nimeonyeshwa mateso mapya yasiyo simlika katika masikio ya watu wenye upendo yakaeleweka.Maana mateso yenyewe hats shetani angelishangaa kuyaona yanavyo fanywa na wanadam. Maana watesaji walio kuwa wamepewa kazi ya kunihoji walikuwa wameifanya kazi yao kwa weledi mzuri.
Kama ni kifo nilikuwa nimepishana nacho mara elfu moja kutoa moja hivyo nilikuwa nimebaki kuishi kwa ajiri jana maana leo yangu kwangu ilimaanisha kifo cha kikatili.
Sikuwa naogopa kifo maana kifo kilikuwa kimewachukua wengi.
Lakini nilikuwa muoga wa kifo cha aina gani nitakufa.
Maana kifo cha heshima walicho kuwa wanakiona kwao kuwa cha starehe sana ni kupigwa risasi mia saba.
Risasi mia saba ilikuwa ni zawadi ya heshima kama ungelipigwa nazo tena upigwe hadharani. Maana ungelikuwa umeingia kwenye kitabu cha walio vunja rekodi ya dunia kwa kupigwa risasi nyingi na askari wasio penda kuua kwa risasi.
Hakika duniani kuna wanyama wakali wa aina mbali mbali lakini yupo mnyama mkari kushinda wote uwajuao naye ni mnyama hatari kuliko neno hatari lenyewe.
Binadam ndiye mnyama hatari kuliko wengine maana anaweza kucheka na kutabasam kwenye uso wake lakini moyoni akawa amejaa chuki na hasira ambayo inazidi kiwango cha ujazo. Chuki na hasira ikiwa ya kutosha na ikajaa pomoni hapo ndipo umwagika mithili ya maziwa yaliyo zidiwa na moto wa gesi. Hasira,chuki,ubaguzi,mauaji ni matokeo ya kujaa kwa mambo yasiyo faa moyoni.
Hivyo chanzo kikubwa kilicho kuwa kimepelekea vita isiyo koma ya waparestina na Waisrael ilikuwa ni ubaguzi.Wao waliuchukilia kama sehemu ya ibada wengine walichukulia kama ukombozi na wengine waliona hapo ni sehemu sahii ya kuwekeza.
Eti kuwekeza ndiyo namaanisha kuwekeza kweli siyo kwamba nekosea maana mataifa ya magharibi yaliuchukulia mgogoro huo kama fursa ya kibiashara.Maana waliwauzia siraha za kivita na vyakula kwa kibadilishana na mafuta na madini. Hivyo vita ilileta faida kwa upande mwingine. Hapo ndipo nilipo kibalia na wahenga wa Tanzania walio sema msemo wa busara. "Akili ni nywele" lakini walipo kuwa wanatoa maemo huo wala awakuwaangalia wenye nywele ndefu tu kwamba ndio wenye akili na vipara ni mabogasi laa. Walikuwana na maana kubwa mno na ndiyo maana walitoa jibu tofauti."KILA MMOJA ANA ZAKE"
Kuwa na akili na kuzitumia ni vitu viwili visivyo na mahusiano mazuri.
Maana wenye akili huwa watumwa wa wasio na akili hapo ndipo nilibaki kinywa wazi nikiushangaa ulimwengu wangu.Mtu asiye na akili akiwa na busara ni busara yake haiwezi kumsaidia na mwenye akili akikosa busara hana faida yeyote na akili yake.
Busara ilikuwa ni bora kuliko akili kama ingelikuwa kwa mtu mwenye hekima.Maana wenye akili walipata pesa za damu kwa akili lakini walizitumia mali hizo za damu katika kumwaga damu nyingine.
Niliutazama mto Efrati ambao kwa haraka nilijua unacho kina kirefu nami nilitamani sana kuwaacha askari kwa njia yeyote maana makosa kidogo yalikuwa ni kama kufungulia mlango wa mauti. Uzuri wa eneo nililo kuwa nimefika lilikuwa karibu na makazi ya watu pia eneo hili lilikuwa ni kitovu kikubwa cha utalii maana wengi was watalii walipenda kutembelea eneo hilo kwa sababu ya mlima ulio kuwa na historia ya kuvutia na maji ya mto Efrati yaliyo kuwa ni maji matamu na baridi lakini yakiwa yamepita kwenye jagwa.
Askari walio kuwa wananikimbiza sikujua idadi yao kamili zaidi ya kukariri sauti za bunduki zao zenye nguvu.Maana kufikia hapo nilisha jua hata jinsi kila mmoja anavyo lenga shabaha na kuachia risasi.Nilikuwa nimeamua kuwabatiza majina kutokana na matumizi yao yalivyo.Maana kila mmoja kuna namna alivyo kuwa anaanza kupiga tofauti na mwenzake. Askari mmoja aliye kuwa anapiga risasi kwa kukandamiza sana traiga nilimpa jina lake "A" maana risasi zake kamwe zisinge niletea madhara maaan shabaha yake ilikuwa inabebwa na uzito wa bunduki yake mpya ambayo alikuwa ajaizoelea kabisa.Maana kama angelikuwa amedum nayo kwa walau mwaka mmoja hivi nisingelisimlia haya leo hii.
Maana kila alipo kuwa akiachia risasi ilikuwa ni lazima bunduki iteme risasi kuanzia kumi na kuendelea hivyo alinipatia uhuru wa kumchenga chenga la mwili na kumuacha solemba.
Askari "B" yeye tabia yake nilimfananisha na mdunguaji aliye toroka mafunzo kabla ya wakati wake kutimia maaana huyu ndiye aliye nipatia wakati mgumu zaidi maaana kila alipo kuwa akiachia risasi mara nyingi zilikuwa za sehemu ya hatari.Maana nilikuwa nimekoswa risasi zake kama kumi ambazo alikuwa na lengo la kunisambaratisha kichwa.Huyu niliona sipaswi kumpa nafasi aendelee kuutawala mchezo maana alikuwa kidogo anauweza mchezo wangu.
Sikutaka kujua kama kulikuwa na askari zaidi ya hawa A na B maana hawa ndiyo nilio kuwa nimeikariri mitupo yao ya risasi.Maana kila mmoja wao alikuwa ananishambulia kwa zamu.Haikuwa imetokea nikasikia risasi kutoka katika bunduki mbili kwa wakati mmoja. Hivyo nilizipata hesabu zao mapema. Akili ya askari hawa haikuwa tofauti na askari wetu wa kiafrika ingawa walikuwa jeshi moja lakini kila mmoja alitafuta ushindi wake kupitia njia yake mwenyewe.Hapo ndipo walikuwa wamefanya kosa ambalo mtu kama mimi ukinipatia nafasi hiyo naiona nafasi ya dhahabu.
Hivyo ilikuwa ni juu nitumie nafasi hiyo ya dhahabu ama niachane nayo.Lakini kwangu nilipaswa kuitumia kwa udi na uvumba maana shombo la kifo na ufugwa sikutaka tena vinukie ndani ya pua zangu.
Nilikuwa nimeutamani Uhuru wangu kwa muda mrefu sana .Sikuwa tayari kuendelea kuuongojea tena kama ndugu zangu wanavyo msubiria Kristo aletwe na mawingu.Mi nilikuwa nimeamua kuutafuta uhuru wangu kwa gharama ya malipo makubwa .Malipo ambayo kama ningelichelewa yangelikuwa batili na ningelivuna mabua.Hivyo kila nafasi niliyo Iona inaweza kunisaidia kupiga hatua niliitumia vilivyo bila hata kuuliza ushauri.Maana hakuna mshauri wa uhai wangu zaidi ya Mwenyezi Mungu wengi ambao wangelinishauri wangelibaki katika duara lile lile la ushauri wa maisha.Upande muhimu wa uhai wangeliutupilia mbali.Maana hata wameshidwa kujishauri wenyewe juu swala dogo kama mapenzi.Mtu wa namna hiyo atakusaidia nini sasa zaidi ya kukuaza ujinga uliyo tukuka ukatakasika. Ujinga mtakatifu kabisa ambao nilikuwa nimeuona kwa askari hawa wasio kuwa makini na wanaye mkimbiza.
Kila nilipo utazama mto akili yangu ilinipatia machaguo mawili makubwa yenye manufaa kwangu. Akili ya kwanza nilihitaji nipate siraha na mavazi ya kunikinga na baridi maana nilijua nina safari ndefu ya kutoka katika eneo hili.Jambo lingine la muhimu lilikuwa ni kupata mawasiliano na pesa maana safari hii ilikuwa ni zaidi ya msafiri kafiri hivyo pesa lilikuwa jambo la muhimu katika safari ya kuutafuta uhuru wangu.
USIKOSE NAKALA YAKO.
KITABU KIPO TAYARI NA UNAWEZA KULIPIA KUANZIA SASA NAKALA MOJA TSH 10000, LAKINI KUNA PUNGUZO KWA WATAKAO LIPIA ZAIDI YA MOJA.
UNAWEZA KULIPIA KUPITIA
0656353765 NELSON NTIMBA.
0625813536 JOHN KAMWELE.
0785039047 NELSON NTIMBA.
MALIPO YOTE YAFANYIKE MAPEMA MAANA VITACHAPISHWA VITABU VICHACHE.
Kama mpango wangu ungelikwenda kama nilivyo usuka uhakika wa kutoka salama ungelifanikiwa kwa asilimia sabini.Hivyo nilipaswa kujiandaa kuwakabili askari hawa kwa njia yeyote ile maana nilisha waona ni zawadi ya pekee katika wakati wa hatari kama huu.Hivyo kama wasingelinifuata ningeliwafuata mimi maana tayari nilikubari kuwa chui na kuacha tabia zangu za kipaka.
Kama mistu ya Afrika ilivyo kuwa imeshonana kwa miti mirefu iliyo jazana matunda tele na manyani na ngedere.Misitu hii ya ukanda huu wa Gaza ilikuwa tofauti kabisa yenyewe ilikuwa imesokotana na miiba mikali aina ya michongoma na mchanga laini wenye kushikwa na joto kwa haraka sana.Hivyo nilipaswa kubadilikana kulingana na mazingira yangu mapya yalivyo nipokea.
Maji huwa na faida kama mtumiaji atakuwa tayari kuyatumia kwa faida lakini maji huwa hatari kama yakitumika kwa papara.Mfano kama wewe ni mnywaji wa maji
Kama mistu ya Afrika ilivyo kuwa imeshonana kwa miti mirefu iliyo jazana matunda tele na manyani na ngedere.Misitu hii ya ukanda huu wa Gaza ilikuwa tofauti kabisa yenyewe ilikuwa imesokotana na miiba milali aina ya michongoma na mchanga laini wenye kushikwa na joto kwa haraka sana.Hivyo nilipaswa kubadilikana kulingana na mazingira yangu mapya yalivyo nipokea.
Msemo usemao mtaka yote kwa pupa ukosa yote niliuweka akilini maana muda wa kuutumia ulikuwa ndiyo huo umekaribia.Hivyo niliamua kucheza na akili ya wawindaji wangu kwa kiwango chao walicho kuwa nacho.
Mavazi niliyo kuwa nimeyavaa niliyavua na kubakia uchi wa mnyama na nguo hizo zulizo kuwa zimetapakaa damu nilizisogeza karibu na mto lakini pembeni ya ulio kuwa umeota karibu kabisa.Mti wa msonobari ulio kuwa umejaa majani ya kijani kibichi niliuona utanifaa walau kwa kitengeneza hila yangu.Hivyo nilisogea mita kama hamsini toka kwenye nguo zangu na kuukwea mti huo mithiri ya gendere aliye ona matunda ya komamanga. Nilipanda hadi sehemu ambayo iliweza kunificha vya kutosha.
Macho yangu hayakubanduka kwenye windo langu maana nilijua lazima watafika eneo hilo na nguo hizo zingeliwatia hofu na kiwewe.Hivyo nilitamani sana wafike eneo hilo kwa haraka zaidi.Maana matumaini yasiyo timia uvunja moyo vipande vipande.
Nilikubali kuwa mvumilivu ili nipate kuzionja mbivu maana unaweza kuzani hazi ni mbivu kumbe ni mbovu.
Hatimaye subira alimvuta heli na siyo bangi kama rafiki yangu wasemavyo. Ndani ya dakika kumi tu askari "B" ilifika kwenye mtego wangu na kuanza kuukagua kwa umakini.Aliangaza kushoto na kulia kisha macho yake yalitazama n'gambo ya mto. Lakini ni kama hakukubaliana na fikra zake maana aliacha kutazama mbele sasa macho yake aliyaelekeza katika mchanga na hapo niliona anajianda kwa kukagua siraha yake na kuanza kufuata nyayo zangu za miguu.
Kama n'gombe anaye kwenda machinjioni kwa hiari yake bila kulazimishwa ndiyo niliyaona anayafanya askari huyu mwenye kifua kama cha Big show.Maana alizidi kufuata nyayo zangu bila kujua kama ni mtego kama alifikilia ninamtoroka hapo ndipo alifanya kosa la mwaka ambalo kamwe asingelipata nafasi ya kulijutia.Maana alikaza macho kwenye vichaka na arithini kuliko kwenye miti.Chui siku zote maficho yake huwa ni ya siri na yanayo muwezesha kufanya shambulio la kushutukiza.Hivyo wawindaji wanao muwinda chui ujikuta pabaya maana wanawinda anaye wawinda. Hivyo nami nilikubali kuwindwa nami nikamuwinda mwindaji Mwenye siraha. Maana alikuwa amekubali kuwa windo langu nami nilimkaribisha kwa utulivu nikiwa juu ya mti wa msonobari.
Chui ni mnyama mwindaji anayewinda kimyakimya sana. Ingawa ni mdogo kuliko wanyama wote wa jenasi ya Panthera, chui bado anaweza kuwinda mnyama mkubwa kwasababu ya fuvu lake kubwa lenye taya zenye nguvu. Ukilinganisha na paka mwili wake ni mrefu zaidi na miguu yake ni mirefu. Urefu wa kichwa na mwili wake ni kati ya sm 125 na 165 na mkia wake unakaribia sm 60 mpaka 110. Urefu wa mab hiiega ni sm 45 mpaka 80.
Tabia zangu za kufanya mazoezi ya kuruka na kupanda ndizo zilinifanya niitwe chui tangu nikiwa mdogo.Nilipo jiunga na jeshi hapo ndipo niligundua nina kitu cha ziada kuliko wenzangu maana siku zote nilikuwa nawaweza wenzangu katika mapigano ya ana kwa ana na pia kasi yangu ilinisaidia .Nilipo kuwa katika mafunzo ya ukomandoo huko Cuba nilifanikiwa kutunukiwa tuzo katika kulenga shabaha hivyo niliweza kuhitimu chuo cha ukomandoo nikiwa mdunguaji hatari.
Mafunzo ya uninja niliyo yapata Japan yalinifanya nikamilike sasa kuwa chui mweusi maana mbali na kujifunza njia ya upanga ambayo ya Samrah nilikuwa ninja kamili mwenye kuweza kutumia mbinu zote kwa ufasaha.Ndiyo nilikuwa katika kiwango cha ninja mweusi.Nikiweza kutumia aina kumi na mbili za panga,Nikiwa nimekamilika katika uwezo wa kutumia black art mapambano hatari katika uninja ambayo ni miiko isiyo zungumzwa wala kutumika maana inakufanya mtumiaji uwe mnyama na katili.
(II)
Kuwa ninja kulinifanye niwe hatari katika mbinu za kujificha na kutoroka katika sehemu zenye vikwazo vizito.Hivyo mapigano ya mstuni ama ya mjini hayakuweza kuipa hofu kamwe. Maana mbinu zote kujilinda nilizifahamu kama tebo ya pili.
Askari "B" aliusogelea mti wa msonobali akiwa anaendelea kuangaza chini bila kufikilia kama chui hanaga tabia za kujificha kwenye vichaka.Maana kuangalia kwake chini ilikuwa ni alama ya ushindi kwangu maana alikuwa anaupoteza umakini wake. Hatimaye alikuwa chini ya shabaha yangu nami nilihitaji nimsafirishe bila nauli kwa pigo moja la shingoni.
Wanyama wala nyama aina ya paka huwa na tabia zinazo fanana wawapo kwenye mawindo yao.Mbinu ya kwanza ambayo wote huitumia ni mbinu ya kulitia hofu windo lao.Hofu ulisababisha windo hususa kutokuwa makini na ndicho nilifanya baada ya kuvua nguo askari huyu alipo ziona alipatwa na hofu. Hofu hiyo ilimfanya afuate nyayo zangu bila kufikilia.
Jambo jingine wanyama kama chui maficho yao kwa ukawaida huwa ni mepesi sana hasa hasa kwenye miti ya vichaka. Hivyo kama ukiambiwa umuwinde chui chunga sana kusogelea miti yenye vichaka maana chui umshambulia mnyama yeyote anaye ingia kwenye maficho yake.Mashambulizi yake huwa ya kushtukiza na mara nyingi ulenga shingo ama kishwa maana anafaham hapo ndipo kwenye udhaifu wa viumbe wote walio ubwa na Mungu.
Hivyo askari "B" nilisubilia ageuze shingo yake na uso wake anitazame tu. Kama nilivyo kuwa nataka ndivyo alivyo fanya alipo tazama juu ya mti tu. Nili jiachia kwa kasi kama mshale nikiwa nimekunjua vidole vitano vya kiganja cha kulia .Aina hii ya pigo ilivumbuliwa huko China na kwa kawaida ilitumika kwa ajiri ya kumpiga adui mwenye siraha.
Vidole vyangu imara kama chuma vilizama kwenye shingo yake laini na kumtoboa matundu matatu kwenye koromeo.
Hakupata hata nafasi ya kuomba maji ya kunywa maana pigo hili upasua mishipa ya damu na hata usimamisha mapigo ya moyo kama usipo pigwa sana. Lakini kwa nguvu nilizo zitumia nilipasua mfumo wa damu na upumuaji kwa wakati mmoja. Hivyo maisha ya askari huyu yaliisha kwa pigo moja tu ambalo huitwa tiger crow.
Nilimvua mavazi yake yote na kuchukua siraha zake zote na beg dogo alilo kuwa nalo mgongoni ambalo makomandoo siku zote hulibeba wawapo msituni .Kila kitu nilikichukua na kumuacha uchi wa mnyama maana tayari hakuwa na lake tena katika ulimwengu wetu wa walio hai.Hivyo hakupaswa kuipata salam ya mwisho wala kuzikwa kwa heshima.
Nilipo kuwa tayari nimeshapata siraha niliona nmsubirie na mwenzake tena ambaye naye alukuwa ni hatari kama angeliendelea kuwapo katika eneo hili maana huenda angelihitisha msako mara dufu kama angeligundua hujuma yangu niliyo mfanyia wenzake. Hivyo niliupandisha juu ya mti mzoga wa askari "B" maana hiyo ingelisaidia usifahamike kwa urahisi.Tabia za chui nilizimudu kwa kiasi kikubwa ikiwemo kutokuacha ushahidi kamwe hata kama ni mdogo sana mithiri ya punje ya ulezi maana kuacha ushahidi wa hatari ni sawa na kujivika bomu la kujitoa mhanga ulilo libuni mwenyewe. Hivyo tangu nianze kazi hii ya kijasusi ni mara moja tu nilipo acha ushahidi katika eneo la tukio ambao uliniletea matatizo hadi leo hii. Kupuuza mambo ya msingi kulinifanya niwe mpuuzi lasimi.
**********MWAKA MMOJA NYUMA******"***
Nikiwa mmoja ya mamluki walio kuwa wamepewa tenda ya kumuua kiongozi wa wanamgambo wa Tarban.Upelelezi wetu ulio kuwa umechukua zaidi ya mwaka mmoja ndani ya kambi hiyo siku hii tulikuwa tumeingojea mithiri ya wanadam wa imani fulani wamsubilivyo Yesu Kristo wakiamini atakuja na mawingu akiwa na jeshi la wapanda farasi.
