Moja ya story kubwa kwenye blogs na mitandao mbalimbali ulimwenguni ni kuhusiana na kile kilicho onekana kwenye Video mpya ya Msanii @asaprocky inayoitwa D.M.B na Rihanna (@badgalriri ) akishiriki kama Video Queen.
Kipande kilicho leta gumzo kubwa toka kwenye Video hiyo, ni kuanzia dakika 03:02 namna A$ap Rocky alivyoomba Kumuoa Rihanna kwa kutumia Grills alizovaa kwenye meno,zikiandikwa MARRY ME? na Rihanna akijibu kwa Grills alizovaa kwenye meno zikiandikwa “I Do“ ikiwa na maana kuwa anakubali kuolewa na A$ap Rocky.
Mwishoni mwa Video Hiyo, Wawili hao wanaonekana kufunga ndoa, Rihanna akiwa kwenye gauni la harusi na maua Rose mkononi,huku mnyamwezi Asap akipiga Suti flani kiaina. Matukio mengi kwenye video hiyo yameshutiwa kipindi ambacho kwa mara ya kwanza Rihanna na Asap Rocky walijitokeza hadharani na Rihanna akionekana ana mimba.
Post a Comment