Mchekeshaji Stan Bakora akoshwa na jitihada za Harmonize kuendelea kumuomba msamaha Kajala kwani amesema anamfundisha kitu cha tofauti sana.
Stan amevitaja vitendo hivyo vya mkali huyo kuwa ni UTU, kwa hadhi yake angeweza kupata wanawake wengi tu lakini mapenzi ya kweli na ya dhati ndio yanamrejesha Tembo kwa Frida, lengo kuu likiwa ni kumaliza mgogoro baina yao na kurejesha mahusiano yao kama ilivyokuwa hapo awali.
Huu ndio ujumbe wa Stan Bakora kupitia ukurasa wake wa Instagram.
"Mara Nyingi Tunaongea Utani, Tunacheka. Lakini Kwa Hili Naomba Nieleweke Kwamba Namaanisha. Suala la Harmonize Kumuomba Msamaha Kajala, Imefika Mahali Linanigusa Sana. Harmonize Ananifundisha Kitu Cha Tofauti Sana Aisee.
Kwa Hadhi Yake, Jina Lake Na Kila Kitu, Anaweza Kupata Wanawake Wengi Tu.Anaweza Pia Kuwa Na Kiburi Aseme Haombi Msamaha. Lakini Angalia Anachokifanya Kwa Kajala!. Huo ni UTU.
Dini Zetu Zote Zinatufundisha Kuomba Msamaha, Zinatutaka Pia Kusamehe. Hivi Kma Mungu Angehesabu Makosa Yetu Ni Nani Angesimama? Kajala, Kwa Kuwa Harmonize Ameomba Msamaha Kiasi Hiki, Rudisha Moyo Nyuma Mwanangu Sana Frida. Samehe Saba Mara Sabini, Tumpishe Shetani Apite.
Acha Mapenzi Yashinde, Achana Na Maneno Na Hofu Kwamba Watu Watakuonaje. Harmonize Ameweka Mbali Hiyo Hofu, Mapenzi Ya Dhati Yamemuongoza. Hakuna Aliye Mkamilifu."
#KajalaGoBack #FridaMsameheRajabu
Post a Comment