Paula Kajala Amkana Harmonize kuwa 'Baba' na Kupakia Picha ya Babake Halisi




Baada ya Harmonize kumvisha pete ya uchumbe mpenziwe Fridah Kajala Masanja ambey inafahamika wazi kwamba alikuwa mke wa mtu tena kwenye ndoa halali kabisa, msanii huyo hakuishia hapo bali aliingia kwenye Instagram yake na kubadilisha pia maelezo ya bio ambapo aliandika kwamba yeye rasmi ni mume wa mtu na pia kwamba yeye ni baba.

Mabadiliko hayo kwenye bio ya mkurugenzi huyo wa Konde Music Worldwide yaliyafsiriwa kwa njia tofauti tofauti na baadhi ya watu haswa kipengee hicho alichokisema kwamba yeye ni baba.


Baadhi walihisi kwamba kwa kusema yeye ni baba basi alimaanisha kabisa kuwa ni babake bintiye Kajala, Paula ambaye ni mpenzi wa Rayvanny japo kuna uvumi kuwa wameshatenana tayari.

Wengine walimtetea Harmonize na kusema kwamba kauli yake kuwa baba ni sawa kwani huenda alimaanisha kuwa baba wa bintiye na yule mwanadada Muitaliano, Sarah ambaye walitengana miaka michache iliyopita.

Lakini gumzo hilo la baadhi kusema kwamba huenda aliridhia kuwa baba wa kambo wa Paula ni kama lilipokelewa kwa njia hasi na binti huyo wa Kajala ambapo Jumanne Paula alielekea kwenye Instagram yake na kubadilisha picha yake ya utambulisho kwa kuweka picha ya zamani akiwa mtoto, picha ya pamoja wakiwa na mamake Kajala pamoja na babake wa kumzaa bwana P. Fank Majani.


Kama bado haitoshi, Paula alipakia picha hiyo na kuifuatisha kwa maneno kwamba hiyo ndio familia yake halisi, yaani mamake Kajala na babake Majani – kuashiria kwamba katu hawezi kumtambua Harmonize kama baba, wa kambo au wa kupanga.

Pili ni kwamba Harmonize sasa atakuwa rasmi babamkwe wa msanii Rayvanny ambaye anachumbiana na bintiye Kajala kwa jina Paula, japokuwa pametokea uvumi kwamba Rayvanny na Paula hawapo tena pamoja kimahusiano.

Tatu ni kwamba Harmonize anamuoa Kajala ambaye inafahamika wazi kuwa ni mke wa mtu – na mtu huyo kwa wakati mmoja akiwa mmoja wa majaji waliokuwa wakitalii vipaji vya wasanii chipukizi, Harmonize akiwa mmoja wao na jaji huyo kipindi hicho mumewe Kajala alimtema nje Harmonize kwa kigezo kwamba msaniihana uwezo wa kuimba.

“Familia yangu, Kajala na Majani,” aliandika Paula kwenye picha hiyo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post