Dada wa kazi anadaiwa kumuua Mtoto Erickson Kimaro (8) kwa kumnyonga. Tukio hilo limetokea Mei 30, 2022 eneo la Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku mbili tangu aanze kazi na Waajiri walikuwa hawajamfahamu vizuri.
Imeelezwa kuwa, baada ya kufanya ukatili huo Mtuhumiwa alimpigia simu Mama kumjulisha Mtoto anaumwa na hapumui vizuri. Kichwa chake kilikuwa cha baridi na sehemu nyingine za mwili bado zilikuwa za moto. Ilithibitika ameshafariki dunia baada ya kukimbizwa Hospitali ya Mloganzila.
Kamera (CCTV) ambayo hakujua ipo nyumbani hapo ilinasa tukio hilo na Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi.
Post a Comment