Simba Yaichapa Kagera 2-0 kwa Mkapa Yaongeza Presha kwa Yanga-Michezoni leo

Kibu Dennis akishangilia bao lililofungwa na John Bocco

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Mabao ya Simba yamefungwa na Kibu Dennis pamoja na John Bocco yote katika katika kipindi cha kwanza na kufanya Simba kufikisha jumla ya alama 49 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

 

Simba ambayo ipo nafasi ya pili imeongeza presha kwa vinara wa msimamo wa Ligi hiyo Yanga ambayo ina jumla ya alama 57 baada ya kuwa na matokeo ya sare tatu mfululizo tangu mechi dhidi ya Simba.

Kibu Dennis akishangilia bao alilofunga dhidi ya Kagera Sugar

Baada ya mchezo huo Simba inatarajiwa kwenda kucheza mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Pamba ambao kama watafanikiwa kufuzu basi watakutana uso kwa uso na watani wao wa jadi Yanga ambao wao walishafanikiwa kufuzu kwa kuwatoa Geita Gold kwa changamoto ya mikwaju ya penati

The post Simba Yaichapa Kagera 2-0 kwa Mkapa Yaongeza Presha kwa Yanga appeared first on Global Publishers.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post