Mipango yetu ilikuwa imefanyika kwa usiri mzito kipindi chote hicho maana hakuna aliye kuwa akiwasiliana na mwenzake kwa njia ya kawaida maana kambi hiyo ilikuwa inaulinzi mkari mara mbili ya ulinzi wa rahisi wa Marekani.
Hakuna ambaye alihifaham sura alisi ya kiongozi hiyo maana alikuwa na ndugu zake ambao alifanana nao sana na wao walikuwa na mamlaka kamili kama yeye.
Kulifaham jina lake halisi nako kulikuwa ni mtihani usio kuwa na majibu sahii maana aliitwa majina tofauti tofauti kila mahali kulingana na walivyo kuwa wanamfahamu.
Jambo la hatari zaidi ambalo kiongozi huyu alikuwa nalo ni kumiliki makombora ya nyukilia na hapo ndipo alipo kuja kuwa tishio kwa ulimwengu wote. Hapo ndipo aliamua kuandka siku zake katika kalenda maana kila taifa kubwa ambalo aliwahi kuwa na shida nalo lilimuingiza kwenye list ya adui yao.
Siku zote tuliwasiliana kwa tahajuni mimi na wenzangu Wawili ambao kamwe sikuwahi kuwafaham sura zao kamili ama majina yao maana moja ya sheria yetu ilikuwa ni hiyo hupaswi kumfamu mwenzako kwa sura wala jina.
Sote tulikuwa ni maninja walio kamili hivyo tulitambuana kwa alama zetu pekee.Hakuna ambaye aliwahi kushtukiwa hadi siku hii ya mwisho ambayo tulimpoteza mwenzetu ambaye alikubali kujitoa muanga kwa ajiri ya kumfahamu kiongozi alisi.Mimi nilipewa kazi ya kuchukua siri ambazo kiongozi huyu alikuwa anazifcha kuliko uchi wake wengi wetu upenda kuzihita sehemu za siri. Ndiyo ilikuwa ni siri nzito haswa maana adui mwenyewe alikuwa ni kiongozi wa nchi tena nchi yenye kuogopeka.Bora kutokujua kuliko kujua ambayo yatakuacha na majuto milele. Hicho ndicho kilikuja kunikuta maana nilijikuta katika utata ambao kamwe nisinge lipona kama ningeliamua kuuweka wazi kwa walimwengu wenye kuishi kwa kutegemea hewa ya oksijen ambayo wasomi wa kisayansi waliipatia jina lao na wataalam wa lugha jina lao lakini kamwe awakuweza kuinunua wala kuiuza maana si mali ya.
Siku ya tukio la kutisha ilianza kama kawaida katika kambi yetu ya siri iliyo kuwa imepewa ni jina lenye kuchefua kama siyo kutisha kwa wanamgambo kwenye kuishika ibada ya kuchinja utazani ni amri ya muhimu kuliko zote maana kama ungeligundulika unausaliti kwa kumwambia hata mtoto wako wapi unafanya kazi ungelijutia na kuulaumu ulimi wako kwa kuropoka mambo yasiyo tamkwa.
******KUZIMU YA MSALITI********
(iii)
Hakukuwa na jeshi ambalo liliwahi kuivamia kambi hii ambayo ilikuwa chini ya arithi maana ilikuwa ipo kuzimu kweli lakini juu ya kambi hii kulikuwapo makazi ya raia wema ambao walihishi kwa amani na furaha. Hakuna raia aliwahi kugundua kama anahishi juu ya mgongo wa kaburi ambalo lilikuwa linawameza watu walio kuwa ni wasaliti.Hapo ndipo palikuwa na fumbo maana walikuwa wanaletwa watu mbali mbali wanateswa hadi kufa katika kuzimu hii na kamwe hakuna aliye wahi kuletwa humu ndani akatoka hai maana waliojiwa kwa njia ambazo kamwe hazikuwezwa kuandikwa na yeyote aliye wahi kuishi.
Mateso yaliyo kuwa katika kuzimu hii hakika siwezi kuyasimlia kwa sasa maana yatisha kuliko kitisho chenyewe.
Maandalizi ya kujitoa muhanga kwa mwenzangu ambaye kamwe sikuwahi kumfamu yalifanyika kwa siri sana maana ilipaswa afe siku hii ambayo sisi tulipaswa kutoka ndani ya jengo hili ili tusiangamie pamoja nao.
Lakini kufa kwa mwenzangu ndiko kuliuleta mkasa ambao kamwe sikuufikiria kama ungeliweza kunifikisha hapa.Ndiyo rafiki asiye fahamiana alikufa na kambi mzima kwa kuujioa mhanga.Namimi na mwenzangu ambaye sikuwahi kumfahamu kwa sura tulitoka salama katika kuzimu hiyo. Lakini siri hii ya kumfaham kiongozi mkubwa katika ulimwengu wa watu wa amani ndiyo imenifanya gaidi.
*********
Baada ya kuwa tayari nimemhifadhi katika sehemu askari huyu mfu ambaye kamwe asingelijitikisa tena niliendelea kumngojea kwa hamu askari "A" ambaye nilijua si wa kunisumbua maana nilisha pata siraha ambazo zingelini rahisishia kazi ya kumsafirisha.Haikupiata hata dakika kumi maana tayari naye aliuvaa mkenge wa nguo zangu na kuanza kuangaza kufuata nyayo. Huyu sikutaka kumchelewesha nilichukua kisu na kukirusha kwa nguvu zangu zote hapo siku subiria kujua nini kingempata maana nilijua majibu yake ni nini. Nilimsogelea na kumkagua hapo nilifanikiwa kupata vifaa muhimu vya kunisaidia katika safari ya kuusaka UKANDA WA GAZA pesa ilikuwa kati ya vitu muhimu nilivyo vihitaji kwa muda huo.Maana siku zote nilijua pesa inapenya popote hata kwenye mapenzi ya haki
Mwendo wangu sasa ulikuwa ni wa nusu kukimbia nusu kutembea.Mzigo wa vifaa visivyo mali yangu halali ulikuwa mgongoni mwangu umejituliza.Haukuwa na ujanja wa kunitoroka maana tayari nilisha jichukulia.Uzuri wa bunduki hizi aina ya IWI X95 TAVOR SMG huwa zinabebeka kwa urahisi zwidi kuliko SMG zote maana ni nyepesi mno.Hivyo hazikunipa taabu katika harakati zwngu za kutokomea katika uhuru wagu.x
Mwili ulikuwa umechoka kwa mwendo mrefu ambao nilikuwa nimeupiga.Jua tayari lilisha anza kurudi kwa mchepuko wake baada ya kumaliza kazi yake ya kutwa nzima.Mwezi nao ushaanza kujipendekeza kutoka katika maficho yake ya siku zote.
Hali kama hiyo huwa nzuri sana kwa Makomandoo wa hadhi yangu maana vurugu zote za waimba kwaya wa mitini huwa zinazima.Hakuna jamii yeyote ya ndege ambaye uendelea kupiga okestra maana muda wake wa kutumbuiza huwa umefikia mwisho.
Sauti pekee ambayo ubaki ni miruzi ya wadudu ambao huwa hawana madhara yeyote zaidi ya kunipa taarifa.
Nilikuwa nimetembea karibu mwendo wa saa saba toka nilipo kutana na kashikashi la kufukuzwa na askari walio kuwa wanaiwinda roho yangu kwa udi na uvumba.
Wakati wa swala ya Magaribi ilinikuta katikati ya mji wa Watarita.Nikiwa na begi langu lilokuwa nimebeba vipande vya bunduki na kila kifaa kinacho mfaa askari wa daraja la kati.
Mji huu ulikuwa na tofauti kubwa na miji mingi ambayo nilikuwa nimeitembelea maana ndiyo mji pekee ulikuwa haujahathilika na vita.Sababu kubwa ya mji huu kuwa wa kistarabu ni kutokana hakukuwa na tofati za kidini.
Kama tukisema tufananishe na nchi za Afrika mashariki nafikilia Wangelikuwa kama Watanzania tena Wasukuma.Maana kumkuta Mwislam kwa mkatoliki wakiongea ilikuwa ni jambo la kawaida.
Lakini jamii hii jambo kuu lililo nivutia mno ni ujasiri wao na umahiri katika maswala ya kulinda amani yao.
Watalita walikuwa ni jamii ya Wamongoliani walio kuwa wamekwisha changanya damu yao na
jamii mbili wenyeji. Lakini bado walibaki na asili yao ya Kimongoliani.
Jamii hii hapo kabla walikuwa wapiganaji wasio rudi nyuma katika vita.Na walipenda kupigana wakiwa juu ya farasi. Kamwe hakuna vita ambayo waliwahi kushidwa .
Jeshi lao siku zote lilikwenda likiwa kundi na kwa kawaida walipeana zamu ya kushambulia adui yao bila kumpa nafasi ya kupumzika.
Tabia ya jamii hii kidogo ilikuwa ni ya kuvutia maana ukarim na kicheko kwao ni sehemu ya maisha lakini kifo ni mwendelezo wa maisha bora ya amani.
Hawakuogopa kupoteza chochote maana walijiona si chochote.Hivyo hakuna adui aliye kuwa tayari kumenyana na watu wasio ogopa kifo.
Katika mji huu mdogo kulikuwa na mwnyeji wangu ambaye kamwe sikuwahi kulifahamu jina lake .siyo tu kufamu jina lake tu hata code yake ya kazi ilokuwa siri yake.Jina pekee nililo lidahamu ni Giza na kuweza kumpata ilitakiwa kuwe giza na upige muluzi wa ndege aina ya mbundi mara tatu.
Lakini kwa muda huo sikutaka kusubilia hadi kuwe giza maana nilihitaji msaada wa haraka sana kutoka maeneo hayo hatari.
Jasusi asiye na hisia ni sawa na mbwa asiye na pua na kanuni hizi za kijasusi ambazo huwa zinaongoza nimezishika sana akilini kama ambavyo siwezi kusahau uzao wangu kwa sababu katika tukio lolote jasusi mwerevu huzitumia.
(IV)
USHAHIDI WA MWILI;
Kukusanya ushahidi linaweza kuwa ni suala gumu mno wakati mwingine kutegemeana na nature ya tukio, pengine mwili umeokotwa, umekutwa, umetupwa majini,umeungua au kuaribiwa vibaya, kwa hali kama hii tutaitaji kupima vinasaba, kupima alama za vidole, kupima mifupa hata kama mwili ulikuwa umeshafukiwa, kupata baadhi ya vifaa alivyotumia marehemu kama mswaki,kitana au mavazi nakadhalika.
Kiujumla baadhi ya vipimo vyote hapo juu ulenga katika kubaini mambo mengi ila baadhi ni kubaini identity ya marehemu, kifo chake kimesababishwa na nani au nini mfano sumu, muda tokea tukio lilipotokea nakadhalika.
KUULIZA, KUFANYA MAHOJIANO NA KUCHUNGUZA
Eneo jirani na lilipotokea tukio(picha ya muhusika uweza kutumika pia wakati wa kuulizia) hapa kama mpelelezi lazima avae uhusika wa kirafiki/kijasusi nakuweza kuwafanya majirani,ndugu jamaa na marafiki au mashuhuda,
Kumpa ushirikiano wa kitaarifa aweze kupata maelezo mawili matatu kumuhusu marehemu ili aweze kuconnect dot za kilichomkuta mwendazake ikiwemo kubaini kabla ya tukio marehemu aliongea nini, alikuwa akifanya nini, ana maadui wangapi, hali ya mwenendo wake kitabia, afya,mahusiano n.k
KUJUA DHAMIRA YA MUHUSIKA KABLA YA KUFIKWA NA MAUTI
Alikuwa akidhamiria kufanya nini; hili ni muhimu mno lakini utaniuliza kuwa utajuaje kuwa mtu aliwaza nini, ukiachilia mbali kufumbua mboni zake nakuona machoni alichoshuhudia kabla ya kuaga dunia,
pia jua kuwa siku hizi duniani tumeathiriwa na matumizi ya kimtandao especially vijana lazima utakuta tumegoogle mf. Porn utajua tu marehemu bila shaka alikuwa idle bila kazi, mpweke au hayuko kwenye mahusiano pengine kaachwa, kukataliwa au kashindwa kuziexpress hisia zake
hivyo ni rahisi akakumbwa na msongo au amnesia, na kama ni politics,elimu, umbea wa mitandaoni pia utajua kama yupo normal au ni shabiki wa star, mwanasisasa au club fulani na aliguswa pabaya kulingana na comments zake n.k
Pia text, post za picha, kuweka status au kuandika chochote kinachoexpress feelings or emotions ambacho ni kielelezo kizuri kujua mwenendo wa maisha yetu kwa siku za karibuni ulivyokuwa, kingine ni siri au stori tulizoshare na waliokaribu, jumbe tulizohifadhi kwa siri, alama,ishara,body language, mkao wa mwili,mazoea yetu n.k
VIHIFADHI KUMBUKUMBU
Hapa tunazungumzia vifaa vya kisasa ambavyo unakili na kuhifadhi kumbukumbu ambavyo vikitumiwa ipasavyo uweza kutoa ushahidi usio acha shaka, mfano ni kompyuta, vinasa sauti, simu, tv, magari, flash,memory card, digital cameras,CCTV nakadhalika.
Inawezekana kukawepo na ushahidi katika moja ya vitu hivyo inayoonesha nature ya tatizo, chanzo cha tatizo mfano pengine ni ushahidi aliokuwa nao marehemu,tukio lilivyotokea au wahusika waliokuwepo wakati wote wa tukio.
HACKING
Kama mpelelezi hakuna kitu muhimu kukijua kama kuwa mbobezi na mtundu wa mambo ya IT unatakiwa kuichezea kompyuta kama menyu vile, ukiwa mzembe au mjinga hapa wahalifu watakutesa mno maana kwa dunia tuliyopo uhalifu kwa njia ya mitandao hauepukiki isitoshe mifumo yote ya kifedha,huduma za msingi za kijamii, mawasiliano, ulinzi na usalama, utawala na uendeshaji uhifadhiwa kwa njia ya kimtandao hivi sasa mpaka vyombo vya usafiri, kilimo, biashara,majokofu na vyombo vya ndani ya nyumba vyote viko under control ya mtandao,
hivyo ikiwa hacking imefanywa na wahalifu inaweza kuwa chanzo cha vifo au hasara iliyopelekea kifo hivyo uchunguzi wa kina kimtandao lazima ufanywe na mbobezi katika kutrace IP, kudukua simu mf.kufanya duplication ya simu kupata GPS, radio frequencies, hacking na virus programs,
kugundua kama mko under surveillance camera za wahalifu, kuhamisha au kufungua files muhimu mtandaoni,au kuilinda system dhidi ya mashambulizi n.k Hivyo kama kitengo cha upelelezi ni muhimu sana kuwa na ujuzi na vifaa vya kisasa,vinavyojitosheleza na more advanced kuliko wahalifu.
MBINU ZA MAPAMBANO
Iwe ni ana kwa ana yaani mkono kwa mkono mpelelezi awe na uwezo wakumkabili adui kwa mbinu mbalimbali zaki-marshal arts mf kareti,boxing, judo, taekwondo, combat karate n.k lakini pia ujuzi wa kutumia silaha za aina zote ni muhimu, uwezo wa kuendesha nakutumia vyombo mbalimbali vya usafiri, kutumia vifaa vya kiteknolojia na uzoefu wa mapambano mbalimbali yakuarrest gangs au notorious people ni muhimu kuweza kufanikiwa katika kukabili kesi za namna hii.
Au iwe ni mapambano yanayohusisha akili na saikolojia inayofanywa na muhalifu kukutoa kwenye mstari,kupoteza ushahidi au kukunasisha kwenye makosa,
ikiwa ni pamoja na kuyakabili mashambulizi ya mtandaoni mfano kati yako na adui anayehack data au vyombo vya mawasiliano au kuattack pasipo kujulikana halipo au aliyembali tuseme nchi nyingine nakadhalika
JICHO LA UPELELEZI
hili ni jicho litazamalo nakufanya kazi kuu tano yaani kuona, kuchunguza, kugundua, kuihundia picha nakutoa uamuzi.
Katika hili mfano mdogo ni picha ya tukio la mwili wa marehemu uliolala chini eneo la mauaji baada ya kunaswa na CCTV camera katika kulitizama tukio hili jicho la mpelelezi alitoishia kuuona mwili tu uliolala pale chini lakini pia mazingira yaliouzunguka na pote camera ilipofanikiwa kupacover,
uwepo wa kithibitisho chochote kama ushahidi mahali hapo, kujaribu kuimagine ilivyokuwa au inavyokuwaga mara nyingi mtu akifa staili kama ile n.k na hapo mpelelezi upata kile alichokihitaji kuendelea na uchunguzi wake.
UWEZO BINAFSI
Hiki ni kipengele muhimu kwa maana uwezo wa kuthubutu,kutenda na kufanya maamuzi kwa ufanisi utofautiana baina ya mtu na mtu, hivyo basi katika hili tunachozingatia ni uwezo wa kuwa na ubongo mpana wa imagination yenye kuangukia kwenye reality au karibia na uwezekano,
Kutoa na kufanya maamuzi ya haraka, kutumia muda kwa ufasaha, kuchakata data kwa wepesi nakuweza kugundua kilichomaanishwa au kufichwa, kuwa na gift ya uwezo wa psychic power, kuwa na uwezo wa ku-influence, ujuzi binafsi katika kupata taarifa/kumfanya mualifu akupe taarifa za kweli,
Ubongo wenye uwezo wa kuhifadhi taarifa na kumbukumbu nyingi kwa muda mrefu na pia weledi wa kukaa na siri, kuwa mwaminifu, nakusimamia kiapo na msimamo wa maadili ya kazi hata kama utabaki mwenyewe au inakulazimu kuhatarisha maisha yako na ya familia.
Kwa maana wakati mwingine chanzo cha mauaji kinaweza kuwa mtu ambaye ukumdhania kabisa aidha ndiye bosi wako, mpenzi, mwanafamilia, mtandao wenye nguvu ya pesa, influence au dola a.k.a hawaguswi/wao ndo kusema au pengine miongoni mwenu wanaupelelezi kuna masnitch(wasaliti) wanaoshirikiana na waahalifu.
Hivyo haupaswi kumuamini yeyote unaye fanya naye kazi na hapo hapo unapaswa kumuamini.
Kwa wakati kama huu sikuwa na chaguo sahihi maana msaada pekee ulikuwa katikati ya hatari za kutokumuamini mtu.
Maana jambo hili la kupuuza hatari za mauaji ziliniweka katika gereza la magaidi kama mmoja ya wanao shirikiana nao.
Sikutaka tena nirudie kosa ambalo nililitenda.
Hivyo kabla ya kuanza kumtafuta mwenyeji wangu niliamua nianze kuuchunguza mji huu kwa makini.
Nilichagua kuanzia upande wa Mashariki wa mji huu ambao kuna barabara kuu iliyo jengwa imara juu ya mchanga wa jangwani.Katika barabara hiyo niligundua ni salama maana hakuna magari yanayotumi barabara hiyo kwa muda mrefu.
Maana inavyoonekana unaweza kuyakadilia ni magari kama ishirini hivi yanayo ingia kila baada ya masaa manne.Ingawa nilikuwa nimetumia dakika ishirini na tano kuchunguza eneo hilo.
Pia niligundua magari mengi yanakuwa yamebeba bidhaa za nyumbani kama vyakula,na thamani za ndani.Lakini niligundua magari yanayo toka ni machache sana kuliko yanayo ingia.
Jambo hili lilikuwa jema kwa upande wangu maana ilionesha wengi wanao fanya biashara ya kusafirisha ama kusafiri ni wenyeji na wageni ni kama hawana nafasi ya kibiashara katika mji huu.
