Wydad waivua ubingwa wa Afrika Al Ahly



Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco imeshinda ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Mabao ya ushidi ya Wydad katika mchezo huu yamefungwa na Zouheir El Moutaraji aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 15 na 48. Hii ilikuwa ni fainali ya 5 Wydad wanacheza katika michuano hii na wamekuwa mabingwa kwa mara ya 3, wametwaa ubingwa mwaka 1992, 2017 na 2022.

Mchezo huu umecezwa katika uwanja wa Mohammed wa 5 nchini Morocco ambao ni uwanja wa nyumbani wa Wydad hivyo walikuwa na faida ya kuwa na mashabiki wengi katika mchezo huu na wakafainikiwa kuwavua ubingwa Al Ahly ambao walikuwa wametwaa taji hili misimu miwili mfululizo iliyopita.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post