Vipofu Wawili Wapendani Kwa Dhati na Kuamua Kufunga Ndoa


Wawili hao pichani ambao wote hawaoni kabisa(blinds) wamefunga ndoa. Mwanaume anaitwa Thankgod na ni mwanasheria nchini Nigeria wakati mke wake huyo kwa jina la Amarachi ni mwajiriwa wa serikali katika wizara ya elimu nchini humo


Mwanaume amesema alijaribu kuvunjwa moyo aliposema anataka kuoa lakini akaweka msimamo wake kwani anajua nini anataka katika maisha. Amesema japo wote yeye na mkewe wake huyo hawaoni lakini wanapendana kwa dhati na kila mmoja wao amekuwa msaada kwa mwenzake


Harusi yao imefungwa kanisa la St.Peters nchini humo na kuhudhuriwa na viongozi wa kikatoliki si chini ya 15 wakiwemo pia viongozi wa kiserikali




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post