Jamaa Aliyening'inia Kwenye Helikopta ya Waziri Munya Anaswa "Atakabiliana na Sheria"


Mwanaume mmoja aliyening'inia kwenye helikopta iliyokuwa ikimsafirisha Waziri wa Kilimo Peter Munya eneo la Igembe Kusini, katika kaunti ya Meru nchini Kenya mapema jana, ametiwa mbaroni.


Tukio hilo lilitokea katika soko la Kiegoi baada ya Waziri huyo kufanikiwa kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja huo, hapo ndipo Mwanaume huyo aliponing'inia kwenye helikopta hiyo wakati ikijiandaa kupaa.


Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya (KCAA) katika taarifa ya hii leo, ilisema kwamba Mwanaume huyo amekamatwa na kwamba taratibu za sheria zitafuata.


Aidha KCAA ilitoa onyo na kukemea vitendo ambavyo vinaonekana kupata umaarufu katika mikutano ya hadhara, ikionya kuwa Watu watakaopatikana karibu na helikopta na kudandia chombo hicho cha anga, watakabiliwa na mkono wa sheria.


KCAA ilisema kuwa ni wajibu wa wahudumu wa vyombo vya anga kuhakikisha kwamba wanazingatia miongozo iliyopendekezwa katika ya kutua na kuondoka.

#MillardAyoUPDATES



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post