AZAM FC YAICHAPA PRISONS 1-0 NA KUREJEA TATU BORA-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa Jumatano Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Bao pekee la Azam FC limefungwa na mshambuliaji wake Mkongo. Idris Mbombo dakika ya 21 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 43 na kupanda nafasi ya tatu, wakiizidi pointi Geita Gold baada ya wote kucheza mechi 28.
Hali inazidi kuwa mbaya kwa Tanzania Prisons baada ya kichapo hicho wanabaki pointi zao 26 katika nafasi ya 14 katika Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitateremka moja kwa moja.
Ikumbukwe timu zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao katika mechi mbili za nyumbani na ugenini na timu itakayoshinda ndiyo itabaki Ligi Kuu, wakati itakayofungwa itacheza na JKT Tanzania ya Championship na mshindi atacheza tena Ligi Kuu msimu ujao.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post