LICHA ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya Miaka 17 Serengeti Girls kushinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Cameroon, tukio kubwa limekuwa ni namna ambavyo mchezaji wa Tanzania Clara Luvanga alivyodhalilishwa nchini humo.
Clara Luvanga alidhalilishwa kwa kuhisiwa kuwa ni mwanaume na hadi ikafikia hatua Madaktari wa Cameroon wakaenda kumchunguza kuwa ni Mwanamke kweli au Mwanaume! baada ya kujiridhisha kuwa ni mwanamke basi akaruhusiwa kurudi na kuendelea na mchezo.
Baada ya matokeo hayo Serengeti Girls itahitaji matokeo ya sare yoyote au ushindi ili kujikatia tiketi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 17.
Post a Comment