Niliacha na barabara hiyo na kuanza kuingia ndani ya mji huu.Ambao ni kama ulisaulika na waanzilishi wake.Ambao asili yao ni Wamongolia.Lakini hawakusahau kuacha alama zao.Rangi ya ngozi ya watumishi hawa ilikuwa ni nyekundu tofauti na waarabu,Macho yao pia yalikuwa ni madogo yaliyo bonyea kwa ndani.Kama ungelitazama kwa haraka ungelifikilia labda wana matatizo ya macho.
Nazani ni kwa sababu ya kuishi karibu na jangwa ndiyo sababu hawakuwa wanakodoa macho sana.Hivyo kama ungekutanisha nao macho ungelifikilia wanakukonyeza.
Nyumba zao zilikuwa ni bora lakini pia mahema yaliyo fungwa kwa mtindo wa Kimongolia yalitokeza kote kote.Nilikubaliana na historia hasa ya eneo hili kwamba ni mji wa watu wenye asili ya bara la Asia.Maana utamaduni wao ulikuwa ni dhahiri kila sehemu.
Hatimaye nilikuwa nimeuchunguza kwa asilimia za kutosha mji huo hadi nilikuwa nimefanikiwa kufahamu aina yao ya maisha hadi mziki unaopendekezwa zaidi na wenyeji.
Mziki huwa una fichua vilivyo mioyoni mwa watu na hicho ndicho huwa kinaweza kutendeka kwa wakati kama huo.Mfano mzuri ni kuhusu watu wa Magharibi mwa ulimwengu huu mziki wao umejaa matusi,hamu za ngono, matumizi ya madawa ya kulevya,ushoga na ubabe. Kialisi tabia zao zinaakisi wa toka kwenye mziki wao wanao upenda.
Eneo hili niligundua ni watu wa amani lakini wenye kuishi na mashaka. Hawana uhakika wa kuiona kesho yake .Hivyo kama ukishi katika mazingira kama hayo na wewe ni mgeni unapaswa uwe kama wenyeji wako waishivyo.
Kuna msemo mmoja usemao "SIKU UKIWA ROMA ISHI KAMA MROMA" ukiwa na maana unapaswa kuishi kama wenyeji wako walio kukaribisha bila kuleta ukuaji wako wa kwenu.Maana mgeni usikilizaji kwanza kabla ya kuamua na hata akiamua afanye maamuzi ya wenyeji wake.
Nilitambua siko salama kufikia sasa maana nguo zangu zilikuwa zinaonyesha mimi ni askari wa jeshi la Israel.Begi langu kubwa lilitosha kabisa kuniona kama mmoja ya watu wa kazi maana kwa wajuvi wangelitambua ni begi la kijeshi lililo na kimilika.
Haikosi kama kuna watu wale wanao nusa siraha wangelitambua.Maana nilikuwa na bunduki mbili za kivita aina ya IWI X95 TAVOR SMG siraha hatari sana vitani.
Katika ujasusi kuna hii mbinu inaitwa important colours(cooper color codes), ambayo utumiwa na majasusi duniani kunusa na kuzikwepa hatari zinazoweza kuwakuta kwahiyo sio mbaya kuzijua pengine siku moja zitakusaidia.
Hatua nne zinazoweza kumfanya mtu anuse hatari haraka inayoweza kutokea ni hizi hapa zifuatazo;
( V )
CONDITION WHITE
Katika ujasusi ukisikia mtu anaambiwa yupo katika condition white, maana yake ni amekata kaa tu na hawazi jambo gani la hatari linaweza kutokea muda na wakati huo kulingana na mazingira aliopo. Mfano,unamukuta mtu anachart au anaongea na simu huku anavuka barabara, mtu anasinzia kwenye bus akiwa anasafiri muda wote, mtu yuko bar lakini muda wote yuko bize na simu yake, katika hali kama hizo hawezi kuwaza ni Jambo gani la hatari linaweza kutokea, maana yake anakuwa unprepared and totally unaware.
CONDITION YELLOW
Katika hatua hii ni hauoni kama kuna jambo au tukio linaweza kutokea, Ila unakaa na tahadhari na unakuwa unakusanya taarifa kuhusu kitu gani kinaendelea kwa wakati huo kulingana na mazingira uliopo, maana yake unakuwa in relaxed alert. Mfano, unaweza kuwa umekaa kwenye gari unasafiri na unaona hakuna dalili zozote za hatari, ila wewe kama wewe unakuwa unachukua tahadhari kwa mazingira yote mule ndani ya gari bila kujali tukio la hatari linaweza kutokea au lah na katika hatua hii mara nyingi ndo mtu unaweza kunusa hatari inayoweza kutokea na maamuzi ya kuchukua kwa haraka zaidi.
CONDITION ORANGE
katika hatua hii mtu anakuwa na tahadhari maalumu , kwa maana ya kwamba anatambua hatari inayotokea au inayoweza kutokea kwa wakati huo na anajiandaa jinsi ya kukabiliana nayo, kwahiyo ni tunasema a state in which there's a specific alert. Mfano, mtu anatembea sehemu ya watu wengi kama kariakoo, sasa katika pita pita yake kuna sehemu amefika anaona ni crowded, hivyo ananusa hatari labda ya kuweza kuibiwa simu, pesa, au kupigwa roba , kwahiyo kutokana na mazingira hayo anaamua kuchukua uelekeo mwingine au kubadili njia.
CONDITION RED
Katika hatua hii ni pale sasa mtu anajiandaa kiakili ama apambane au aikimbie hatari, katika ujasusi unaambiwa unapokuwa katika condition red inakupasa kuwa na ufanisi wa hali juu muno kuishinda hatari inayotokea au inayotaka kutokea ,hivyo inashauriwa ili kunusa vizuri hatari na kuzikwepa ni vyema kukaa katika condition orange.Mfano, mtu anatembea vichochoroni kwenye giza usiku kisha ananusa kwamba anaweza kupigwa roba na vibaka, ila kwakujiamini sasa ya kwamba atapambana nao kwa nguvu, kumbe adui wana silaha nzito kumuzidi kwahiyo anajikuta ameingia kumi na nane zao na amepoteza pambano ,ambapo angekimbia au kubadilisha uelekeo ingekuwa na manufaa Zaidi kwake.
Ukiweza kuzielewa hatua hizo, itakusaidia kunusa hatari nyingi na kuweza kuzikwepa.
Hivyo hata nilipo kuwa katika eneo hili nilikwisha ona kuna hatari ambayo siwezi kupambana nayo nikiwa mwenyewe.Maana hata kama nilikuwa najua mbinu nyingi za kivita na mpigano hakuna sehemu niliwahi kuona shujaa anawashinda adui zake akiwa katikikati yao tena kwa mikono mitupu.Labda kwenye sinema za kufikirika tu na hadithi za kishujaa. Lakini katika maisha halisi ni bora kukutana na nusu shari kuliko shari kamili.
(Vi)
Tumbo lilinidai haki yake nami sikuwa na budi kutafuta walau mgahawa ama hoteli itakayo weza kunipatia shibe.
Nilianza kupiga hatua zangu za kijeshi kuelekea mashariki mwa mji.Nyakati kama hizi katika mji huu kuna utaratibu ambao huwa ni wa kawaida kwa wenyeji wake.Maana wengi wao huwa wamekwenda msikitini ama huwa wamejifungia ndani wakipata chakula cha mchana.
Hivyo katika barabara huwa kuna watu wachache sana na wengi wao huwa wapo katika nyumba za ibada.Hivyo kuendelea kuonekana kama nisiye na kazi ingelinipatia kazi ya kujitetea.Sikupenda kufanya hivyo kwa muda kama huo maana nilikuwa bado sijapata ninachotaka.Nilikuwa ni sawa na msanii asiye na sanaa ya kumtambulisha kama na yeye ni msanii.Hivyo nilipaswa kuepuka kutiliwa shaka kwa njia yeyote ile.
Hatimaye niliupata mgahawa ambao ulikuwa inajihusisha na mapishi ya kiasili.Nilisoma bango lake kwa nje ambalo lilikuwa limeandikiwa kwa kiarabu na maelezo yote ya vyakula yalikuwa wazi.
Lakini kuna kitu nilikuja hakipo sawa ingawa nilikwisha ukaribia mlango wa hoteli hiyo.Roho yangu ilibidi simba baada ya kugusa kitasaidia cha mlango.Ingawa maneno yaliyopo mlangoni yalionekana yenye ukarimu lakini kuna lugha fulani ilionekana ni ya ziada.
Maana kwa kawaida herufi za kiarabu huwa sahihi ziandikwapo lakini kulikuwa na kosa la wazi katika matumizi ya nukta za neno "mlango upo wazi karibu.."Maana si kawaida kukuta neno linalo sema "MLANGO UPO WAZI KARIBU.." Niliona kuna jambo lakini tayari maji nilisha yavulia nguo kurudi nyuma lingekuwa kosa kubwa .
Nilihisi kuna mlango kama inavyo onekana lakini nilihisi pia kuna kitu kizito kinacho uzuia.Kama ningelikuwa raia wa kawaida nisingekuwa na wasi wasi maana milango ya kusukumwa huwa mizito.Lakini uzito na ugumu wa mlango huu ulinipa majibu.
Hapa ni sehemu yenye usalama na mlango huo ingawa inaonekana ni wa kawaida inaendeshwa na mitambo.
Swali lilibaki kichwani hawa ni watu gani hasa mbona wana ulinzi kwa kila hatua.Jambo ambalo si la kawaida katika migahawa .Ingawa nilifanikiwa kuingiza walau mguu wangu wa kushoto niligundua pia sakafu ya eneo hilo ina kitu kipo chini yake kama mtego.Kulikuwa na mtikisiko mdogo ambao huwa inawekwa kwenye nyumba hasa safe house (nyumba za wanausalama) Maana kila jambo lilifanywa kwa siri na kwa uficho,Ingawa kwangu uficho si lolote maana naongozwa na hisia kuliko macho.
Mazingira ya ndani yalikuwa ni tulivu na masafi haswa.Wahudum waliendelea na kazi zao kama kawaida.Wengine waliendelea kula vyakula vyao.Ingawa jambo hili lilinipa wasiwasi kidogo pia.Maana muda wa swala watu wapo wanakula kama kwamba hawakusikia wito wa mhazini aliye kuwa akiwakaribisha katika swala ya magharibi.
Hilo nalo nililiweka moyoni na kusubiri yajayo maana mgahawa huu ingawa ulionyesha ni wa watu wa dini lakini watendaji wake walikuwa tofauti na maandishi yao yaliyo nje.Maana hawakujali sana mambo ya kimungu.Mavazi ingawa yalikuwa ni makanzu ama punjapi na kofia walivaa kabisa lakini hawakuwa wazembe kama raia.
Nilitafuta sehemu isiyo na mtu ambayo ingelinisaidia niweze kuwatazama wote waingiao na kutoka kwa wepesi. Meza niliyokuwa nimeichagua ilitazamana na mlango wa kuingilia ambao niliutumia kuingia humo ndani.Lakini niligundua kuna milango zaidi ya kutoka nje ambayo haikuwa rasmi.Ungeliitazama labda ungelihisi hapa ni maua yamepangwa ama labda kuna kabati la vyombo lakini mi siku ona hivyo. Kuna vitu niliona vimejiweka kimtego na kificho.
Nikiwa naendelea kutazama niligundua pia kuna kamera za siri ambazo zimetengenezwa kwa umakini.Hapo nilikwisha fahamu siko sehemu salama kabisa.Ingawa hakukuwa na usalama kuna jambo nisingependa linikute kwa wakati huo.Nalo ni kukamatwa tena na Waisrael maana nisingeli achwa hai tena.Maana tayari nimekwisha tangaza vita pamoja nao wasio penda kushindwa.Nilijua watanitafuta na watahitaji kunilipa kwa niliyo kwisha kuwafanyia.Maana muda wa kulipa huwa haikawii labda mdaiwa alipiwe na ndugu zake ama afe.
Kuua wanajeshi wao wawili kwa mikono ilikuwa ni vita kamili kwao.
Hivyo nisingelitaka kwa vyovyote kuwa mikononi mwao nikiwa hai.Maana ningelijuta kuwa mfungwa wa kivita.
Kuna jambo lilitokea kwa ghafla na ambalo sikulitazamia kwa wakati huo.
Mhudumu niliye muona anakuja kunihudumia kuna vitu alivibeba mikononi mwake. Saa yake ya mkononi ilionekana ni zaidi ya saa ingawa ilionekana ni saa ya kisasa.Kama upo sehemu isiyo na usalama unapaswa kuwa makini na kila kitu kitakacho kufanya usiwe salama.Kanuni hii ndiyo ilikuwa imeanza kupewa nafasi, Lakini sikutaka kufanya haraka kuonyesha nimegundua kitu.
Nilikuwa nimeamua kutumia akili kwanza kabla ya nguvu maana nilikwisha n'gamua nipo kwenye makao ya watu hatari.
"Karibu tukuhudumie chakula gani kwa wakati huu?" Aliniuliza mhudumu huyo ambaye sura yake ilionyesha ubabe na mikono yake nyenye misuri mithili ya mizizi ya mpera. Sura yake yenye rangi nya'ngavu,Nywele zake alizokuwa amezifanya vyema kabisa Waarabu vijana wanyoavyo,Ingawa umri ulikuwa unamkimbiza kwenye uzee.
Nilimjibu kwa kutikisa kichwa kwenda juu chini ishara ya kukubali,Ingawa sikuwa nimeagiza chakula lakini niliamua kucheza karata yangu ya kwanza kwake.Kwa kawaida ishara ya kukubali ilikuwa ni sehemu ya alama muhimu kwa mwajeshi wa Tarban.Maana huwa inamaanisha unahitaji maelezo ama unataka njia nyingine ya mazungumzo kuliko hiyo aliyo ileta mwenzako.
(Vii)
Nilikwisha fahamu watu hawa ni wanamgambo wa TARBAN kupitia saa yake ambayo alikuwa ameivaa kwenye mkono wake.Maana saa hizi hasa huwa na vifaa maalum vya kupigana kurekodi matukio.Pia dira huwa wazi kabisa katika saa hiyo.Maana ni lazima mwanajeshi awe na mpango sahihi na majira sahihi,kwa kila tukio ni muhimu kuweka kumbukumbu.
Ingawaje alionekana kama kunishangaa kwa sababu nilikuwa nimevaa mavazi ya jeshi la Israel pia begi langu na buti zilionyesha mi ni mmoja ya Waisraeli lakini hakutoa neno.Aliondoka mbele ya macho yangu kama mtu anaye fuata huduma niliyo kwisha itaka.Lakini hakurudi kama nilivyo kisia maana hakuniamini.
Mwanajeshi asiye jua kusoma hatari na alama ni sawa na mbwa asiye na pua.Maana kama ukitaka kumtega mbwa na umuue kwa wepesi zaidi kama ukianza kuua seli za pua yake na kumzuia kunusa hiyo ni zaidi ya kifo.
Maana hawezi kudumu muda mrefu lazima afe.Nilijua ukweli huo na mbinu hiyo hivyo niliamua kuanza kuitumia ili kujinasua katika mikono yao.Maana nilimfahamu natazamwa na walio nyuma ya kamera.
Mhudumu mwingine wa kiume alikuja akiwa amevalia sare kama yule wa kwanza lakini tayari alikuwa amebebelea sinia lenye nyama ya kuchoma na maziwa ya mtindi.Huyu alikuwa ni kijana kati ya miaka ishirini na tano hadi ishirini na nane.Maana viatu vyake vya buti aina ya cobra vilikuwa miguuni.Alikuwa amemuoa nywele zake kama mwanaume wa kwanza ambaye aliondoka bila kutia neno tena.Lakini huyu alionekana ni mtulivu zaidi.Ingawa hakuonekana kama mpiganaji uso wake ulionyesha anayo maarifa.
"Karibu sana natumaini huduma hii utaipenda zaidi maana nimepewa maelekezo na mwenzangu kwamba wewe ni mmoja kati ya wanao husika." Alisema sentensi hizo akiendelea kupakua chakula hicho kikavu lakini kiupao mwili nguvu,Na matendo yake yalikuwa tofauti na anayo yafanya kwa maneno.Labda nielezee kidogo kama unongelea mapishi hili hali upo unafua ni matendo yasiyo endana. Mbinu hii hutumika kupoteza maboya ama uelekeo kwa wanao kufuatilia.
Nilibaki najishughulisha na chakula kama vile simskii ambacho amekiongea.Maana niligundua ananipatia ujumbe muhimu nisio uelewa kwa wakati huo.
"Haya maziwa ni mazuri kwako lakini yanaweza kukichafua kama ukiyanywa kwa pupa.Unatakiwa ukanawe kwanza ndiyo upate kuyanywa."
Alinitupia sentensi nyingine zenye mafumbo.Hapo nilikwisha pata majibu kamili kumhusu huyu mhudumu.Maana maziwa huwakilisha usafi na usalama.Lakini maziwa yakiwa yamekatika huwakilisha sumu,Kifo,hatari na kulingana na nyama aliyopewa ileta alimaanisha napaswa kuwa tayari kwa vita ama kifo.
Kama ukipata ujumbe wa namna hiyo kwa kawaida huwa kuna kujitetea lakini sikufahamu kwanini wameamua kunipa ujumbe huo.
Ingawa nilikuwa na njaa nilianza kuhisi njaa inanitoroka na kurudi kwao.Maana kifo kilikuwa kinanisubiria lakini nilipaswa kujitetea kama walivyo hitaji.
Mhudumu huyo wa ajabu alirudi baada ya kunihudumia.Nami niliamua kuanza kula chakula hicho maana nilipaswa kuwa na nguvu baadaye niweze kuutetea uhai wangu.
Nusu saa ilipita tangu nimalize kutumia chakula hicho.Niliamua kunyanyuka ili nipate kuondoka katika eneo hilo. Maana nilifahamu watanitafuta hata niwe wapi maadam nilikuwa katika nchi yao. Lakini nilipo kuwa nimefika mlangoni mhudumu mwingine alinikimbilia akiwa na tabasamu.
Kwanza nilifikiri anahitaji kunidai lakini haikuwa hivyo.
Alicheka kidogo lakini cheko la mauti,ingawa niliyoona meno yake na kusikia kicheko chake.Nilijua anajambo mbali na kicheko chake, Maana vicheko kama hivyo huwa ni vya watu wachache sana katika ulimwengu huu.
Watu wa namna hiyo huwa wanacheza na hisia za nje lakini moyo huwa na hisia nyingine.Anaweza kukua akiwa anacheka na anaweza kusamehe akiwa na hasira.
Huyu alikuwa ni miongoni mwa binadamu wachache walio kuwawamebaki wakivuta hewa ya dunia bila kuwaona faida maana kiasili ni wanyama wakali wasio paswa kuishi na wanadamu.
"Komred tunahitaji hilo begi lako ndiyo malipo ya chakula, Lakini pia kama hutojali sana baki nalo ila fuatana nami kutoka hapa ili tuzungumze vyema nawe."
Akiwa na tabasamu lake lile baya alinipatia kikaratasi chenye namba 199. Pia alinipatia bahasha pana iliyo na kadi ya benki na ndani yake kulikuwa na barua yenye mà ndishi ya kiarabu.
"Hata hivyo sisi siyo watu wabaya nafikiri wewe hilo unalifaham vyema.Ndiyo maana tumekupatia msaada lakini utatakiwa ulipe."
Nikatabasam maana maneno yake na aliye mtangulia kuongea nami yamejaa mitego.Inaoneka wanahitaji kuniharibu kama naweza kusababisha madhara kwao.
Niliona napaswa sasa kumjulisha mimi ni nani ingawa sikuwa nataka kufanya hivyo kwa wakati kama huo maana nilikuwa katika uwanja usio wangu.Maana mcheza kwao hutuzwa,Niliamua niwe kinyume na shauri hilo.
