MDHAMINI mpya aiingizia hasara Vunjabei, ni sababu ya jezi kuchelewa

MDHAMINI mpya aiingizia hasara Vunjabei ni sababu ya jezi kuchelewa

MDHAMINI mpya aiingizia hasara Vunjabei ni sababu ya jezi kuchelewaKAMPUNI ya Vunjabei Group ambayo ina mkataba wa kutengeneza na kusambaza jezi za timu ya Simba SC, imesema kuwa imeingia hasara ya dola 150,000 (zaidi ya shilingi milioni 340) kutokana na kubadilisha mfumo wa jezi za awali.

Mkurugenzi wa Vunjabei Group, Fred Fabian maarufu Fred Vunjabei amesema, hasara hiyo imetokana na kubadilisha mfumo wa jezi za awali baada ya kubadilishwa kwa mdhamini kutoka SportPesa na kuwa M-Bet.

Amesema, mkataba mpya ulipokuja alikuwa ameshabuni jezi za mdhamini wa awali, hivyo kumtia hasara ya kiasi hicho cha fedha za kuweka mdhamini mpya.

“Simba waliponipigia simu kuniambia juu ya kusitisha uzalishaji wa jezi kutokana na mkataba mpya basi ikanibidi na mimi nipige simu zoezi lisitishwe jambo ambalo limefanya jezi zichelewe.

“Mkataba na mdhamini wa sasa ulikuwa mzuri na ndio maana tuliamua kutulia ili kuzungumza na kuweka mambo sawa, kwa kuwa zile ni pesa za Wanasimba, kitendo cha kukurupuka kisa mkataba una pesa ndefu halafu mkaharibu sio sawa,”amesema.

Pia Fred Vunjabei amesema, athari ya kuchelewa kwa jezi ni kitendo cha Wanasimba kukwazika, lakini hakuwa na namna aliona ni bora kuchelewa kuvaa jezi halafu mkataba ukawa mzuri.

“Hata mimi niliumia jezi kuchelewa, usafirishaji umekuwa shida kubwa kutokana na mambo mengi kwa sasa, lakini kuanzia Jumatatu jezi zitakuwa zimefika na meli,”amesema.

Wakati huo huo, Fred Vinjabei amesema, mkataba wa jezi za Simba umemfanya jina lake kuzidi kuwa kubwa hivyo hata kitendo cha kupata hasara hiyo ya matayarisho ya awali hakuona shida na aliamua kukaa kimya.

MDHAMINI mpya aiingizia hasara Vunjabei ni sababu ya jezi kuchelewaMwaka jana, uongozi wa Simba SC uliingia mkataba na Kampuni ya Vunjabei Group wa kutengeneza na kusambaza jezi za timu ya wakubwa, wanawake na vijana wenye thamani ya shilingi bilioni mbili.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez alisema kampuni 11 ziliomba tenda hiyo, lakini Vunjabei Grouop alitimiza vigezo vilivyowekwa ndiyo maana walisaini mkataba huo.

Alisema, licha ya kutengeneza jezi, kampuni ya Vunjabei Group pia watatengeza vifaa kama barakoa, makasha ya simu, mabegi, miwani na kofia ambazo zitakuwa na nembo za klabu ya Simba.

“Tunategemea mkataba wetu utakwenda sawa na makubaliano, kwani tunaamini Vunjabei Group ni kampuni kubwa iliyobobea katika uuzaji nguo,”alisema Barbara.

Naye Mkurugenzi wa Vunjabei Group, Fred Fabian aliushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kufuata weledi katika tenda na kutoa haki kwa mshindi kufuatia kushindanishwa na makampuni makubwa.

Fred aliongeza kuwa, anaamini atapata faida kubwa kutokana na chapa iliyopo Simba ambapo alikiri ni mkataba mkubwa waliosaini tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo.

“Naushukuru uongozi wa Klabu ya Simba kwa kutuamini na kutupa nafasi hii, sisi ni kampuni ndogo na tumeshindana na kampuni kubwa kutoka nje ya nchi, lakini nafasi imetuangukia sisi kutokana na klabu kufuata weledi.

“Katika usambazaji wetu, tutakuwa na duka na gari maalumu kwa ajili ya kuuza jezi na tutatembea kila sehemu ambayo timu itakuwepo kikubwa ni kuhakikisha kila Mwanasimba anapata jezi halisi ya Simba,” alisema Fred Vunjabei mwaka jana wakati akiingia kandarasi hiyo.

The post MDHAMINI mpya aiingizia hasara Vunjabei, ni sababu ya jezi kuchelewa appeared first on Nijuze Mpya -| Pata Habari zote za Michezo kitaifa na Kimataifa, Tetesi na Usajili, Magazeti ya Michezo, Ratiba na Matokeo, Mahusiano Pamoja na Nafasi za Kazi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post