UHAMISHO wa Gabriel Jesus kutokea Man City kwenda Arsenal ulitarajiwa kutangazwa muda wowote kuanzia jana jioni baada ya jana asubuhi kutua jijini London kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya.
Mara baada ya kutua katika viwanja vya mazoezi vya Arsenal, Jesus alipokelewa na Mbrazili mwenzake, Edu ambaye alikumbatiana naye kabla ya kukamilisha uhamisho huo wa pauni milioni 45.
Tayari Arsenal na Man City zimeshakubaliana kila kitu, huku pia Mbrazili huyo, 25, akiwa ameshakubaliana vipengele binafsi na Arsenal na hatua ya mwisho ilikuwa ni vipimo vya afya kabla ya dili hilo kutangazwa.
Jesus, 25, ameamua kuachana na City ili akapate nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza Emirates. Atasaini mkataba wa miaka mitano. Atakuwa usajili wa nne wa kipindi hiki cha usajili akiwafuata straika kinda Marquinhos, kiungo mchezeshaji Fabio Vieira na kipa Matt Turner.
Jesus aliyefunga mabao 95 katika mechi 236 za Man City, atawania namba na Eddie Nketiah.
KOCHA WA VIWANGO ATUA SIMBA, ALIFUNDISHA WYDAD CASABLANCA, MORSON ARUDI KUAGA SIMBA…
The post Jesus Atua Arsenal, Afanya Vipimo Akitokea Man City, Mashabiki Wapiga Shangwe! appeared first on Global Publishers.
Post a Comment