"Mnahitaji vita ama amani pamoja nami maana kama ni vita nikianzisha mtapata hasara kubwa.Unajua ni nini kitaendelea baada ya eneo hili kunuswa na wahasim wenu?.... Jengo hili ambalo ni mboni yenu ya jicho itaanza kutembelewa na wasio hitajika."
Nilinyamaza kidogo kisha nikatoa begi hilo mgongoni.
"Ndani ya begi hili kuna siraha hatari sana nimezipata mikononi mwa wanajeshi hatari walio na ujuzi wa kukiangamiza kikosi chenye wanajeshi hodari 100 kwa siraha nyepesi kama kisu."
Wakiwa wamenikodolea macho wasijue wafanye kitu gani niliamua kuvua begi langu. Lenye siraha ambazo sikuwa nafikiria kuzitumia kwa muda kama huo.Nikachukua kisu kidogo kutoka kwenye mfuko wa begi na kuwapa ishara ya kunishambulia.
Wote walibaki kimya wasiweze kufanya jambo lolote zaidi ya kuitazama kama sanamu la nyoka.Niliweka mkao wa kupigana kwa kisu.Mkao huu hata mtu akiwa na panga ni ngumu kukishambulia maana unakufanya uwe mwepesi na kila pigo toka kwa adui unalitazama hata kabla ya kukishambulia.
Mtindo huu ni maarufu kwa jamii ya wajapani ambao ni ukoo wa Yakuza.Upendelea kutumia visu kama siraha yao kuu tofauti na Wajapani wengineo ambao upendeleo a upanga kama Samrahi.Ingawa kwa wengine kutumia kisu huiona kama silaha dhaifu ila kwangu huwa siraha muhimu maana unanisaidia kumkwepa adui kwa haraka na kufanya mashambulio ya kushitukiza.
"Kwa sasa tunaomba tusipigane na wewe maana muda wa hatari unakaribia.Jambo la kuzingatia ni moja soma ndani ya bahasha hiyo utajua la kufanya ukisha maliza kuisoma.Sisi ni wajumbe tu tumetumwa kukufikisha maelekezo toka kwa BUNDI MWEUSI."
Walipo maliza kutoa maelezo yao walitawanyika nami nikairudisha siraha yangu kwenye begi kana kwamba sina matumizi nayo.Nilinyanya begi langu na kuanza kuusaka mtaa wa pili toka kwenye hoteli ambayo sasa niliweza kuifahamu vyema inamilikiwa na mmoja ya watu hatari duniani.
Ingawa kwangu ni rafiki asiye fahamika zaidi ya kukutana katika kazi za hatari.Yeye huwa msaada wakati wa dharura pekee na mimi huwa mtangulizi katika kuleta hatari.
Bundi mweusi ndiye mtu pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kunisaidia mahali popote hata katikati ya vita angeliweza kuwasiliana nami.Maana alikuwa na mawakala kila mahali ambao nao hawakuwa wanamfahamu hata sura yake.
Maana hakuna aliye kuwa anafahamu anafanya kazi chini ya nani.Maana kazi yake ilimfanya asiwe na upande wowote.Ingawa nilijua ana upande ndiyo maana kamwe hakujulikana kwa sura.
Wapelelezi wa namna hiyo huwa ndumila kuwili kama unafanya nao kazi unapaswa kuwatambua kama taarifa alizozo kupatia ni sahihi ama ni mtego.Maana kama usipokuwa na uhakika unajikuta umeingia kwenye mtego bila kufahamu.
Nikiwa nimetembea kama maili mbili toka nilipokuwa nimepewa ujumbe na vijana wa Bundi mweusi nikihisi kuna watu wananifuatilia kwa ukaribu maana hisia zangu zilionyesha kuna marafiki wameamua kunifuata.
Laiti kama wangekijua wanaomfuata kiumbe wa namna gani na yapi anayo yapitia wangelibali maamuzi yao.Maana nilikuwa nimetamani kumwaga damu ya adui kuliko chochote maana kukimbizwa kulikuwa kumezidi kiwango cha uwezo wangu.Niliukumbuka msemo usemao.
"Mawindo yakiaamua huwinda,Na hapo sungura kumfukuza mbwa.
Niliamua kuwaonyesha methali kwa vitendo kuliko maneno.
(Viii)
Kwa kawaida huwa sipendi kufuatiliwa na wapelelezi wasio fahamu kujificha maana huwa vigumu kuwatofautisha kama ni raia wema ama ni adui.Maana waandishi wengi wa habari wale wanao husa hatari huwa na tabia ya kufuatilia tukio kwa pua na mdomo.
Na wapelelezi wanao kufunza kazi hii uanza kazi zao kizembe sana kama hawa ambao walikuwa wakimfuatilia.Maana walionekana wana wasiwasi ingawa tayari walikwisha ingia kwenye anga langu.
Kamwe nisingeliwaonea huruma hata kidogo maana walikuwa wamechagua kazi hiyo hatari,Kukifuta kifo huku wakiwa wamechagua njia mbaya zaidi kukikaribisha kwa macho na pua.
Nilikuwa nimepiga hatua zisizo kuwa kubwa sana lakini nikiwa na lengo la kuwavutia ndani ya mtaa ambao haukuwa na watu ili niweze kujiletea tuhuma na kuchafua mji kwa mshituko wa mapigano. Nilipo kuwa nimemaliza kukunja kona hapo ndipo nilifanikiwa kuona nakaribia mwisho mwa kichochoro.Lakini kwangu lilikuwa jambo zuri maana ningelikuwa kuwashambulia kwa kuwashutukiza na hakuna ambaye angeliweza kujitetea.
Aliye kutokeza akiwa wa kwanza nilimzawadia pigo hatari la judo ambalo nilikuwa nimekusudia kupiga Chemba ya moyo na kumzimisha maana sikutaka kuchelewa katika kufanya maamuzi .
Huyu wa pili baada ya kushuhudia mwenzake akifa kizembe alijipanga kwa ajiri ya pigano. Mtindo alioutumia kuwa ameuweka ni mtindo ambao hutumia akili kuliko nguvu Kungfu huyu niliona walau naweza kuchemsha damu.Maana mtindo huu huwa ni wa akili na mara nyingi hutumika kujilinda.
Nami niliweza mtindo kama wake na hapo nilianza kumshambulia kwa kasi sana lakini mapigo yote yenye kuweza kumletea madhara aliyapangua kama mchezo wa dirama.Na kasi yake ya kupangua ilikuwa ni nzuri hadi nikaanza kujuta kukubali kuweka mtindo wake maana alikuwa ni mjuvi sana kiasi nikaona nakaribia kutoka mchezoni kwa kasi yake.
Baada ya kuona sitaweza kwenda kasi yake maana alionekana ni mjuvi kama mimi hivyo nilitakiwa kuanza kutumia akili na ujuzi wangu wa ziada. Hapo nilibadisha mtindo wa kushambulia kwa kutumia ngumi nikaanza mtindo ambao huwa ni hatari katika medani za mapigano.Wushu mtindo wa kijapani ambao mtumiaji hutumia chenga la mwili kumlaghai mpinzani kisha uachia konde zito chini ya tayari ama kwenye mbavu changa.
Hivyo nilimsukumia ngumi nyingi za kasi lakini lengo langu kuu nilitaka hasahau kulinda sehemu za chini hasa kwenye kifua na tumbo ili nipate kumshambulia kwa ngumi yenye uzito wa kutosha. Nilifanikiwa kuzipata sehemu hatari kwake nami bila kuchelewa nilimsukumia ngumi ya kata funika ambayo hupigwa kwa lengo la kuvunja mifupa.Hapo niliweza kusikia sauti ya mvunjiko wa mifupa ya mbavu.Halibaki akiwa amejihinamia baada ya kumshambulia kwa pigo hilo hatari.
"Unaweza kuniambia kwanini mnanifuata kwa dhati na ni nani aliye watumwa?"
Nilimuuliza lakini nilifahamu asingeliweza kunipa majibu yangu kwa muda huo.
Alinitaka kwa tabasamu lake kisha akaniambia neno ambalo hata mimi kama nikiwa katika hali kama yake ningelisema.
"Unajua siwezi kusema hata kama ukinipa mateso na hiyo ni kanuni ya kazi yangu hivyo hacha kupoteza muda wako bure kwa kuniuliza maswali ambayo siwezi kukupa majibu yake."
Hapo hapo alijin'gata ulimi wake na kuaga duniani mbele ya macho yangu.Damu ilinisisimka maana kukutana na majasusi ambao wapo tayari kufa kuliko kutoa siri ilikuwa ni ishara mbaya sana kwangu. Maana kanuni kama hiyo mara nyingi hutumika na vikosi vya siri ambavyo havitakuwa kamwe uwepo wake ujulikane kwa jamii ama vikosi vya kiharifu na magaidi kama vile Alkaida na Mafia.
Niliisogelea miili hiyo na kuanza kukagua ili nipate kufahamu ni watu gani.Lakini hakuna nilicho ambulia zaidi ya kupata kadi tatu za benki, Bunduki aina ya UZI,visu vya kukunjwa viwili na pesa za Kimarekani kiasi cha dola 2000$,
Lakini wakati namaliza kuchukua vitu hivyo niliona jambo la ajabu katika mikono yao ya kushoto.Kulikuwa na alama ya mchoro wa kisu kinacho tiririsha damu.Machoro huu ulionyesha jambo ambalo sikulitazamia kamwe kukutana nalo katika nchi kama huo.Maana ni alama ya kundi hatari la wauaji wa kulipwa.
Kundi hili linamilikiwa na Mwitalia katili Don Tadero ambaye yupo katika ukoo wa kiharifu la MAFIA.Kazi ya kikosi hiki huwa ni kutekeleza mauji ya viongozi wa kisiasa kwa malipo.Kundi hili pia hutumiwa na serikali mbali mbali kuwaondoa watu ambao ni hatari kwao . Lakini ili kujificha uhusika wao huwakodisha wauaji hawa ili watekeleze kazi zao kwa siri.
Hivyo kuonekana kwa watu hawa nilijua kuna watu wanahitaji kunitoa kwenye mchezo mapema ingawa sikuwa nafahamu lengo lao ni lipi?.
Kuna msemo usemao kuishi karibu na mahakama si kigezo cha kuzifahamu sheria.Huenda msemo huo una ukweli ndani yake.Maana pamoja na kuishi kwenye mfumo wa kijeshi kwa muda mrefu kamwe sikuwahi kujihisi nafahamu mambo ya jeshini kwa kuwang'oa cha kutosha.
Maana dalili mbaya zaidi ambayo ilinifanya nijione bado sijafahamu jeshi kwa kiwango cha kutosha ni wakati wa mashambulio ya kujitoa mhanga.Kipindi kama hicho huwa kigumu kwa mwanajeshi anaye nusurika kufa.
Maana hujiona ameponyoka toka kwenye tundu la sindano .
Mwingine hufikiria hata kuachana na jeshi akawe raia mwema.Lakini jambo la ajabu hutokea baada ya kumaliza kuwazika walio kufa naye hujiona hao walio kufa wamekufa kwa ujinga wao ama wamekufa kishujaa.
Kwa kuwa mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke amekuwa kiumbe kinacho sahau na kukubali matokeo hurudia hali yake na kusahau yaliyopita.Mambo machache niliyoweza kuyafaham yaliniweka mbali zaidi na hatari ya kifo.
Siku zote niliutazama uhai kama kitu cha pekee sana ambacho unaweza kukipoteza na kisipatikane kamwe.
Sikuwahi kuua bila kuwa na sababu maalum na niliua kwa sababu ya kuutetea uhai wangu na wa wengine.
Wakati mmoja tu ndipo niliweza kuua kwa sababu ya kuficha makucha yangu ya wema.Maana kuishi na wauaji usiwe muuaji ni kazi kubwa.Tukio hilo lingali linanitesa hadi leo hii maana nililazimika niue kikatili raia wasio na hatia.
Mnamo mwaka 2011 nikiwa katika kazi maalumu ya siri ambayo nilikuwa nimepewa kwa siri kwa ajili ya kulinda masilahi ya Wapalestina nchini Afghanistan.Nilikuwa mmoja wa wapiganaji wa waislamu wenye msimamo mkali. Kuna siku nililazimika kuua familia moja ya kizungu ambayo ilikuwa haina hatia.Maana wao walikuwa watu ambao ilionekana haina msimamo upande wowote.
Hivyo nilitakiwa kuua baada ya kuwa wenzangu wote walikuwa wamekwisha kuua.Wakati wangu wa kumwaga damu ulinikuta katika nyumba hiyo hivyo hakuna ujanja wowote ningeliufanya ili kuwaokoa.
Lakini wakati huu nilikuwa nimetumia katika vita ya kuutea uhai wa ndugu yangu.Ambaye alitakiwa aendelee kuishi hata kwa kuimwaga damu yangu maana sikuwa na cha kupoteza zaidi katika ulimwengu huu wenye kujaa usaliti.Nilitakiwa kuua kwa kusudi wakati huu tena kusudi la kujitetea kizazi changu kisifutike katika uso wa dunia.Kamwe sikutaka kuwa kibaraka wa wazungu tena.
Walio watuma wauaji kuniua walikuwa wamejitangazia vita lasmi na chui maana hupaswi kumtazama chui usoni na kuendelea kumtazama.Maana huo ndiyo mwisho wako.Hivyo na wao walikuwa wameingia kwenye orodha ya kutafutwa na lazima ningeliwapata.Labda waishi kusiko fikika kwa wanadamu ambapo ni mahali dhahania kama mbinguni na kuzimu.Lakini kwa sababu ni mahali pasipokuwepo walipaswa wanitaze tena wakiuacha uhai wao.
SPECIAL ACTIVITIES DIVISION.
**********ISRAEL**************
Sina kumbukumbu ya amani katika maisha yangu yote ambayo nimekuwa hapa duniani.Nilizaliwa miaka Ishirini na tisa iliyopita katikati ya uwanja wa vita.Baba yangu alikuwa ni mmoja wapo wa makamanda Jeshi la Israel.
Hivyo nimezoe kuziona siraha za kila aina za kivita.Maisha yangu ya utotoni sikupata hata nafasi ya kucheza mpira kama vijana wanao ishi katika nchi nyingine ulimwenguni.Maana michezo pekee ambayo nimezima kuiona ni mapigano.
Utotoni mwangu
kujifunza kuendesha mambo ya kivita.Ikiwemo kuendesha magari ya kila aina ya kivita ningali na umri mdogo.
Siku moja ambayo ilikuwa mbaya kwangu nilikuwa kati ya askari wa Israel ambaye nilipewa ujumbe wa siri wa kujiunga na mafunzo maalum ya kijeshi.Ingawa nilikuwa ni muuji wa kuaminika katika kitengo cha KIDO.
Kido ni kitengo cha kijasusi kinacho husiana na mauaji.Lakini ili kujiunga unakuwa umepitia katika mafunzo ya hali ya juu.Wengi wanaojiunga na KIDO hutakiwa kuwa ni Waisraeli wa damu kabisa.Ambao hutakiwa kuwa Wazalendo wa nchi hii.Nami nilikuwa nimetimiza mengi katika nchi yangu.Hivyo nafasi ya kuwa mmoja wa Majasusi wa Kido ilikuja kwa uwazi kwangu.Maana pamoja na kuwa ni mpiganaji hodari nilikuwa na kipaji.
Maana niliwahi kushiriki kwenye kiwanda cha uundaji wa ndege za kivita.Pia nilikuwa ni mmoja wapo ya watu walio uundaji helkopta ya kisasa ya Mmarekani aina ya SH-60J.
SH-60J
Ama kwa jina la utani Seahawk, ni kati ya Herkopita bora ya jeshi la Marekani.Mara ya kwanza tulipo kazi hii tulitakiwa kuirekebisha Helkopita aina ya UH -60 ambayo ilihitaji mabadiliko makubwa ya muundo ili kuibadilisha na kuipa muundo bora kwa ajiri jukumu la kupambana na manowari.
Lakini kutokana kuwa na muda wa kutosha tulipata wazo tofauti la kuiunda helkopta aina yaSH-60.
Muundo huu tuliupata ambao ulikuwa ukitumika nchini Japani chini ya leseni ya Sikorsky. Hivyo tulipo changa ya ujuzi na muundo wa ndege hiziSH-60B na SH-60F, tukaiondolea mlio wa avionik tulijikpata katika toleo bora kabisa la ndege ya kivita isiyo na sauti.
Kulingana na dhana ya JMSDF, HQS-103 Dipping Sonar, HPS-104 inayofanya kazi kwa njia ya elektroniki unaweza kukwepa ama kuzima Rada ya kwa kubofya sehemu ya rada system ambayo ilipachikwa kwenye kibofu ya kuongoza ndege hii.Pia ndege hii tuliiongeze vifaa vya Mfumo wa HLR-108 ESM wa avionics ya SH-60B na kuifanya iwe tofauti na Helikopta nyingine za kijeshi. Injini ni GE / IHI T700-IHI-701C turboshaft, ambayo Ilitengenezwa na kiwanda cha kijeshi-Harima Heavy.Helkopita hizi kwa sasa zipo hamsini tu ulimwenguni.
Helikopta moja tu ambayo ilipotea na askari wa kulinda dolia katika anga la Iraq lakini bado inatafutwa maana inasemekana ilishambuliwa na wanamgambo wa Tarban.
Lakini kuna tukio ambalo huwa bado linanisumbua kichwa hadi leo hii.Maana kuna mwanajeshi mmoja ambaye alikuwa amenizidi ujuzi kwa kila kitu aliweza kupotea katikati ya misheni hatari.
Ingawa alikuwa ni rafiki kwangu ila matukio aliyokuwa anayafanya yalikuwa ni mazito na mara nyingi alipenda kufanya kazi akiwa peke yake.Kamwe hakupenda amri kama desturi za kijeshi zilivyo lakini hakuwahi kuipinga amri.Lakini nakiri mimi nilimfahamu kwa kiwango kikubwa kuliko yeyote.
Tukio ambalo lilinitenganisha naye lilikuwa kati ya misheni za muda mrefu ambazo tulikuwa tumepewa.
Lakini kuna tukio ambalo alifanya kinyume na makubaliano ya mkuu wetu ambaye kamwe nami sikuwahi kumfahamu.
Ingawa tulikuwa tumeambiwa haruhusiwi kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Wapalestina hata iweje lakini yeye alioa tena kwa ndoa ya Kiislamu kabisa.
Na bado hakuishi kuoa nahisi ndiye alivuruga mpango wa kumuangamiza kiongozi wa Tarban kwa kisu ama sumu .Baada ya kufeli kwa matukio ya kimya aliweza kusababisha taifa langu kutumia ndege za kivita kushambulia kambi nzima.
Nimebaki kumkumbuka kama adui aliye na urafiki ambaye ni ngumu kumuangusha kwa risasi.
Siku zote nilitamani kuwa na uwezo kama wake ama zaidi.Maana nilijua ndicho kitu pekee kitakachoweza kunisaidia kumdhibiti komandoo wa daraja lake.
Siku zote nilitamani kuwa juu na nilifanya yote niwezavyo ili niwe katika sehemu bora ya kunifua na kunipa uwezo mara dufu ya makomandoo wa kawaida katika jeshi na katika kikosi changu cha KIDO.
Lakini kuitwa katika kikosi tofauti na nchi yangu tena kwa siri ilikuwa ni mitihani kwangu kukubali.Maana nilikuta katika kikosi chenye kazi maalumu kwa ajiri ya kuukomboa ulimwengu wa wasio na nguvu kupitia kivuli.
Kikosi maalum cha Special Activities Division.
Kikosi hiki kiliundwa kwa malengo ya kuwaondoa watu hatari.
Kutokana kuongezeka kwa changamoto za kimataifa , ambazo nyingine zinatishia usalama au maslahi ya mrekani lakini marekani haiwezi kuchukua hatua zozote kutokana kujiepusha na lawama kutoka jamii ya kimataifa na ndipo hapo ikaonekana kuna umuhimu wa kuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya suala hili.
