Bosi wa WCB Diamond Platnumz amefufua upya hisia kuwa yupo kwenye mahusiano na msanii wake Zuchu.
Hii ni baada yake kujitambulisha hadharani kuwa yeye ni mume wa malkia huyo wa Bongo kutoka Zanzibar.
Jambo hili lilitokea kwenye mtandao wa Instagram ambapo alikuwa anacomment kuhusu video inayomuonyesha akitumbuiza mashabiki wake nchini Ureno. Video hiyo ilipakiwa kwenye ukurasa rasmi wa WCB.
"ALIZALIWA ILI KUBURUDIKISHA DUNIA 🌍🌎🌎 PICHA YA KARIBU YA SIMBA 🦁 MFALME MR ELECTRICITY JUKWAANI 🙌🙌🙌. Matumbuizo ya @diamondplatnumz Moja kwa moja Katika @afronation huko Ureno," Maelezo ya WCB chini ya video hiyo yalisoma.
Katika video hiyo Diamond alionekana akifanya sarakasi mbalimbali jukwaani huku wimbo wake 'Number One' ukicheza.
Yeye ni miongoni mwa mamia ya wanamitandao waliojumuika kwenye ukurasa wa WCB kuangusha comment kwenye video hiyo.
"Huyo ni mume wa Zuuh," Aliandika.
Wanamitandao kadhaa ambao waligundua tukio hawakusita kutoa hisia zao. Hizi hapa baadhi ya jumbe:-
this_nachu Diamond Platinumz, wee Zuu yupi tena
wiskibabu @officialzuchu simba kathibitisha uku 🙌
zohabeni Kwani Zuuh huyu ni Yule Chuchu au mi ndo nachanganya mambo?😍❤️❤️❤️😍😍😍🔥🔥🔥🔥
officialpaula umeanza tena Kiki zako za ajabu ajabu heee
_cartoon47 sasa ndio unakosea naomba mzalishe kwa harake nikalee nae mtoto bro maana unaniweka sana
Zuuh ni jina la utani la Zuchu.
Kwa kipindi kirefu mwaka huu, yeye na Diamond wamedaiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Wawili hao hata hivyo hawajawahi kujitokeza kukiri waziwazi kuwa wanachumbiana. Hapo awali waliwahi kukana madai ya mahusiano huku Zuchu akiweka wazi kuwa Diamond ni bosi wake tu.
Staa huyo wa muziki kutokea Zanzibar alisisitiza kwamba kwa sasa tayari ako kwenye mahusiano na mwanamume mwingine ambaye ni mfanyibiashara.
Mwezi Februari malkia huyo wa Bongo alidai kwamba yupo kwenye mahusiano na mwanaume mwingine ila sio Diamond.
"Mimi sikai kwa Diamond. Kwa kweli nachumbiana na mtu, niko na boyfriend. Ni mtu tu wa kawaida. Ni mrefu kuliko mimi, ni maji ya kunde, ni mfanyibiashara na anafanya mazoezi. Siwezi kuwa na mtu ambaye hafanyi mazoezi, afya ni kila kitu" Zuchu alisema katika mahojiano na Wasafi Media.
Mwezi huohuo Diamond pia alithibitisha kuwa yeye ni bosi tu kwa Zuchu. Hata hivyo wawili hao wameendelea kufanya mambo mbalimbali pamoja ambayo yamezua shaka kubwa kwenye uhusiano wao halisi
Post a Comment