IMEELEZWA kuwa, Simba imepiga hodi TP Mazembe kumfuata mshambuliaji Zemanga Soze kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo ya kumsajili.
Wapo baadhi ya washambuliaji wanaotajwa kuwaniwa na Simba katika kukisuka kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.
Kati ya washambuliaji wanaotajwa kutua Simba ni Yunus Sentamu anayeichezea AS Vita ya DR Congo na timu ya taifa ya Uganda.
Mmoja wa mabosi wa Simba, ameliambia Spoti Xtra kuwa, wamepokea majina tofauti ya washambuliaji kutoka kwa mawakala waliowapa tenda ya kuwatafutia wachezaji wa kigeni wenye kiwango bora.
Bosi huyo alisema jina la mshambuliaji huyo lipo katika orodha ya wachezaji wanaotajwa kutua Simba, hivyo kama mipango ikikaa sawa, basi atasaini mkataba wa miaka miwili.
Aliongeza kuwa, tayari mabosi hao wa Simba wamepeleka ofa baada ya kuridhishwa na kiwango chake ambaye atakuja kuchukua nafasi ya Mkongomani, Chris Mugalu anayemaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu.
“Kuna majina ya wachezaji wengi ambayo yapo katika orodha ya wachezaji watakaokuja kuichezea Simba msimu ujao ambao tumepanga kufanya usajili mkubwa.
“Usajili huo tutakaoufanya maalum kwa ajili ya michuano ya kimataifa na kikubwa timu tunataka kufika hatua nzuri kimataifa ikiwezekana fainali.
“Hilo linawezekana kabisa, kwani mipango yote imekamilika na nafasi ambazo kocha amezipendekeza ni safu ya ulinzi na ushambuliaji ambayo Soze yupo katika orodha hiyo ya wachezaji tunaowahitaji,” alisema bosi huyo.
Pablo alizungumzia usajili wa msimu ujao akisema: “Nimepanga kuifanyia maboresho safu ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao, hiyo ni kutokana na washambuliaji wangu kuniangusha katika michuano ya kimataifa msimu huu kutokana na kukosa umakini mdogo katika kufunga.”
STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA
Post a Comment