Ndipo hapa ambapo serikali ya marekani ikaagiza shirika la kijasusi la CIA kuanzisha kitengo maalumu ndani yake ambacho kitakuwa na maafisa (wanajeshi) ambao wanaweza kutekeleza oparesheni yoyote ya kijeshi kwa kujitegemea pasipo kuhusisha serikali ya marekani.
CIA wakaanzisha idara maalumu ndani yake na kuuita Special Activities Division au kwa kifupi SAD ambayo idara yenyewe ilikuwa na maafisa wa siri ambao hawabebi vitambulisho na majina yao ni siri kubwa hayawezi kupatikana hata kwenye orodha ya maafisa wa CIA.
Lengo kubwa la kuanzishwa kwa idara hii ni kutekeleza oparesheni maalumu za kijeshi au proaganda na iikitokea wakakamatwa au kushitukiwa basi serikali ya marekani wanawakana kuwa si maafisa wao.
Kwahiyo kitengo hiki kilikuwa kinafanya kazi kwa niaba ya serikali ya marekani lakini kulikuwa hakuna uwezekano wowote wa adui kuunganisha uhusika wa kikosi hiki na serkali ya marekani.
Ndani ya Idara hii ya SAD kuna vitengo vidogo viwili;
Kitengo cha kwanza kinaitwa Political Action Group: kitengo hiki kazi yake kubwa ni kufanya ushawishi wa kisiasa (political influence), oparesheni za kisaikolojia (psychological operations) na vita za kiuchumi (Economic Warfares). Pia kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, kitengo hiki kimeongezewa jukumu la vita za kimtandao (cyberwarfares).
Tuchukulie kwa mfano; katika nchi fulani kuna serikali au mwenendo wa serikalin unatishia maslahi ya Marekani basi kitengo hiki kinaingia kwa siri kubwa na kufanya mojawapo ya mambo ambayo nimeyaorodhesha hapo juu.
Moja ya matukio ambayo kitengo hiki kimehusika sana na CIA wamekiri kwenye nyaraka zilizowekwa wazi mwaka 2013 ilikuwa ni kueneza propaganda ambayo ilichangia kupinduliwa kwa Rais wa Iran mwaka 1953 ambapo kisa hiki nitakieleza kwa kina katika makala hii.
Pia kitengo hiki kilitumika kuzuia chama cha kikomunisti cha Italia kushinda uchaguzi mwaka 1960.
Pia kitengo hiki kimewahi kufanya oparesheni ya siri iliyoitwa Operation Mockingbird katika taifa la marekani. Oparesheni hii ilikuwa na lengo la 'kucontrol' habari zinazoandikwa na Vyombo vya habari nchini humo.
Oparesheni hii imekuja kupingwa vikali siku za karibuni na baraza la seneti kwa kuwa sheria hairuhusi CIA kufanya oparesheni yeyote ndani ya ardhi ya marekani.
Kitengo cha Pili kinaitwa Special Oparatins Group (SAG); na kazi yake ni kama ifuatavyo;
Kitengo hiki kinajumuisha wanajeshi wenye weledi wa hali ya juu kutekeleza malengo ya kivita pasipo kujulikana uhusika wa serikali ya marekani.
Ili kulinda utambulisho wao, wanajeshi wa kikosi hiki maalumu hawavai sare za jeshi wala kubeba vitambulisho.
Inaelezwa kuwa hiki ndio kikosi maalumu cha oparesheni za kijeshi chenye usiri mkubwa nchini marekani.
Maafisa wa kitengo hiki wanapatikanaje??
Maafisa wote wanaojiunga katika kitengo hiki maalumu cha SAD wanachaguliwa kutoka katika vikosi vingine vya weledi vya jeshi la marekani mfano Army Rangers, Combat controllers, Delta Force, 24TH STS, US Army Special Forces, SEALs, Force Recon n.k.
Ukisha chaguliwa unapelekwa katika kituo maalumu cha mafunzo ya CIA kilichopo Virginia kinachojulikana kama Camp Peary (au maarufu kama 'The Farm') ambapo miezi 18 ya kwanza wanakufundisha kuhusu intelijensia na ushushushu.
Baada ya miezi 18 hiyo wanakupeleka kwenye kituo kingine cha CIA kilichopo California ambacho kinajulikana kama 'The Point'.
Hapa wanakufundisha mafunzo ya hali ya juu ya kijeshi ambayo hayapatikani kwa kiwango hicho katika vikosi vingine vya marekani.
Ukiwa hapo utafundishwq mapigano ya ana kwa ana ya kiwango cha juu zaidi (special hand to hand combat), kutumia karibia aina zote za silaha na milipuko ya jeshi la marekani na nchi za kigeni, ufuatiliaji adui (tracking)
Kukabiliana na hali ngumu kwenye mazingira ya kawaida na nyikani ( extreme survival and wilderness train ing), Kumkwepa aduia, kuzuia adui na kutoroka adui (evasion, Resistance and escape - SERE) na pamoja na mafunzo hayo unaongezewa kozi maalumu ya kutambua fiziolojia ya binadamu (Udaktari).
Ukisha fuzu mafunzo haya kwa muda wa miezi 36 unakabidhiwa katika idara ya SAD ndani ya CIA na hapo unatambulika kama "Afisa Mwenye Mbinu Maalumu" (Specialized Skills Officer).
Katika oparesheni za SAD unapaswa kutekeleza misheni mkiwa katika vikundi vya watu wachache sana wasiozidi sita na oparesheni nyingine zinatekelezwa na Afisa mmoja pekee.
Katika Ofisi za CIA zilizopo kitongoji cha Langley jijini Virginia kuna ukuta wa majina ya Maafisa wa CIA waliotunikiwa tuzo za heshima kutoka na utumishi wao uliotukuka ( Distinguished Intelligance Cross na Intelligence Star). Majina ya maafisa wengi kwenye ukuta huo ni ya wale waliotumikia kitengo cha SAD ndani ya CIA.
Ni idara hii maalumu ya CIA ambayo ilikawabidhiwa raia wanne wa Tibet kutoka kwa kaka mkubwa wa kiongozi wa kiroho wa Tibet Mtukufu Dalai Lama ambapo idara ya SAD iliwapa mafunzo ya kikomando watibeti hao kisha wakawarudisha Tibet kutafuta raia wengine 300 ambao SAD iliwapa mafunzo ya kijeshi kwa siri katika kisiwa cha Saipan na mwezi oktoba SAD ikawaongoza wanajeshi hawa mpaka Tibet kuanzisha vuguvugi la kudai kujitenga na China.
Pia ni kikosi maalumu hiki cha idara ya SAD ambacho kilimtorosha kwa siri mtukufu Dalai Lama kwa kupita katikati ya majeshi ya China yaliyokuwa mpakani na kumpeleka India.
Mpaka leo haijulikani ni namna gani waliweza kufanya tukio hili.
Ni idara hii ya SAD ndani ya CIA ambayo ilihusika kuwapatia mafunzo ya kijeshi raia wa Cuba waliokuwa wanaishi uhamishoni na kuwaongoza katika jaribio la kumpindua Fidel Castro. Mapigano haya yakihistoria yalidumu kwa siku tatu na yanajulikana kwa jina maarufu la 'Bay Of Pigs Invasion'.
Jaribio hili la mapinduzi halikuwezekana na ndilo lililochangia kudorara kwa mahusiano kati ya Marekani na Cuba mpaka leo hii.
Kwa mujibu wa nyaraka za siri za CIA zikizowekwa wazi mwaka 2004. Amri ya kumpiga risasi Che Guevara katikakati mwa miaka ya 1960 ilitoka kwa makomado wa SAD.
Ilikuwaje; Jeshi la msituni lililojiita Jeshi la Ukombozi la Bolivia (National Liberation Army of Bolivia) lilianzisha vita dhidi ya serikali ya Bolivia ambayo ilikuwa inaungwa mkono na Marekani. Jeshi hili likuwa na vifaa vya kisasa na liliungwa mkono na mwanamapinduzi Che Guevara.
Katika hatua za mwanzo za mapigano jeshi hili la waasi lilionekana kushinda dhidi ya majeshi ya serikali.
Ndipo hapo CIA wakatuma makomando wa kitengo cha SAD ambao walienda kutoa mafunzo kwa majeshi ya Bolivia katika milima Camiri. Na baada ya hapo wakawaongoza kupigana na waasi na kufanikiwa kuwashinda. Kisha makomando wa SAD wakawaongoza makomando wa jeshi la Bolivia (Bolivia Special Forces) kumkamata Che Guevara ambapo Mara tu baada ya kukamatwa komando wa SAD aliyeitwa Felix Rodriguez akaamuru auwawe.
Hii ni mifano michache kati ya mifano mingi amabayo CIA kwa kutumia kitengo cha SAD wameendesha opesheni maalumu za kijeshi katika nchi nyingi.
"Baada ya kuwa nimepata mafunzo na kutekeleza misheni ladhaa za majaribio nilitakiwa kurudi katika nchi ya mababu zangu ambako pia nilikuwa nimebadilika kuanzia tabia hadi umbo.Sikupaswa kuwa yule aliyekuwa ni mtu wa watu na mtukufu wa mambo ya teknolojia."
Jina langu la kazi kwa wakati huo lilikuwa Abdillah Azizi Bin Huseni.Code name yangu mpya ikiwa ni Black Bird.Jina ambalo nililipata kutokana na kuwa mwendeshaji bora wa ndege hiyo ya kivita.
Jina langu la asili nilibaki nalo tu kama kibandiko maana sikupaswa kulitumia tena katika sehemu yeyote ile katika ulimwengu huu.Maana nilipaswa kuishi sitini na kusahau yote yaliyotokea na niliyokuwa nimeyafanya hapo awali.
Nilikuwa nimekuja katika nchi ya Parestina kwa oparesheni maalum.Oparesheni ya kuwatafuta watu hatari kwa taifa la Israel na Marekani na kuwaangamiza kwa njia iliyo boresha.Maana hakupaswa kuwepo ushaidi wa kitakacho wapata.Ili kuzuia taharuki na vita kubwa zaidi.
"Nilikuwa nimeingia katika nchi hizi ya Parestina kwa kutumia kivuli cha Mfanyabiashara ya Mafuta.Na kufikia wakati huo nilikuwa nimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kumiliki vituo viwili vya mafuta.Lakini kazi iliyo kuwa imenileta katika nchi hiyo ilikuwa bado.Na bado muda wa kuitekeleza ulikuwa bado haujatimia.Maana nilipaswa kupokea ujumbe toka kwa watu maalum ambao bado nilikuwa sipaswi kufahamiana nao.Nao hawakupaswa kunifaham.
Maana katika kazi hii kujificha na kuhuficha uhusika wangu ilikuwa ni muhimu kuliko chochote.
Nikiwa natokea katika msikiti mkuu wa Al-Aqsa ambao jamii mbili ziliruhisiwa kushiriki.Saa yangu ya kijasusi ikilia mlio wa kunijulisha kuwa kuna ujumbe.Nilikwenda moja kwa moja hadi kwenye gari langu ambalo nilikuwa nimeliegesha mbali kidogo na msikiti huo.Kisha nilifungua simu tyangu kukuta ujumbe ulio kuwa umetumiwa kwa njia salama ambao ulikuwa na maelezo machache ya kumuondoa mtu hatari.
Kwanza nilibaki kinywa wazi mtu hatari ambaye alikuwa amewekwa katika sehemu hiyo ni mmoja wapo wa makomandoo hatari walio kuwa wanauwezo mkubwa.Jambo baya zaidi ni mtu aliye kuwa rafiki yangu.Jambo ambalo lilimuacha kinywa wazi ni uhusika wake na magaidi.Alikuwa ametoroka gerezani na kuua askari wa Israel wawili,akiwa ameondoka na siri nzito ambayo haikupaswa kufika kwenye mikono isiyo salama maana angelikuwa ameumwagia mafuta ya taa mzozo wa Parestina na Israel.
Jambo ambalo hawakulifaham walio nipa kazi ni uhusiano wetu na mtu huyu hatari.Maana nilifahamu hapendi kuwidwa.Ukimuwinda unakuwa unampa nafasi ya kukuwinda wewe kwa udi na uvumba.
Hivyo niliona ni bora nimpe mtu kazi hiyo kwa ajiri ya kuifanya kwa niaba yangu.
Niliingia katika mtandao wa Dark Web na kuwatafuta wauaji wa kulipwa ambao walikuwa wamefungua tawi lao hapa Parestina.
Niliwapatia maelezo na picha ya mtu ambaye walipaswa kumuondoa kwa usiku huo.Baada ya kuwa tumekubaliana kwa kila kitu niliwasiliaha malipo na kusubiria majibu ya kazi yao.
Lakini kama utani baada ya nusu saa tangu nitoe ofa hiyo nilipata ujumbe wa kunikatisha tamaa.Maana niliokuwa nimewapatia kazi waliniambia wameshindwa kumpata akiwa hai mtu zaidi ya kuwaualia wapambanaji wao. Ingawa nilijua watakipata na kuumizwa ila uharaka wao ulinipa majibu sahihi ya kumpata siku hiyohiyo adui yangu.
Mazingira ambayo wauaji hawa wa kulipwa walikuwa wamejiwekea nilijua kama nikiyafuatilia nitampata akiwa karibu.
Niliwasha gari langu na kuanza kuifuata mitaa hiyo ya Gaza. Niliamua kutokubeba siraha maana nilikwenda mahali walipo watu hatari.Kubeba siraha ilikuwa ni hatari ya kujitakia mwenyewe bila kulazimishwa.
Nikiwa nakaribia kituo cha redio na televisheni ya Al-Aqsa. Sehemu ambayo niliwahi kuishambulia kwa bomu la ndege aina ya Mi-28N Night Hunter.
Helikopta ya Kirusi yenye kasi 162 knots [186 mph or 300 kmph]
Kasi yaCruise: 145 knots [167.7 mph or 270 kmph]
Toleo : 126 ambayo ilikuwa imebeba makombora ya kuweza kusambaratisha mji majengo makubwa.
Niliweza kumuona mwanamke ambaye alikuwa na uhusiano na kiongozi wa Jamaa.Ismail Haniyeh ambaye ndiye alikuwa taget yetu katika misheni iliyo tangulia hapo kabla.Nyumba yake ni kati ya nyumba ambazo nilizishambulia kwenye usiku wa tarehe ishirini na tisa mwezi julai mwaka elfu mbili kumi na nne.
Mwanamke huyo namkumbuka maana alikuwa chanzo cha kunifanya niue watu kinyama kwa maana alimfanya rafiki yangu awe adui.Hivyo nilipo muona anatoka kwenye kituo hicho cha habari nilijua ndiye atanipa mwangaza wa kumpata mtu hatari maana udhaifu wake pekee ambao nilifahamu ulikuwa mbele yangu.
Hivyo nilishuka na kuanza kumfuatilia kwa macho yaliyo fichwa nyuma ya miwani.Muda si mrefu nilimshuhudia akiingia kwenye jengo kubwa mali ya kituo hicho cha habari.Ndiyo nyumba hii ilikuwa ni ile ile ambayo nilikuwa natembelea mara nyingi.Ingawa kwa sasa ilikuwa imerembeshwa kwa rangi nyeupe.
Nilisubiri kama dakika tano kisha nami nilisogea kwenye mlango wa nyumba hiyo na kubisha hodi kwa mtindo ambao tulikuwa tunatumia hapo zamani.
Maneno yale yale ambayo nilikuwa natumia nilipo kuwa nawapeleleza wanamgambo wa Tarban niliyasikia yakinipatia majibu tokea ndani.
Hatimaye mlango ulifunguliwa na macho yangu yakawa yanatazamiwa picha mbaya kwa wakati huo.Mtu ambaye alikuwa amenifanya niwe hapo alikuwa mbele yangu akiwa na bunduki hatari aina ya IWI X95 TAVOR SMG.
Alinifanyia ishara ya kuingia ndani nami nilitii maana madhara ya siraha hiyo nayafahamu yalivyo mabaya.
Aliniamrisha kwa alama nifuate njia ya chini ambako nakumbuka kulikuwa na chumba cha mazoezi.Lakini chumba hicho wakati fulani tulikuwa tunakitumia kuhifadhi siraha za mateso.Maana alikuwa hapendi kuona siraha hizo zilitumiwa mara nyingi.Hivyo nilijua huenda ana lengo la kuhitaji kuzitumia kwangu.
Nilipo ufikishe mlango wa chumba hicho nilisikia sauti ya kuigwa kwa bunduki yake kwa nyuma.Ishara ambayo bado nilikuwa naikumbuka maana kama ungelisikia bunduki inagogwa hivyo unatakiwa ugeuke uangalie nyuma.
Hivyo niligeuka na kumkuta akiwa bado ameshikilia bunduki kama mtu ambaye anahitaji kuniua.Lakini alikuwa hasemi jambo lolote zaidi ya kunitazama.
Hatimaye niliona nivunje ukimya nimuulize lengo lake la kuniweka chini ya ulinzi ni nini?
"Kwanini umenifanya mateka Komred hili hali unanifahamu vyema nami nakufahamu?"
Nilimuuliza nikiwa katika utulivu wangu wa siku zote maana nilikuwa nafahamu tabia yake ya kusoma ufahamu na kupima swali lako.Maana nilikuwa namkubali kwa kipawa chake cha kipekee cha kutafuta majibu bila kuuliza muhusika.
"Utakuwa unahitaji mambo mawili ama matatu toka kwangu maana wewe kwa sasa ni mtu mwingine tofauti na yule ambaye nilikuwa naishi naye."
" Wewe kwa sasa ni muuji aliye pewa ruhusa na kuaminiwa na ulimwengu huu"."Unaweza kuwadanganya wengine kuhusika kwako na mauji na jina lako lakini mimi kamwe hutonidanganya."Maana mahali uliko pitia nami nilikwisha kupitia hapo hapo uenda tupo katika safari moja lakini wewe umeamua kujifanya upo mbali nami"."Kumbuka walio kutuma ufanye kazi hii ya kuniua waliwahi kunipa kazi hiyo hiyo ya kuua."
Alisema maneno ambayo yalinifanya nibali kinywa wazi maana ni kama kazi yangu haikuwa ya siri.Maana mtu nilikuwa takiwa kumuua amefaham nahitaji kumuua.Jambo ambalo si la kawaida katika utendaji kazi wangu maana mimi hufanya kazi zangu kwa siri na kuingia katika nchi hizi ilikuwa ni siri.
Kichwani nilibaki najiuliza nani kaniuza kwa muuji huyu anaye nifaham.Nilijiona kama mbuzi wa kafara maana hakukuwepo ujanja tena kila kitu alikuwa amekifahamu.
Niliamua kumjibu kwa kuulizia maana ukichwa wake nilifahamu akiwa amekasirishwa anaweza kumuua bila huruma.
"Wewe nani kakuambia nimetumwa hapa kukutafuta maana si rahisi kwako ambaye umetoka gerezani kuyafahamu haya yote. Niambie maana naona nafanya kazi ya kuuzwa kwako ili imalize hata kabla ya kukumbatia na kujuliana hali yako"
Alinitazama kisha akaanza kuniambia mambo ambayo nilikuwa nayafahamu.
"Adui ni adui hata kama ni mzazi wako akikaa upande wa adui ni adui.Hupaswi kumuonea huruma maana yeye akipata nafasi atakuwahisha kwenye kifo"
Akitabasamu tena kisha akaishusha siraha yake na kuiweka mbali na yeye.Kisha alichomoa magazine ya risasi na kunipatia.
"Mimi ni kama wewe tu natumika kama siraha ya maangamizi.Lakini nimesha jitambua ndiyo maana umetumiwa kuniua.Siku moja itafika na wewe utajitambua hivyo utatumiwa wauaji wakuue maana unayo siri.Siri ambayo unapaswa ufe nayo hata kama ukipitia hali gani.Maana ni kwa ajili ya maslahi ya wachache na kizazi chao."
