MFANYAKAZI lazima awe Mwanachama – Simon Patrick
KAIMU Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga SC, Simon Patrick ametoa ufafanuzi na kuwajibu wanaohoji kwa nini Yanga imeweka ulazima wa anayetaka kuwa mfanyakazi wa Yanga kuwa Mwanachama.
Simon amesema hitaji hilo liko ndani ya Katiba ya Yanga, Katiba ambayo ilitungwa mara ya kwanza ya Wazee wa klabu hii kongwe zaidi nchini.
Simon ameeleza kushangazwa na baadhi ya wanahabari kuingia katika mkumbo wa kuhoji masuala ambayo wangeweza kupata majibu yao kama wangesoma Katiba ya Yanga.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Simon Patrick amesema kuwa; Nimesikia kuna Wachambuzi wanalalamikia kigezo cha Uanachama kwenye ajira za Yanga, wengine wameenda mbali na kusema kipengele hicho kimewekwa kwa nia ya kunufaisha kikundi cha watu, naomba niwajuze yafuatayo;
Kigezo cha Uanachama hakijawekwa leo au jana, kiliwekwa na wazee wetu wenye akili kubwa ambao ndio waanzilishi wa hii Yanga ambayo vijana wa kisasa kwa kibri cha followers wa instagram wanaona wana haki ya kuidhihaki.
Katiba ya kwanza baada ya uhuru wa Tanzania ya mwaka 1968 ibara ya 5 iliainisha kigezo cha Uanachama kwenye Ajira za Yanga, ikaenda mbali na kusema lazima awe na sifa za Uongozi za Azimio la Arusha.
Kwa wale wenye taaluma ya Elimu za katiba, kuna kitu kinaitwa “Grundnorm”, hii inamaana kila katiba ina misingi yake ambayo hata ukibadilisha Katiba misingi hiyo haiguswi, mfano rangi ya Klabu, Nembo ya Klabu, kigezo cha Uanachama, slogan ya Klabu na itikadi za Mwanachama.
Mabadiliko yote 13 ambayo yamefanyika kwenye katiba ya Yanga hayajawahi kugusa hayo maeneo sababu ndiyo grundnorm ya katiba ya Yanga.
Katiba ya 2010 ambayo ndiyo imebadilishwa juzi, ibara ya 37 iliweka kigezo cha Uanachama kwenye Ajira za Yanga, kitu ambacho hakijabadilishwa kwenye katiba ya sasa.
Inasikitisha kuona mtu unajiita mchambuzi au mwandishi huku huwezi ata kufanya research ndogo kama hii, nchi ngumu sana hii.
Uandishi wa habari ni taaluma inayoheshimiwa Duniani, ila huku Tanzania ni ya masela wenye followers wengi kwenye mitandao ya kijamii.
Ndugu zangu WanaYanga, Yanga ni ya Wanayanga sio ya kila mtu, fursa za ajira ni za Wanachama wa Yanga tu.
The post MFANYAKAZI lazima awe Mwanachama – Simon Patrick appeared first on Nijuze Mpya -| Pata Habari zote za Michezo kitaifa na Kimataifa, Tetesi na Usajili, Magazeti ya Michezo, Ratiba na Matokeo, Mahusiano Pamoja na Nafasi za Kazi.
Post a Comment