RASMI: Mwisho wa Enzi za Roman Abramovich Chelsea Yauzwa kwa Mmiliki Mpya-Michezoni leo

Todd Boehly anatarajiwa kuwa mmiliki mpya wa Klabu ya Chelsea

KLABU ya Chelsea ya Uingereza imeuzwa rasmi kwa mmiliki mpya na hivyo kufikisha mwisho wa enzi za utawala wa bilionea wa Kirusi Roman Abramovich.

 

Kupitia tovuti ya klabu hiyo imeandika:

 

Klabu ya Chelsea inaweza kuthibitisha kuwa imefikia makubaliano ya uuzwaji wa klabu hii kwa mmiliki mpya, Kundi likiongozwa na Todd Boehly, Clearlake Capital, Mark Walter na Hansjoerg Wyss kuinunua klabu hii.

 

Jumla ya kiasi cha pesa kilichowekwa kwa ajili ya manunuzi ya klabu, kiasi cha dola bilioni 2.5 kitawekwa kununua hisa za klabu hii na kisha kiasi hicho kitawekwa katika akaunti maalum ya Benki ya Uingereza ambapo asilimia 100 ya pesa hiyo itatumika kuchangia hisani ya wahanga wa vita nchini Ukraine kama ilivyokuwa nia ya Abramovich.

 

SerIkali ya Uingereza itatakiwa kupitisha uhamishaji huo wa pesa kutoka kwenye akaunti maalum kwenda moja kwa moja kusaidia wahanga wa vita ya Ukraine.

 

Kiasi kingine cha fedha cha dola bilioni 1.7 kitatakiwa kutolewa na wamiliki wapya kwa ajili ya uwekezaji hasa wa marekebisho ya Uwanja wa Stamford Bridge, Akademi ya vijana, timu ya wanawake pamoja na kuendelea kusaidia mfuko wa hisani wa klabu hiyo.

 

Taratibu zote za mauzo ya klabu hiyo zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei ikihitaji kukamilika kwa taratibu zote za msingi, taarifa nyingine kwa kina zitatolewa ndani ya kipindi kijacho.” Taarifa kutoka Klabu ya Chelsea.

Mark Walter mmiliki mwenza wa klabu ya Chelsea

Kwa sasa inasubiriwa kuona ni kwa namna gani klabu hiyo itaweza kuendeshwa katika zama hizi mpya ukilinganisha na jinsi ilivyokuwa na mafanikio enzi za utawala wa Roman Abramovich kwani kumekuwa na sintofahamu juu ya mustakabali wa baadhi ya wachezaji huku wengine wakiondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

 

Mfano mzuri ukiwa ni walinzi wa kati kama Antonio Rudiger na Andreas Christensen ambao wote watatimka mwezi ujao lakini pia hatima ya wachezaji wengine kama Romelu Lukaku, Christian Pulisic, Timo Werner, Cesar Azpilicueta, Marcos Alonso pamoja na Ross Barkley bado haijulikani

The post RASMI: Mwisho wa Enzi za Roman Abramovich Chelsea Yauzwa kwa Mmiliki Mpya appeared first on Global Publishers.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post