"Leo nitakuambia yaliyo pande hizi mbili yaani upande wa Parestina na Israel.Sitapendelea upande wowote maana mimi nimeshiriki damu ya pande zote mbili."
"Niliendelea kumsikiliza maana alionyesha anayo mengi ya kunifahamisha.
CHANZO CHA VITA KATI YA PARESTINA NA ISRAEL
"Mgogoro kati ya nchi hizi mbili umeanzia mbali sana.Tunaposema mashariki ya kati tuna maana eneo zinapopatikana nchi hizi Iraq, Jordan, Israel, Egypt, Sudan, Syria, Lebanon, Saudi Arabia, Kuwait, Iran, Turkey, Yemen, United Arab Emirates, Palestina na Oman
Mengi kati ya mataifa haya ni ya kiarabu kwa maana kuwa idadi kubwa ya wananchi wake ni waarabu isipokuwa Israel, Turkey na Iran yenye watu mchanganyiko."
"Wayahudi ni uzao wa Ibrahimu ambaye inasemekana aliishi yeye na wazazi wake katika nchi ya Iraq ya sasa kabla ya kuambiwa na Mungu atoke na kwenda katika nchi atakayompatia ambayo ni Palestina ya sasa japo wakati huo ilikuwa ikiitwa Kanaani".
"Mungu alimwapia Ibrahimu kuwa kupitia yeye litazaliwa taifa na watairithi ardhi ya Kanani yenye utajiri mwingi. Hiyo ni kwa mujibu wa vitabu vya dini. Ibrahimu anaheshimiwa na wote wakristo kwa waislamu kama baba yao kiimani."
"Mpango wa Mungu kumfanyia Ibrahimu taifa na kuwarithisha nchi ile aliyomuahidi Ibrahimu ulikamilika pale alipowatoa watoto wa Israel(uzao wa Ibrahimu) utumwani Misri na kuwaleta katika nchi ya Caanani ambayo alimwahidi Ibrahimu baba yao kuwa angewapa waitawale. Japokuwa nchi hiyo ilikuwa tayari ina wenyeji ambao ni mataifa tofauti tofauti yalikuwa yanaikalia. Wana wa Israel walitakiwa kupigana na mataifa yote yaliyokuwepo na kuyashinda ili kuiteka nchi ile na kuweka dola yao. Na walifanikiwa kufanya hivyo na wakaanzisha taifa lao la Israel."
"Chimbuko la mgogoro au uhasama kati ya wayahudi (Israel) na Waarabu (Palestina)ni kuanzia karne ya kwanza baada ya Kuzaliwa Kwa Yesu Kristo (A.D. 71). Katika kipindi hiki Wayahudi waliondoka katika nchi yao (Homeland) wakikimbia au kukimbizwa na WARUMI (Romans). WARUMI walipoivamia Israel waliifanya kuwa kama jimbo mojawapo la dola ya kirumi."
"Baadaye Waisrael wakaasi na kupigana vita na WARUMI kisha wakashindwa vibaya. Wakapigwa marufuku kuishi katika mji wao wa Jerusalem na kutakiwa kuondoka mara moja. WARUMI wakalipa jimbo hilo jipya waliloliteka jina "Palestina."
"Walitoka katika eneo lao ilipo Israel na Palestina kwa sasa. Kwa wakati huo dola ya kirumi ilikuwa kubwa,yenye nguvu ikitawala eneo kubwa sana la mashariki ya kati na katika sehemu ya Ulaya
Ni jamii za wayahudi wachache sana waliobakia eneo hilo la Israel ya zamani lakini wengi wao walikimbilia uhamishoni katika mataifa mbalimbali ya Urusi, Ufaransa, Ujerumani, Switzerland na kwingineko ili mradi wawe salama."
"Baada ya miaka ipatayo 1700 baadaye Wayahudi wachache walianza kurejea kidogo kidogo katika nchi yao (Homeland) ambapo ndipo yalipo mataifa ya Israel na Palestina kwa sasa. Walipowasili katika eneo lile la nchi yao walikuta Waarabu (Wapalestina) wamelishikilia yaani wanaishi hapo tayari".
"Kwa maneno mengine walibadili pale baada ya wao kuwakimbia Warumi na kwenda kuishi uhamishoni katika mataifa mengine kwa miaka mingi. Dola ya Kirumi baadaye ilikuja kusambaratika na kufa hivyo maeoneo yake iliyokuwa ikiyamiliki kuwa huru."
"Hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 19 walikuwa ni Wayahudi wachache sana waliokuwa wamerejea wakiishi na Wapalestina kiasi kwamba Wapalestina hawakuwaona kama wangekuwa ni tishio kwao."
Tunapataje kujua historia hii kuwa eneo la Wapalestina hapo awali lilikuwa likikaliwa na Wayahudi(Waisrael)? Ushahidi upo wa aina kadhaa;
Ushahidi katika vitabu vya dini.
Ushahidi katika vitabu vya Kihistoria"
"Ilipofika mwaka 1897 baadhi ya Wayahudi walioishi uhamishoni Ulaya mathalani Switzerland waliamua kuunda umoja wao wa kuwaunganisha Wayahudi wote popote pale au nchi yoyote waliyopo duniani. Kuhamasisha undugu na mshikamano miongoni mwao popote walipo katika mataifa waliko tawanyikia. Hii ni kwa sababu walipokuwa wakikimbia walielekea mataifa tofauti tofauti.
Umoja huo ulijulikana kama "WORLD ZIONIST ORGANIZATION". Maono ya viongozi wa umoja huu wa Wayahudi duniani ulikuwa na lengo la kuwaunganisha Wayahudi na kuanza harakati za kuwezesha Wayahudi kurudi katika nchi ya baba na mama zao (Homeland) ambako Wapalestina kwa wakati huo walikuwa tayari wanalikalia.
Walitaka kuwezesha kuundwa tena kwa Taifa la Israel kama lile lililokuwepo hapo kwanza mashariki ya kati kabla ya uvamizi wa WARUMI uliowaondoa katika ardhi yao.Hawakupendezwa na maisha ya mateso waliyokuwa wakiyapata ugenini.
Mahali walikokimbilia katika nchi zingine Wayahudi walipata tabu sana. Kutokana na vipaji vikubwa walivyobarikiwa vya akili,mafanikio na kuzaliana sana walionekana kuwa tishio katika nchi walizokuwa uhamishoni.
Chuki ya wenyeji wa nchi ambako walikimbilia ikazidi kuwa kubwa dhidi ya Wayahudi. Wayahudi wakazidi kupata shida kwa kuchukiwa na wenyeji waliowahifadhi
Kwa mfano kiongozi wa Ujerumani Adolf Hitler yasemekana aliwaua Wayahudi wapatao milioni sita kwa sumu,njaa na risasi akiwatuhumu kuwa waliisaliti Ujerumani kwa kuwasaidia adui katika vita ya kwanza ya dunia na ndiyo sabau Ujerumani ikashindwa vibaya Katika vita ile.
Baadhi yao aliwapeleka katika kambi za kijeshi za mateso na kuwafanyisha kazi ngumu. Pia inadaiwa kwa vile kulikuwa na wanasayansi wa kiyahudi ambao ni "GENIOUS" aliwalazimisha kuokoa maisha yao kwa kuwataka wabuni au wamtengenezee silaha nzuri za kisasa la sivyo watakufa.
Wakati mwingine aliwapanga mstari mmoja na kuwamiminia risasi. Njia nyingine ilikuwa ni kuwaingiza Katika chumba chenye gesi ya sumu na kuwafungia wafe kwa kulewa sumu.
Sababu ya Hitler kuwaua Wayahudi baada ya vita vya kwanza vya dunia haikuwa Wayahudi kusaliti Ujerumani bali ilikuwa ni hofu na chuki dhidi ya Wayahudi. Wajerumani waliamini wao ndiyo kizazi bora na kinachotakiwa kuitawala dunia na SIYO Wayahudi walioitwa taifa teule (lililoteuliwa na Mungu) Ndiyo maana waliamua kuwaangamiza ili kujihami dhidi ya washindani wao.
Wayahudi walionekana kuwa vizuri karibu kila sekta. Ilionesha wazi kuwa baadaye wangekuja kuwatawala wenyeji kwa namna moja au nyingine.
Wayahudi walipata tabu sana katika nchi za Urusi, Ufaransa na Ujerumani hadi kufikiria kurudi katika nchi ya baba zao kule Palestina. Lakini tatizo lilikuwa ni kwamba katika nchi ile kwa sasa kuna Wapalestina tayari wanaishi baada ya Warumi kuondoka na dola yao kuanguka. Sasa wayahudi watapaingia vipi?.
Wapalestina hawakuwa tayari kuona ardhi yao inawarudia tena Wayahudi.
Harakati za Wayahudi za kutaka kuwa na taifa lao tena zilipata uungwaji mkono na mataifa makubwa kama Uingereza na Marekani.
Baada ya mwaka 1919 ambapo Wapalestina walikuwa wapo chini ya utawala wa Uingereza kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa Wayahudi walianza kuingia kwa wingi nchini Palestina wakirejea kutoka maeneo mbalimbali walikokuwa wamekimbilia. Hii ni kwa sababu Uingereza ilikubaliana na kuwa Wayahudi wanapaswa kuondokana na mateso kwa kuundwa tena taifa lao pale walipokuwepo awali.
Kitendo hiki cha Wayahudi kuanza kuingia nchini Palestina kiliwaudhi sana Wapalestina na kuwapinga vikali Waingereza wakiwa kama watawala kwa kuruhusu Wayahudi kuingia kwa wingi. Wapalestina walitaka kuwa na taifa lao lililo huru na kwa ajili ya Waarabu pekee. Pia walitaka kusitishwa mara moja kuhamia kwa Wayahudi katika nchi hiyo.
Ilipofika mwaka 1922 Waingereza waliona hakuna haja kwamba Wayahudi waikomboe na waichukue nchi ya Palestina yote na kuunda tena taifa lao kama zamani, bali waliona ni vema wawaache wote waishi pamoja kwa amani. Walitaka wawabembeleze Wayahudi na Wapalestina waishi pamoja kwa amani, wakashindwa kuona tofauti kubwa za kidini walizokuwa nazo watu hao.Wakawaahidi Wapalestina waliokuwa wamekasirishwa kuwa hawatawaruhusu tena Wayahudi zaidi kuendelea kuhamia nchini humo. Lakini mpango wao huo wa kuishi wote pamoja ukafeli.
Mateso ya Chama Cha NAZI Cha Adolf Hitler kwa Wayahudi kulisababisha Wayahudi wengi kukimbia Ujerumani na kuwa wakimbizi. Wengi wa Wayahudi walikuwa wakikimbilia Katika eneo la nyumbani kwao kule Palestina. Hadi kufikia mwaka 1940 nusu ya watu katika eneo la Palestina likawa ni Wayahudi na nusu nyingine ni Wapalestina.
Mwaka 1937 tume moja ya nchini Uingereza ilikuja na mapendekezo kuwa Palestina igawanywe kuwa nchi mbili. Wayahudi upande mmoja na Wapalestina upande mwingine. Lakini Waarabu wa Palestina wakakataa kabisa wazo hilo
Waingereza walijaribu tena mwaka 1939 mpango wao wa kuligawa taifa la Palestina kuwa mataifa mawili wakiwaahidi Wapalestina kuwapa Uhuru wao na kujitawala baada ya miaka kumi. Na wakaamuru idadi ya Waisrael kuhamia nchini humo idhibitiwe na kuwa watu laki moja tu kwa mwaka (100,000). Kudhibiti au kupunguza idadi ya wahamiaji wa kiyahudi nchini Palestina safari hii hakukuwafurahisha Wayahudi nao wakakataa pendekezo hilo.
Vita vya pili vya dunia vilipotokea ndiyo vikafanya mambo kuwa mabaya zaidi.Vita hivi vilifanya kuwepo kwa mamia elfu ya watu kama wakimbizi waliokimbia utawala wa Hitler wa Ujerumani na hawajui pakwenda.
Mwaka 1945 Marekani ikaishinikiza Uingereza iwaruhusu wakimbizi 100,000 wa kiyahudi kuingia nchini Palestina. Na shinikizo hilo lilipewa nguvu zaidi na kiongozi wa Wayahudi "David Ben Gurion" lakini Uingereza ikakataa shinikizo hilo kwa kuogopa kuwaudhi Waarabu au Wapalestina.
Wayahudi wakiwa wamechoshwa na mateso ya Chama Cha NAZI Cha Hitler walikuwa tayari kupigana hadi lipatikane tena taifa lao. Walianza kufanya matendo ya kigaidi dhidi ya wote Waingereza na Waarabu. Moja ya tukio linalokumbukwa ni kulipuliwa kwa Hoteli ya "King David Hotel" mjini Jerusalem ambayo ndiyo ilitumika kama makao makuu ya serikali ya Uingereza. Watu 91 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waingereza walijibu kwa kuwakamata viongozi wa Wayahudi na kuzizuia meli kama ile iliyojulikana kama THE EXODUS iliyokuwa imebeba Wayahudi wakuja kuhamia Palestina, wakaiamuru irudi ilikotoka.
Waingereza wakiwa wamedhoofishwa na vita vya pili vya dunia waliona hawangeweza kuendelea kushughulikia Jambo hili la wakimbizi wa kiyahudi, Kiongozi wa Uingereza Ernest Bevin akaamua auombe Umoja wa Mataifa( UN) kulishughulikia tatizo hili.
Novemba mwaka 1947 Umoja wa Mataifa ulipiga kura kuigawa Palestina rasmi kuwa nchi mbili. Nusu ni kwa ajili ya Taifa huru la Wayahudi na nusu nyingine kwa ajili ya Taifa huru la Wapalestina. Mapema mwaka 1948 Uingereza iliamua kujitoa moja kwa moja huko kwenye koloni lake nchini Palestina na kuiachia UN ifanye kazi yake licha ya kuwa mapigano kati ya Wayahudi na Wapalestina yalikuwa yakiendelea.
Sababu ya mapigano yaliyokuwa yakiendelea kati ya Wayahudi na Wapalestina ni kuwa Wapalestina walikasirishwa na kitendo cha ardhi ile kugawana na Wayahudi waliolowea katika nchi zingine kwa miaka mingi.
Uingereza iliondoa vikosi vyake vyote kurudi nyumbani Uingereza. Japokuwa Kitendo hicho kililaumiwa na mataifa mengine yaliyotaka Uingereza isingali harakisha kuondoa majeshi yake nchini Palestina na kuhakikisha kuna amani na utulivu kabla ya kuondoka.
Waarabu au Wapalestina walikuwa wakiilaumu Uingereza kuwa ilikuwa inawapendelea Wayahudi kuliko Wapalestina. Pia waliilaumu vikali Marekani kwa kuunga mkono pendekezo la kuundwa kwa taifa la ISRAEL ndani ya Palestina.
Mnamo mwezi Mei 1948 Ben Gurion kiongozi wa Wayahudi wa wakati huo alitangaza rasmi uhuru wa taifa jipya la ISRAEL. Kwa maneno mengine umoja wa Mataifa UN ulianzisha rasmi taifa jingine ndani ya Palestina mwaka huo wa 1948.
Hata hivyo taifa hilo changa lilishambuliwa haraka sana mwaka huohuo na Egypt, Syria, Jordan, Iraq, na Lebanon. Mataifa yote haya yaliungana kuipiga Israel.
Wapalestina walikataa kulitambua rasmi Israel kama taifa. Na waliapa kuliharibu. Hadi leo hawaitambui Israel kama ni nchi iliyopo katika ramani ya duniani hii.
Tokea hapo kulikuwa na vita nyingi za muda mfupi fupi Kati ya Israel na Palestina pamoja na washirika wake wa kiarabu waliokuwa wamelizunguka taifa changa la Israel. Kwa mfano kulikuwa na vita (1948-49, 1956, 1967, 1973 n.k.) Miongoni mwa vita iliyopata umaarufu ni ile iliyojulikana kama "The Six Day War, 1967" vita ya siku sita. Ni vita nyingi sana zimepiganwa mpaka sasa kiasi kwamba eneo hilo la mashariki ya kati linajulikana kama ni moja ya maeneo hatarishi duniani. Katika vita zote hizo mashambulizi ya Wapalestina dhidi ya Wayahudi yalifeli na Israel ikaokoka na kuibuka mshindi kimuujiza na kwa namna isiyoelezeka.
Inawezekanaje taifa changa likachangiwa kwa kupigwa kila upande na nchi kubwa zinazoizunguka Kama Egypt, Iran, Iraq, Jordan, Syria, Lebanon, Kuwait, Saudi Arabia, na bado ikashinda vita hizo zote.
Mara baada ya Umoja wa Mataifa kuigawa nchi ya Palestina mwaka 1948 na kupatikana mataifa mawili, yaani la Wayahudi waliorejea kutoka Ulaya na la Wapalestina vita havijawahi kukoma. Ni kama wanakuwa na mapumziko ya miaka miwili mi tatu wanaliamsha tena.
Mgogoro wa mashariki ya kati unayagusa mataifa mengi makubwa ulimwenguni kutokana na umuhimu wa eneo lenyewe ikiwa ni pamoja na utajiri wa mafuta. Mataifa ya kimagharibi na yale ya kikomunisti yanajihusisha sana na eneo hili kutokana na unyeti wa eneo la mashariki ya kati.
Kuna habari zinazohitaji kuthibitishwa zinazodai kuwa mataifa haya mawili kila mmoja ana washirika wake wanaomsaidia kijeshi,fedha na silaha. Upande wa Israel inatajwa Marekani na Uingereza kuwa ndiyo washirika wakuu wa ISRAEL ukiondoa mataifa mengine ya kikristo. WAPALESTINA kwa upande wao inadaiwa wamekuwa wakipokea msaada wa kijeshi, fedha, na silaha kutoka nchi za kijamaa (communist powers) kama Urusi pamoja na mataifa ya kiarabu.
Wakati wa Kugawanywa kwa mataifa haya Wayahudi walipewa asilimia 55 ya ardhi na Wapalestina walipewa asilimia 45. Kabla ya hapo Palestina ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza ambao waliondoka na kuwaacha wajitawale.
Mji wa Jerusalem hakuna aliyepewa kati yao maana ulionekana kung'ang'aniwa vikali na kila upande. Badala yake ilipewa Jordan jirani yao iushikilie. Mji huo ulipiganiwa kutokana na kuaminika kuwa ni asili au chimbuko la dini tatu, Uislamu, Ukristo, na dini ya kiyahudi ya Judaism.
Eneo moja mjini Jerusalem ambapo unapatikana msikiti wa Al-Aqsa iliamuriwa kuwa litabakia kuwa mali ya jamii ya kimataifa, yaani mali ya watu wote wa dunia hii maana linagusa dini zao lakini litakuwa katika usimamizi wa UN(Umoja wa Mataifa) kuepusha mzozo.
Katika kila vita ambayo imekuwa ikipiganwa Israel imekuwa ikiteka maeneo zaidi na kuweka katika milki yake. Baadaye Israel iliteka mji wa Jerusalem kutoka kwa Jordan kutokana na kuwa Jordan iliungana na Palestina na mataifa mengine kama misri, Syria, Irani na Lebanon kuwapiga Wayahudi.Israel ikaufanya ndiyo makao makuu ya serikali yao. Imeendelea kufanya hivyo hadi kufikia kumiliki ardhi zaidi ya 78%. Inapoteka eneo fulani katika vita huidhinisha kujengwa kwa makazi kwa ajili ya walowezi wa kiyahudi jambo linalopingwa na mataifa mengi.
Israel inautaka mji wa Jerusalem kwa gharama yoyote kutokana na historia ya mji wao wa kale uliokuwepo hapo pamoja na HEKALU lililojengwa na mfalme Suleimani ambalo inasemekana lilijengwa ulipo msikiti wa Al-Aqsa kujumlisha na maeneo mengine mengi inayodai ni matakatifu na ya kihistoria.
