FACT-Mwenyezi MUNGU anayotabia ya kuwatumia wale watu ambao wamekataliwa. MUNGU anayo tabia ya kuwabariki wale watu ambao wamedharauliwa, kuumizwa na kufedheheshwa.
MUNGU anayotabia ya kuwainua, kuwapa hadhi na kuwaheshimisha wale walioumizwa vibaya.
Hufanya hivyo makusudi kabisa, ili tu, pale utakapofanikiwa, asiinuke mtu awaye yote na kusema kwamba, bila yeye wewe usingekuwepo hapo ulipo.
Mwenyezi MUNGU atakubariki ule wakati ambapo hakuna hata mmoja anaesimama na wewe kukusaidia. Ili tu, pale utakapofanikiwa mtu awaye yote asiinuke na kusema mimi nilikusaidia mpaka kufanikiwa.
Endapo mtu ataanzisha vita na wewe, endapo mtu atakuumiza, kukufedhehesha na kushushia heshima, hebu furahi maana hiyo ni dalili tosha kwamba, MUNGU ameamua kukubariki.
Sijui ni yepi unayoyapitia, ila elewa kwamba, kwa yote yanayokuumiza muda huu hebu kuwa na furaha, wala usioneshe huzuni. Usiwape ushindi wa mezani. Kilima uzuri mbali, karibu kina majuto.
You are a candidate for God's next blessing!
Post a Comment