Kaka mmoja ambaye ni shoga anayefahamika kwa jina la Emmanuel, ameuawa baada ya kukutwa akijisaidia ktk choo cha wanaume.
Tukio hilo limetokea katika baa 1 Nchini South Africa, ambapo shoga huyo alikuwa akinywa pombe hapo, baada ya kubanwa na haja akaelekea chooni kujisaidia ambapo kinatumiwa na wanaume.
Ndipo akaingia mtu mwingine hapo chooni na kumkuta huyo shoga, akamuuliza anatafuta nini katika choo cha wanaume, shoga huyo wakati akiwa anatoa majibu, ndipo huyo mtu akaanza kumchoma na kisu tumboni, hali iliyopelekea damu nyingi kuvuja, na umauti umemkuta njiani akipelekwa hospitali.
Wakati tukio hilo linatokea kuna baadhi ya watu walikuwa wanashuhudia ila hawakutoa msaada wowote, hadi pale hali ilipokuwa tofauti.
Baadhi ya raia wa South Africa wametuma pole na salamu za rambirambi kwa familia ya Emmanuel, na wamelaani vikali kitendo hicho kwani sio cha kiungwana na sio cha kufurahisha, na ni jambo la kukemewa. Pia mtu aliyefanya mauaji hayo hajulikani alipo, japo hakuna hatua yeyote ya sheria iliyochukuliwa dhidi yake.
Ila jamani Waafrica mashoga wamewakosea nn lakini? Mbona mnawaandama sana? Kwani mkiwaacha wao wakaishi maisha waliyochagua mnapungukiwa nn? Kutwa kuwapiga, kuwaua, kuwabagua, kuwanyanyapaa, kuwatenga, hamuoni tabu? Hamjisikii vibaya? Hamuogopi? Inasikitisha mnoo. Ifike hatua kila mtu aishi maisha yake aliyochagua na sio kupangiana. Khaaah.
Pi na hawa baadhi ya mashoga wa ki Africa nao wanajisahau sana, wanajua wazi kwamba ktk bara letu nchi karibu zote hawatakiwi na bado haijawa rasmi utambulisho wao, lakini kutwa kujifaragua na kujishaua mbele ya jamii, ili tyuuh waonekane na wao wapo, ndo wanaishia kukutwa na haya masaibu, mtu unajijua n mlevi kwann usinunue Pombe zako ukakaa kwako ukanywa? Tena kwa uhuru kabisaaa, huko bar wanatafuta nn? Haya wengine km hapa kwetu Bongo wao ni shughuri na parties hadi wanakamatwa wanapigwa wee na kudhalilishwaaa, shida yote ya nn? Kwan usitulizane na maisha ya upekee kwani lazima kuchangamana na watu, si una balance tyuuh shoboo zako. Mara wengine kujitongozesha kwa wanaume straight, yaan ni tafrani tupu. Inauma.
Kwa tukio hili, nategemea kuona shirika la haki za binadamu hasa kutoka UN litoe tamko na lichukue hatua stahiki kulingana na husika, pia sheria ichukue mkondo wake ilk kukomesha tabia mbovu ya unyanyasi na ukatili dhidi ya mashoga.
Kila binadamu ana uhuru wa kuishi vile atakavyo ili hali asivunje kanuni, taratibu na sheria za nchi.
Post a Comment