Hadi hivi sasa ni nchi moja pekee duniani inayoutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya serikali ya Israel. Marekani peke yake ndiyo imehamishia ubalozi wake mjini Jerusalem chini ya utawala wa Trump.
Nchi zingine zote huweka balozi zao katika mji wa Tel Aviv. Nchi yoyote inayothubutu kuweka ubalozi wake au kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya serikali ya Israel inakuwa imetangaza vita na jamii ya kiarabu na hushambuliwa kwa matukio ya kigaidi.Na hii ni moja ya sababu nchi nyingi hawaweki balozi zao mjini Jerusalem.
Wakati Israel inauteka mji wa Jerusalem kulikuwa na Wapalestina ndani yake. Wapalestina wapatao 400,000 wanaishi Jerusalem. Wameambiwa wanayo haki ya kuishi lakini hawatambuliwi kama wananchi.
Wapalestina Waliopo nje ya mji wa Jerusalem huruhusiwa kwenda Jerusalem kwa masharti magumu. Mjini Jerusalem Israel ilijenga nyumba kwa ajili ya makazi ya Wayahudi zipatazo 200,000.
Waislamu wanalitaja eneo ulipo msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem kama ni eneo la tatu kwa Utakatifu duniani baada ya Mecca na Madina. Walikuwa wakilitumia eneo hilo la Al-Aqsa kwa ajili ya kibla(qibla) yaani walipokuwa wakiswali waligeukia au kutazama msikiti huo wa Al-Aqsa kabla hawaja hamishia kibla kwenda Mecca.
Wanaamini kuwa eneo hilo la msikiti wa Jerusalem ndilo eneo ambalo mtume Muhammad alipaa mbinguni.
Wayahudi wanaamini kuwa jengo hilo takatifu kwa mara ya kwanza lilikuwa ni Hekalu lao. Lakini sheria ya kiyahudi inakataza kuingia na kuabudu kwa kuwa ni eneo takatifu sana.
Ukuta uliopo magharibi mwa msikiti huo hujulikana na Wayahudi kama ukuta wa maombolezo. Unadaiwa kuwa ni ukuta uliosalia wa Hekalu lao la kale la mfalme wa Wayahudi Suleimani.Wayahudi huenda hapo kuomboleza na kujutia dhambi zao.
Lakini Waislamu wao huamini ukuta huo ni ukuta wa Al-Burqa. Eneo ambalo mtume Muhammad alifunga al-Burqa wakati alipopaa mbinguni ili kuongea na Mungu.
Mwaka 1967, Jordan na Israel zilikubaliana kuwa Waislamu wataruhusiwa kuabudu ndani ya msikiti wa Al-Aqsa pamoja na kuhakikisha ukarabati wake lakini usalama wa nje ya msikiti huo utadhibitiwa na Israel
Wasio Waislamu wataruhusiwa kutembelea eneo hilo la msikiti wa Al-Aqsa kwa saa kadhaa lakini hawatarusiwa kufanya ibada ndani yake
Lakini mashirika ya kupigania eneo hilo kuwa ni Hekalu ya kiyahudi, kama vile Hekalu la Mount Faithful na lile la Hekalu la Institute, wamekuwa wakishinikiza serikali ya Israel kuwaruhusu Wayahudi kuingia katika jumba hilo la msikiti na wanataka Hekalu la tatu kujengwa katika eneo hilo
Mwaka 2000 waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon alitembelea na kuingia katika msikiti wa Al-Aqsa akiwa na polisi 1000. Kitendo hicho kilisababisha ghasia iliyopelekea Wapalestina 3000 na Waisrael 1000 kuuawa
Wapalestina kutoka West Bank (nje ya Jerusalem) huwekewa vikwazo kwenda katika msikiti huo. Ni wale wenye umri wa zaidi ya 40 pekee ndiyo huruhusiwa kuutembelea msikiti huo wa Jerusalem siku ya ijumaa na wengine hadi kibali maalumu
Nchi hizi mbili husapotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kueneza propaganda za chuki dhidi ya mwenzake ulimwenguni na kutafuta kuonewa huruma kimataifa.
Kwa mfano, vita vinavyoendelea sasahivi ukifuatilia utagundua Wapalestina wamerusha makombora zaidi ya 1000 nchini Israel. Lakini ukiingia katika Account ya Facebook , Instagram au YouTube ya Al Jazeera hautakuta habari yoyote yenye kuonyesha au kuzungumzia mashambulizi ya Palestina nchini Israel, bali utakachokiona ni uhalibifu na mauaji yaliyofanywa na Israel pekee kana kwamba upande wa Palestina haufanyi lolote umekaa tulii unapigwa tu. Hapo ndipo utaanza kuelewa ninacho maanisha.
Media is a very powerful weapon. Na vyombo hivi vya habari vimefanikiwa kuuaminisha ulimwengu kile walichokitaka wao kiwe ndiyo ukweli badala ya ukweli halisi.
Chombo hiki cha habari kipo kwa ajili ya mataifa ya kiarabu. Huuonesha ulimwengu ubaya wa Israel ili watu wajenge chuki dhidi ya Israel na kuwahurumia Wapalestina.
Na vyombo vya habari vya kimagharibi navyo vimelaumiwa kupendelea upande wa Israel kuliko Palestina. Hiyo ndiyo habari kama ulikuwa hujui
Kugawanywa kwa nchi ya Palestina na umoja wa mataifa ambavyo hakuku uridhisha upande wowote. Pande zote mbili hazikuridhika na mgawo ule japokuwa kiongozi Wa wazayuni au Wayahudi (ZIONIST LEADER) alikubali kupokea walichokipata wakati Waarabu wa Palestina walikataa.
Waarabu wameishi katika ardhi ya Palestina kwa miaka zaidi ya 2,000 wakati huo wote Wayahudi wakiwa ughaibuni katika mataifa ya ulaya.
Na pia tukaona kuwa vita kati ya Israel na Palestina vilianza tu punde majeshi ya Waingereza yalipoondoka katika ardhi ya Palestina. Mwaka ule ule lilipoundwa taifa la Wayahudi.
Na tukaona jinsi David Ben Gurion waziri mkuu wa kwanza wa Israel alivyotangaza Uhuru wa taifa jipya la ISRAEL mwaka 1948.
Kutangazwa kwa taifa la kiyahudi kulikuwa na maana kwanza kuwa Wayahudi wangelikuwa huru dhidi ya mateso na taabu walizozipata huko katikati mataifa walikokuwa wakiishi.
Maana ya pili ya kutangazwa kwa taifa jipya kwa Wayahudi ilikuwa ni kutimia kwa unabii uliotolewa miaka mingi kuwa Wayahudi wangepata tena kujitawala wenyewe katika ardhi yao wenyewe. Hiyo ndiyo ilikuwa maana ya uhuru huo kwa mujibu wa Wayahudi.
Pia tuliona kuwa WARUMI walipowashinda Wayahudi katika vita na kuwakimbiza katika nchi yao walibadili jina la Israel na kuita jimbo lao hilo jipya waliloliteka "Palestina".
Pia tukaona sababu zilizowezesha au zilizosukuma kuundwa kwa taifa la ISRAEL ndani ya Palestina kuwa ni;
Mauaji ya Wayahudi Ujerumani na changamoto walizokuwa wakipata Wayahudi ughaibuni
Msaada wa Uingereza na Marekani
Kuundwa kwa umoja wa Wayahudi duniani (Zionism ideology) iliyowaunganisha Wayahudi duniani kote
Athari za vita vya kwanza na vya Pili vya dunia.
Anguko la uchumi wa dunia la mwa 1930s
Mkono wa Umoja wa mataifa
Na kazi kubwa aliyoifanya kiongozi wa Wayahudi Theodor Hertzl
n.k
Israel na Palestina wamepigana vita vingi sana tangu kuundwa kwa taifa la kiyahudi ndani ya Palestina.
Vita vilivyopiganwa hadi sasa ni takribani vita 20 hivi. Ninaandika hivi ili utumie muda wako kutafakari na kuziombea nchi hizi ikiwezekana Mungu aweze kuwapatia suluhu ya kudumu. Maisha yao yote yamekuwa ni taabu, dhiki na majeraha yasiyopona
Nitakwenda kutaja baadhi ya vita walivyopigana hapa bila kutoa maelezo mengi maana ni vita vingi sana kuweza kuelezea. Ninaandika hivi hapa moyoni ninaumia na nina uchungu na maumivu makali kutokana na kinachoendelea kwa binadamu wenzetu huko mashariki ya kati.
Vita hivyo ni kama vifuatavyo;
Vita ya kwanza vilivyo piganwa mnamo mwaka 1948 Vita vya uhuru. (War of Independence)
Hivi vilikuwa ni vita vya taifa jipya la Israel kuhusu kufa au kupona. Vilipiganwa mwaka huohuo wa kuanzishwa taifa hilo dhidi ya majirani zake walioungana wa mataifa ya kiarabu. Mataifa hayo ni Egypt, Syria, Jordan , Palestina na Lebanon
2. Retributions operations 1951-1955.
Hii ni operation iliyofanywa na Israel miaka ya 50s. Operation hii ilikuwa ni kujibu uvamizi wa mara kwa mara wa wanamgambo wa Palestina waliokuwa wakijipenyeza ndani ya Israel na kufanya mashambulizi ya kushitukiza kwa raia wa Israel na wanajeshi wakitokea upande wa Syria, Egypt, na Jordan
3.Suez Canal War on October 29th 1956.
Katika vita hii Israel ilivamia peninsula ya Sinai(Egypt)na kuzima upinzani haraka huku ikisonga mbele kuelekea mfereji wa Suez. Ufaransa na Uingereza zikajitokeza haraka kutaka kushikilia ukanda huo wa mfereji wa Suez ili kuyatenganisha majeshi ya Egypt na Israel kwa muda. Abdel Nasser kiongozi wa Egypt alikataa kitu hicho na oktoba 31 mwaka huo Ufaransa na Uingereza zikaivamia Egypt
4. Six-Day War 1967.
Pia vinajulikana kama vita vya Juni 1967 vya Israel na Waarabu. Vilipiganwa kati ya Israel na majirani zake ambao ni mataifa ya Egypt, Jordan na Syria. Na hivi ndo vita maarufu zaidi
5. War of Attrition 1967-1970.
Hivi ni vita vilivyopiganwa kati ya Israel na Egypt. Vilipoisha vita vya siku sita (six day war) hakukuwa na diplomasia nzuri yoyote iyokuwa imefikiwa kati yao hivyo vita nyingine ikatokea.
...6. Yom Kippur War October 1973
Vilikuwa ni vita vya muungano wa mataifa ya kiarabu yakiongozwa na Egypt na Syria dhidi ya Israel kama njia ya kuyarudisha maeneo ambayo Israel iliyateka katika vita vya Six day war. Mataifa hayo yalifanya mashambulizi ya kushtukiza kwa Waisrael katika siku takatifu ya Waisrael iitwayo Yom Kippur.
7. Palestinian Insurgency in South Lebanon.
Mataifa ya Palestina na Jordan yalivamia Israel kutokea kusini mwa Lebanon. Kutoka huko yalishambulia vikali mji wa Galilaya. Mashambulizi haya yalipelekea vita kamili vya 1982.
8.1982 June Lebanon War
Israel ilivamia kusini mwa Lebanon ili kuwafurusha au kuwatimua muungano wa Palestina na Jordan kutoka katika eneo lake. Serikali ya Israel ilitoa amri ya kuvamia kufuatia jaribio la kuuliwa kwa balozi wake wa nchini Uingereza bwana Shlomo Argov.
Pia ilivamia Kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara kutokea kaskazini mwa Israel kutoka kwa Wapalestina.
9. South Lebanon Conflict 1982-2000
Hivi vilikuwa ni vita vilivyodumu kwa takribani miaka 20 kati ya Israel na Waislamu (Hezbollah) wa Lebanon wakiongozwa na Iran.
10. First Intifada 1987-1993
Hii ni vita iliyoenea eneo kubwa sana kati ya Israel na Palestina katika maeneo ya WEST BANK na UKANDA WA GAZA.
11. Second Intifada 2000-2005
Hivi ni vita vya pili vya Intifada vilivyohusisha ghasia kubwa kati ya Israel na Palestina.
12. 2006 Lebanon War
Vita hivi vilianza kama operesheni ya kijeshi ikiwa ni matokeo ya kuuliwa kwa wanajeshi wawili wa akiba wa Israel na wanamgambo wa Hezbollah.
13. Gaza War 2008-2009
Haya yalikuwa ni mapigano ya wiki tatu kati ya Israel na Hamas wakati wa msimu wa baridi mwaka 2008. Israel ilijibu mashambulizi ya rocket yaliyotoka ukanda wa Gaza. Israel ilifanya mashambulizi ya angani kuzuia mashambulizi ya roketi kutoka Gaza na uingizwaji wa silaha Gaza. Israel ilifanya mashambulizi ikilenga wanajeshi, raia, vituo vya polisi na majengo ya serikali ya Palestina.
14. Gaza strip air raids 2011
Mauaji na mshambulio ya kulengwa yalifanywa na Israel kwa jeshi la muungano wa Palestina na nchi washirika za kiarabu (PRC). Hii ilikuwa ni kujibu mashambulizi yaliokuwa yanatokea kusini mwa Israel.
14. Operation returning echo- March 2012
Hii ilihusisha mfululizo wa mashambulizi ya rocket za Wapalestina dhidi ya Israel kufuatia kuuawa kwa kiongozi wa jeshi la muungano wa nchi za kiarabu na Israel.
15. Operation Pillar Defense -November, 2012
Hii ilitokana na mamia ya mashambulizi ya rocket za Hamas katika miji ya kusini mwa Israel. Israel ilijibu kwa kufanya operation Gaza kumlenga na kumuua Kiongozi wa Hamas Ahmed Jabar. Pia Israel ilifanya shambulio la anga na kuharibu mahandaki ya maficho ya silaha za Hamas za masafa marefu zenye uwezo wa kufika mji wake wa Tel Aviv yapatayo 20.
..................
Vita zilizopiganwa kati ya Israel na Palestina ni nyingi sana. Zingine hazikuwa vita kamili ila ni oparesheni fupi fupi za kijeshi walizokuwa wakifanyiana. Kipindi kijacho tutaangazia kwanza sababu za kutokea kwa vita hivi vilivyodumu kwa muda mrefu kabla ya kuendelea na vita na operesheni za kijeshi zilizobakia.
...Vita kati ya Israel na Palestina vina historia ndefu na vimedumu kwa zaidi ya miaka 70. Kila vita, kila kifo na kila kitendo cha kikatili wanachofanyiana huongeza chuki na uhasama zaidi kati yao.
Baadhi sababu zinazohusika kuendeleza mgogoro baina yao ni hizi;
Kuanzishwa kwa taifa la Israel ndani ya Palestina.
Kitendo hicho kilipingwa na wapalestina na kuamusha hasira kali iliyowafanya waape kuliharibu taifa hilo.
Tofauti za dini kati yao.
Wapalestina ni Waislamu wakati Waisrael ni Waumini wa dini ya kiyahudi (Judaism) na Wakristo (Christians). Tofauti hizi hufanya wasipikike chungu kimoja.
Ukosefu au upungufu wa ardhi.
Mataifa haya yanapigana kumiliki ardhi zaidi kuliko mwenzake. Mataifa haya yapo katika eneo dogo sana lisilotosheleza idadi wa wakazi na isitoshe sehemu kubwa ya ardhi ni jangwa.
Sera ya Israel ya kupanuka na kuteka ardhi zaidi ya Wapalestina. Katika vita vya Six Day War 1967 Israel ilichangiwa na mataifa ya Lebanon, Syria, Iraqi,Jordan, Egypt na Palestina. Katika vita hiyo Israel iliwapiga mataifa haya na kuteka maeneo yao kama Sinai desert (Egypt),Gaza strip (Palestina), Golan Heights (Syria), West Bank (Palestina), East Jerusalem (Jordan).
Kitendo hicho kilichochea hasira zaidi miongoni mwa mataifa hayo.
Kupigania kumiliki maeneo matakatifu. Maeneo mbalimbali yanayoaminika kuwa ni matakatifu yanagombaniwa vikali na Israel na Palestina. Ikiwa ni pamoja na eneo ulipo msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem ambapo inaaminika ndipo Hekalu la Kwanza ya mfalme Suleimani wa Wayahudi lilijengwa. Maeneo mengine ni kama eneo alipozaliwa Yesu Kristo na mengine mengi.
Chuki na matendo ya kigaidi kati yao.
Kila mmoja anamchukia mwenzake kwa dhati. Waisrael wanawaona Wapalestina kama watu wasio na demokrasia, masikini, wagomvi, na waumini wa dini yenye kuhamasisha chuki na ugaidi. Na Wapalestina wanawaona Waisrael kama wavamizi wa kikoloni ndani ya ardhi yao, watu wenye nia ya kutawala mashariki ya kati yote. Pia kuna chuki dhidi ya Wayahudi kutokana na Wayahudi kufanikiwa na huku waarabu wakifeli kama taifa. Israel pia anaonekana kuwa ni taifa linalotumiwa na nchi za magharibi kuwatawala Waarabu huko mashariki ya kati."
"Hali kwa sasa imekuwa mbaya zaidi na kamwe hutoweza kuizuia kwa nguvu wala kwa kukaa mezani."
"Huu ni mtego wa wakubwa nami na wewe tumetegwa katika wavu hivyo unamaamuzi ya kuchagua kufikia sasa"
Baada ya kuwa nimemsikiliza kwa muda mrefu hatimaye nilipaswa kufanya maamuzi sahihi maana nilijua nipo na mtu ambaye amekosa kutii amri ya jeshi.Ingawa sikuwa nimeyazalau mawazo yake ila nilijua nakwenda kupatwa na mambo makubwa zaidi.
Niliamua kumpa mpango maana bila hivyo tutaangamizana kwa itikadi bila kujali ubinadamu.
Mpango ambao ulikuwa ni hatari kwa wote alio kuwa wanafadhili yetu na kuifanya iwe ya uhasama na kuonekana watu wa ajabu duniani.
Maana tulipaswa sasa kuukata mzizi wa fitina kwa kuanzia kwenye chanzo.
"Kuna mtu tunapaswa kumuua, Hu
.MWISHO.
DHIKI KUU
Mpango unasukwa katika riwaya hii inayo fuata.
Hivyo hakikisha unakisoma kitabu hiki pia kujua yaliyo jiri kwa majasusi wawili walio paswa kuwa maadui.
Ni mpango ulio kwisha anakuwa vyema na waandaaji wanawasubiri wachezaji walicheza.
MANINJA WAWILI WAKIKUTANA NA MDUNGUJI KICHAA MUUJI ALIYE LIPWA KUWAUA HATA KAMA WAKIWA WAMEKUFA.
KIONJO
RIWAYA:DHIKI KUU
MWANDISHI:NELSON NTIMBA
MTUNZI#2BETA DAISOPIA
Tukio la siku hii lilikuwa tofauti na matukio ya mauaji aliyo kuwa ameyazoe kwenye macho yake.Ingawa kazi ya upelelezi haikuwa sehemu ya majukumu yake kwa wakati huo.Kazi pekee isiyo husisha kushika siraha wala damu,zaidi ya kushika kalamu na penseli na kupiga picha na kuchora mwenendo wa matukio ndiyo pekee ilikuwa imemuweka katika tukio hili lenye utata.
Kiukweli aliutambua ukweli wa ugumu wa kazi hiyo, mpelelezi aliye kuwa amepewa kazi hii alikuwa na mtihani wa kuwatambua wauaji hawa ambao kialisi hawakuwa wamefanya kosa lolote katika matukio haya.
