BAADA ya kumalizana na Moses Phiri kutoka Zanaco ya Zambia ikimpa mkataba wa kuitumikia Simba, mabosi wa timu hiyo hawajalala kwani wamenasa mashine nyingine mpya kwa ajili ya msimu ujao.
Usiku wa Jumamosi mabosi hao walipambana na kufanikiwa kunasa saini ya Habib Kyombo kutokea Mbeya Kwanza aliyojiunga nayo dirisha dogo la usajili akitokea TS Sporting ya Afrika Kusini.
Mwanaspoti lilielezwa baada ya mvutano wa muda mrefu kwenye kikao cha kukubaliana masuala ya kimaslahi Kyombo akiwa na wasimamizi wake pamoja na viongozi wa Simba mwisho wa siku walikubaliana.
Inaelezwa baada ya mvutano huo Kyombo alikubali kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba msimu ujao na sasa atarudi Mbeya Kwanza kumalizia tu michezo iliyobaki Ligi Kuu.
Simba imevutiwa na Kyombo kutokana na uwezo aliouonyesha kwenye ligi amecheza mechi chache ndani ya mkopo wa miezi sita, ila hadi sasa amefunga mabao matano ambayo ni muhimu na kati ya hayo kuna yaliyoipa pointi pamoja na kutoa pasi ya mwisho moja. Simba imedhamiria kuboresha kikosi ili kurudisha makali waliyoyakosa msimu huu ndio maana iliposhindwa kukubaliana kumlipa Kyombo maslahi
Post a Comment