Hii ndo Gharama ya Kuleta basi la Ubingwa la Yanga kwa Siku Moja



Moja kati ya vivutio katika sherehe za Ubingwa wa Yanga ni pamoja na basi la wazi ambalo wamelikodi kutokea Uganda kuja Tanzania katika parade ya Ubingwa na watu wengi wamekua wakitamani kujua gharama za kuleta basi hilo nchini kwa siku ni kiasi gani,

Dereva wa basi hilo katika mahojiano na Ayo TV amefafanua kuwa, kwa makadirio, kukodi basi hilo ni kiasi cha dola elfu moja kwa siku ambayo ni zaidi ya Milioni mbili na laki moja tatu za kitanzania.

Amesema, matumizi ya basi hilo kwa Uganda ni pamoja na Kufanya tour za mjini na za shule, sherehe mbali mbali zikiwemo harusi, za kuzaliwa na hata mikutano vyote vinafanyika ndani ya basi.

Dereva huyo amefafanua kuwa aliwahi kuja Tanzania kama abiria, lakini kuja na gari hiyo kwa shughuli hizo za mpira kwake ni mara ya kwanza na amesema jambo hilo ni zuri sana na hajawahi kuona kwao Uganda.

“Ni jambo zuri sana, aina ya Mashabiki na sapoti wanayotoa kwa timu kama hivi, sijawahi kuona,” Alisema dereva huyo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post