Mtu wa kwanza kuondolewa uhai wake alikuwa ni waziri wa ulinzi. Waziri alikuwa amekufa kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwili wili chake.Lakini ilionekana kabla ya kuondolewa uhai wake alipitia mateso makali sana.Maana mwili wake ulionekana kubabuka ngozi.
Mtindo huo wa mateso hasa huwa maalum kwa ajiri ya kuwatesea majasusi ambao huwa wagumu kutoa siri.Ni mtindo mbaya sana ambao jamii za kimataifa na watu wa haki za binadam wanaulaani na kwa sasa hakuna shirika la usalama linautumia.Lakini nilishangaa kuona wauaji hawa wanautumia tena kwa raia ambaye sizani kama ana madhara kiasi hicho.
Mateso haya hasa hutumia sindano za maji ambayo yametiwa pilipili.Ambapo maji hayo uchomwa juu ya ngozi.Maji hayo ya pilipili uanza kufanya kazi mara tu yakisha ingia kwenye mwili.Ukiteswa kwa mtindo huo ni mara chache kutokua majibu wayatakayo maana huwa unasema kile unacho kuwa umeulizwa tu na su vinginevyo.
Hivyo ukisha achiwa ama hata ukifa kuna madhara makubwa ngozi yako itapata ikiwemo kuvimba ngozi na kuwa mwekundu.Hivyo mmwili wako huwa rahisi kuooza haraka sana hata uwe umehifadhiwa kwenye barafu haizui mwili kuoza.
Kifo chake kilikuwa cha ujumbe maalum ambao kialisi haukueleweka wazi wazi maana ulikuwa ni wa kifumbo na ulio kuwa na michoro ya kisanii.Lakini katika michoro hiyo kulikuwa kuna namba ambazo hazikutiliwa maanani sana ingawa nazani zilichukuliwa na kuhifadhiwa kwa ajiri ya matumizi ya baadae.
Tukio la pili lilikuwa la daktari ambaye aliufanyia vipimo mwili wa waziri.Huyu alidugwa sindano ya kemikali ambayo hatukuwa tumeijua ipoje lakini nayeye alionekana alipitia mateso kama ya waziri ingawa huyu ni kama alikufa kifo cha amani sana maana hakuwa ametoa macho wala hakuonyesha kama aliupigania uhai wake.Nikama mapigo yake ya moyo yalisimama ghafula.
Hawakuwa wameacha alama yeyote pia hata kimakosa isipo kuwa mchoro wao pamoja na namba za kifumbo ambazo pia zilionekana kama hazina maana yeyote ile kwa wakati huo.
Kifo hiki cha mtaalam wa michoro na alama za siri ambaye alikuwa ameacha kazi yake serikalini na kuamua kuwa mchora tatuu.Ndicho kiliweza kumfanya ahanze kutamani kujua kwanini watu hawa wanakufa vifo vya kufanana kwa kila kitu.Alitamani kuyafahamu maisha ya watu hawa walio kufa kiundani zaidi. Maana hapo ndipo wangeliweza kupata majibu ya mafumbo yao ambayo yalikuwa katika kamera yake Lakini hawakuwa tayari kuomba msaada.Ndiyo alitambua halikuwa jukumu lake kupeleleza kesi ambayo haikuwa maslahi wala madhara kwake maana msemo wa wahenga ulikuwa upo kichwani. Mchuma janga hula na wa kwao .Maana kwa wakati huwa hakuwa na cheo wala nguvu ya kuingilia yasiyo mhusu zaidi ya kufanya kazi yake pekee aliyo kuwa ameamua kuifanya kwa moyo mkunjufu.
Ni kweli maisha yake ya nyuma alikuwa ni mpelelezi ambaye alipoteza kumbukumbu ya ujuzi wake. Hakuna aliyejua nilikuwa nani hapo mwanzo maana nilipata kufahamu ni mimi miaka miwili iliyo pita nikiwa hospitali.Hata jina langu tu niliambiwa na nikafundishwa kazi ya kupiga picha na kuchora.Sikuwa namfamu yeyote zaidi ya askari wa kitengo cha upelelezi ambao walikuwa wananifuata kwenye nyumba ambayo niliambiwa ni mali yangu. Hadi nilipo pewa kazi ya siri nchini Urusi nikiwa kama mtaalam wa sheria na mpiga picha.
Ugojwa uliokuwa umempata kwa wakati huu haukuhitaji dawa ya hospitali.Ulikuwa umezidi uwezo wake wa kufikili,kwa maana kila jambo katika ofisi yake lilikuwa limevurugwa na kuchafuliwa kabisa.Hakufahamu nani alikuwa ameingia na kumuachia ujumbe wa ajabu katika muda ambao alikuwa ameimeipoteza familia yake katika mazingira ya kutisha.
Kazi yake ya kupiga picha na sheria aliona ndiyo mwanzo wa mkasa wake usio eleweka. Lakini bado alibaki na maswali yasiyo na majibu kwa wakati huo maana aliye kuwa anamfanyia mambo hayo alionekana anamfahamu vilivyo hata zaidi ya anavyo jifahamu.
Kila tukio na kila hatua aliyo ipiga kuwakaribia waliifuta na kumfanya aanze mwanzo ama anzie sifuri.Kwa maana hawakuacha hata tone la ushahidi wa kuweza kunisaidia kuwapata.
Ofisi yake inatazamana na majengo ya gereza la Mordvinia.
Upande wa kulia inanapakana na mgahawa wa Kiitaliano,ambamo humo ndimo huwa anapata chakula chake cha mchana ama kitinda mlo.
Jengo ambalo zipo ofisi zake ni jengo la ghorofa kumi na tano kwenda juu.Wenyeji wa Urusi upenda kuliita jengo lla biashara maana kuna maduka mengi ya urembo na bidhaa za nyumbani.Lakini jengo hili kialisi kwangu naona ni sehemu iliyo na misuko suko mingi maana ni jengo lililo jaa wageni toka nchi mbalimbali.Katika jengo hilo wengi wanao pangisha si wenyeji wa urusi maana maeneo mengi kuna sheria kali za kupangisha.
Kama raia wengine wa kigeni wasivyo penda kuvurugwa na maafisa uhamiaji wa Urusi wapangaji wengi walipendelea jengo hilo kwa sababu liliwapatia nafasi ya kufanya kazi zao kwa uhuru.
Maana kabla ya kuamia katika jengo hili Nickson Chabela alikuwa amefungua ofisi za mambo ya kisheria katika jiji la Mosco.Jiji hili lilikuwa ni sehemu nzuri ya biashara ya mambo ya kisheria.Maana raia wengi wa Urusi upenda kushinda katika kesi zao mahakani, kampuni aliyo kuwa anaisimamia ilikuwa na wanasheria makini wanao jua vizuri kazi yao.
Lakini wenye mamlaka baada ya kuona kuna mianya yao inazibwa waliamua kumfutia leseni yake na kumtaka achane na mambo ya sheria .Kwa wakati huo alikubali maana mkataba wake na waajiri walio mtuma ulimtaka awe mpole kama watu wa serikali watamtaka afanye hivyo na lazima kufuate maoni yao.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuwa kinyonga maana alipalipaswa kufanya kazi isiyo husika na kuikosoa serikali ya Urusi.Na kwa kuwa mji pekee ambao haukuwa na sheria kali ambamo watu toka nchi za kigeni walikuwa ni wengi ulikuwa ni Mordvinia.
Mlango wa ofisi ya Nickson Chabela ulifunguliwa kwa nguvu na mwanaume mwenye asili ya Kijerumani,Aliyekuwa na sura ya kikakamavu akiwa na kovu la kisu kwenye shavu lake,Ambalo inaonekana alilipata akiwa anautetea uhai wake.Mwanaume huyu hakuwa na sura ya tabasamu zaidi ya kuonyesha kuwa ana haraka sana na kazi iliyo mfanya awe hapo.
Mkono mwake alikuwa ameshikilia bahasha nyekundu yenye ukubwa wa A2. Hatua zake pana na kubwa zilimfikia Nickison na tayari alikuwa ameitua bahasha hiyo kwenye meza.Na alianza kugeuka bila kusema neno lolote lile.Alipo fika mlangoni aligeuka tena na kumpatia ishara ya kijasusi ambayo alikunja vidole viwili vya kati na kufanya alama ya kukata kama mkasi.
Kisha aliufungua mlango na kutokomea kusiko julikana na kumuacha Nickson akiwa na maswali yasiyo na majibu kumhusu mtu huyo wa ajabu.
_______Chumba Namba; 302______
Kitabu chenye rangi ya fedha kilikuwa mkononi mwa mwanaume ambaye uso
wake haukuwa ukionekana vema, kwani aliuficha kwa kuvaa maski
iliyouficha uso na kubakisha macho pekee. Kwa umbile alikuwa mwenye mwili
ulioshiba misuli iliyochipuka kwa kufanya mazoezi ya viungo yaliyo ya
kiwango kikubwa. Kwa hakika, alionekana kuzama katika msitu wa maandishi
ya kitabu alichokuwa anasoma. Wakati akiwa ndani ya chumba hicho
kilichoonekana kuwa cha kisasakilichosheheni nyenzo za kisasa na silaha,
nje ya chumba chake ulinzi uliendelea kuwa madhubuti. Kwa namna
alivyokuwa katilia umakini maandishi na michoro iliyondani ya kitabu, ni wazi
alikuwa kakusudia kutekeleza jambo la hatari.
Ukafika wakati mwanaume huyo akajikuta anaupekua ukurasa wa 302. Mkono
wake wa kushoto ukaambaa hadi kwenye mchoro ambao ulionakana kama
ramani ya jengo fulani lenye mfumo mgumu kulitambua. Hatimaye baada ya
dakika chache, mwanaume huyo alitingisha kichwa kukubaliana na hisia zake
kwa alichokiona na kukifikiri.
Wakati huo, upande wa pilichumba namba 304 alikuwepo Nickson Chabela,
alikuwa akifuatilia kwa kamera za video kila hatua aliyokuwa akiipiga
mwanaume ambaye hakuwa akitambulika. Hakuwa na muda wa kupepea
hata macho yake akitaka kujua kila kitu kilichokuwa kikirekodiwa na mashine
zake. Wakati akiwa makini kutaka kuiruhusu kamera yake isogeze ile ramani
na kuikuza ili aitume moja kwa moja katika makavazi ya utambuzi wa ramani,
katika idara ya usalama wa Taifa, Nickson alisikia mlio kama wa nzi arukapo,
nziiii, kisha umeme ulikatika pakawa na giza totoro. Wakati anahangaika
kutaka kuirejesha hali vema, umeme ulirudi. Akaikagua mashine yake na
kujikuta haina tena uwezo wa kumulika upande wa pili. Hata kamera yakeilipotengemaa, chumba cha mshukiwa kilikuwa kitupu, lakini akauona
mwanga mwekundu wa duara ukiwa umetua kifuani pake. Ni silaha ya
mdunguaji ilikuwa ikingoja kumtoa uhai..
Sasa afanyeje? Akichezeha mwili kweli ataishi?.
Kuutetea uhai wake kwa gharama yeyote ilikuwa ni lazima.Lakini hakujua adui yake alikuwa na uwezo gani wa akili maana kujikuta ndani ya shabaha ya mdunguaji ni kati ya hatari ambazo kamwe hakupenda kuwa nazo.Hakuwa na nyingine zaidi zaidi ya kutuliza akili yake na kusubilia mdunguaji afanye makosa ya kiufundi ili aweze kuwa huru.
Wakati akiwa anaendelea kuhesabu hatua na dakika zake za mwisho bila kufanya jitihada yeyote mlango wa chumba chake ulianza kutekenywa na funguo tokea nje ukionyesha kuna mtu asiye husika anahitaji kuingia ndani ya chumba yake.
Hakuna kitu alikuwa anakisubilia kama hicho kiweze kutokea maana kingelipunguza umakini kwa mdunguaji aliye nje ya jengo na kumpatia nafasi ya kujipanga upya.Kama alivyo kuwa amekusudia ndivyo mpango wake uliweza kuwa.
Wanaume wawili waliingia kwa kasi kama umeme ndani ya chumba cha Nickson Chabela ambaye tayari alikuwa amawasubilia kwa hamu.Kuingia kwao kwa kasi na kishindo ilikuwa ndiyo tiketi yake ya kumweka huru,toka kwa mdunguaji maana ni kama naye hakutegemea ujio huo.
Hakukuwa na wakuchaguliwa maana walipo ingia ni wakati huo huo huo mdunguaji alipo amua kuwadodosha lakini alokuwa kachelewa san.Wakati alipo tazama uingiaji wa wavamizi kwwnye chumba cha mteja wake Nikison aliweza kuhama na kujibanza nyuma ya kiti.
Hivyo walipo ungia wavamizi walisalimia na mdunguaji mwenye hasira.
Hivyo walijikuta wanadondoka kama kuku wa mdondo bila kutimiza wajibu wao wa kumtia nguvuni mtu wao.
Kazi ilikuwa bado maana mdunguaji baada ya kuwaangusha wavamizi aliendelea kusubilia windo lake liamke alipatie zawadi ya milele maana hakutakiwa kubaki yeyote mwenye kujua siri yao iliyo kuwa ikilidwa kwa akili nyingi na nguvu kubwa.
Hivyo Nickisoni kujua hata nukta ya mpango wao ilikuwa ni hatari kwa shirika lao,Laiti kama angelijua huja baada ya.
Hivyo shaka zote alizo kuwa nazo alizifukia katika akili ya usijali na kujivisha ujasili ambao hauachi asili abadani.
Hakujua kama alitakiwa kusafirishwa kwa haraka sana tena kwa gharama yoyote ile ili siri kubaki ikiwa siri.Lakini kama ilivyo mnyama awindwaye asivyo tambua mtego wake upoje naye hakutambua mtego wake umetegwaje.Huenda kuna jambo angelijisaidia mapema.
Hawakujua wanaye mtafuta ni nani laiti kama wangelijua, huenda wangebadilisha mpango wao na kutengeneza mbinu nyingine ya kukabiliana naye.
Lakini kwa sababu neno ningelijua huwa baadae awakulipa nafasi zaidi ya kutekeleza mpango wao.
Nickson jambo kuu alilokuwa akifahamu kwa wakati huo ni kufuatilia na kazi yake ilikuwa na hatari kiasi gani
.Lakini baada ya kuona yanayo mkumba alijua kumekucha sasa hivyo kujikomboa kutoka kwenye mikono ya mfungaji ilikuwa ni lazima na uharaka pekee ndiyo ungelimfanya zaidi kuwa hai na kutimiza jukumu lake muhimu ambalo lilikuwa tayari limewasafilisha baadhi ya rafiki zake walio kuwa wamemtangulia katika kufuatilia mpango ambao hadi kufikia sasa ulikuwa umepewa jina lisilo lasimi COD "0".
Ili aweze kujisaidia kutoka kwenye mikono ya mdunguaji kulikuwa na mambo mawili ambayo angeliweza kuyajaribu kwa wakati mmoja nayo hakujua kama kalata hizo zingeliweza kuzaa matunda maana ilikuwa sawa na
"Kuchezea shilingi pembeni ya shimo la choo"
Hivyo ili kujikomboa ilimpasa acheze mchezo wa shilingi katika shimo la choo kwa kuuchezea uhai wake ili aweze kuupata kikamili.
Taa iliyo kuwa ikitoa mwanga katika chumba alichokuwemo ilikuwa ni shilingi yake ambayo alipaswa kucheza nayo ili aweze kununua uhai wake.Hakujua atatumia gharama gani lakini akili tu ndiyo ingelimfanya apate nafasi ya kuendelea kuishi tena na alifurahi uhai wake.
Taa iliyo kuwa kwenye chumba chake ilikuwa imetengenezwa kwa glasi laini,hivyo lilikuwa ni tendo la dakika chache kupasua na kucheza na mwili na shabaha za mdungaji.Muda tu ndiyo aliugojea apate kufanya tukio la ajabu ambalo mdunguaji angelikuwa kumfahamu na kutambua mbinu zake alizokuwa amezifanya kwa kushitukiza.
Nickson aliandaa siraha yake ya kininja ambayo ni nyota.
Sirahaa hii hutumiwa na maninja walio daraja la kwanza hasa kwa ajiri ya mashambulizi ya kujihami na huwa haikosi shabaha kamwe.
Kwa mtindo wake wa nyota ulivyo huwa ina makali pande zote. Lengo la kuiwekea makali na pembe kali katika sehemu zote ni kwa ajiri ya kuifanya iweze kunasa windo hata kama lipo katika sehemu yenye uficho.
Ninja wenye shabaha nzuri wana uwezo wa kurusha siraha za nyota kuanzia tano na wasikose shabaha ya karibu,Lakini kama ninja anahitaji shabaha nzuri zaidi mara nyingi hutumia nyota moja moja kwa nusu sekunde kabla ya kurusha nyingine.
Na jambo la kwanza kabisa kabla ya kuweza kushambulia ninja anahakikisha shabaha yake ipo sahii na windo lake lipo katika hali ya utulivu,ama kama lipo katika mjongeo anapaswa kutumia pumzi yake na mapigo ya moyo kutabili litakuwa limehama kwa nchi ngapi.
Maana hapaswi kupoteza shabaha yake ya kwanza akiwa kwenye maficho ama katika hatari.Nyota ndiyo huwa siraha nyepesi zaidi ya kisu na zinabebeka hata katika mazingira yenye ulinzi mkali maana zinafichika kwa wepesi zaidi kuliko visu.
Hivyo alifahamu kuna wavamizi watafika ndani ya dakika moja zijazo.Hivyo mtu aliye kuwa anampatia wasi wasi ni mdunguaji maana hakufahamu ana uwezo gani hasa.
Maana katika sanaa ya siraha za wadunguaji kuna wadunguaji wa aina nne hatari ambao si rahisi kuwakwepa hata muwe katika hali gani.Mdunguaji hatari kuliko wote ni mdunguaji ambaye huwa katika daraja la kwanza ambaye huitwa doble monster.
Huyu ana uwezo wa kuachia risasi tatu katika ubora ule ule kwa kasi ya sekunde tatu toka kwa shabaha moja hadi nyingineHata kama hana siraha bora ya mdunguaji ana kasi ile ile na ni mwepesi pia hata kama akigundua yupo kwenye hatari anawea kufanya tukio na kulifanikisha kwa weredi.
Uwezo wake unatokana na kuweza kutumia mikono yao na macho yao yote kwa usahii.Anaweza kutumia mkono wa kusshoto na kulia kwa usawa sasa na macho yake yote yapo hivyo.Hili kwa Nickson hakuwa na shaka nalo aliamua kutumia mbinu yake dhaifu kwa mpinzani.Lakini kwake ni mbinu ya hatari kutumia silaha ya bomu la moshi ambayo ninja akiipiga chini utoka spidi kali kama kwamba ametoweka.Lakini kialisi huwa hajatoweka kama upepo bali kasi yake ndiyo humfanya ionekane ametoweka.Mlango ulikuwa upo wazi ndani ya sekunde hiyo.
Mdunguaji hakujua la kufanya baada ya kuwa amelikosa windo lake.Alifahamu kama ameshindwa kumpata kwa wakati huo ilikuwa ni zamu yake kuwidwa na Ninja aliye ponea chupu chupu.Hivyo aliibeba siraha yake haraka na kuiharibu ili asiache ushaidi eneo la tukio na makasha ya risasi hakuyaacha eneo hilo.
Baada ya kuwa amemaliza kuifuta ushahidi wote alishuka akiwa mikono mitupu hadi jengo la chini.
Ambapo alifahamu anaweza kuwa yupo ninja ambaye alikuwa amemkosakosa.Kwa kuwa alikuwa mikono mitupu akijihami vilivyo kama mtu asiye hatari na mtu.
Kiu ya kuua ilikuwa imejaa vilivyo na alipaswa kuua kwa lazima maana windo lilikuwa limeanza kukimbia .. ........
USIKOSE KUISOMA RIWAYA HII.
*******DHIKI KUU*******
Post a Comment