Rapp Chidi Beenz Afunguka Kutapeliwa PESA Zake Sehemu...Amechoka Adai Kufunguka A to Z


Rapp Chidi Beenz amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kuna sehemu amezulumiwa/kutapelewa pesa zake na sasa amechoka hivyo muda wowote ataongea.

Hapa chini ni ujumbe wa @official_chidibeenz

"Kuna namna Wasanii wanakua chini kifedha but saa zingine kuna mengi. Kuna wengi ambao wanasababisha maisha hayo na wao hawaonekani wala kujulikana zaidi ya wao tena kuchangia uonekane umefeli. Kuna namna nimefatilia pesa zangu na watu wanaozimiliki na kuziiba. Ok kuna wakati Binadamu unaghafilika ila haimaanishi uchukue vyangu kwa ujinga unauona wewe.

Nimepigania Nchi yangu nimepigania mashabiki wangu na nimewapa Burudani Wananchi wangu wa ndani na nje. Bora kuniibia au kunionyesha labda sitokula mimi ila Wanangu watapata na Mama zao? Familia yangu pia hata Mashabiki zangu. Unaiba zangu za wengine na husaidii chochote zaidi ya kubomoa kuhonga na kula Bata. Then mimi kichaa?

Kuchanganyikiwa au kughafilika katika Maisha kila mmoja anapitia, hutakiwi kucheka hutakiwi kutokua na Heshima. Tunapitia vingi na tunakutana na wengi. Sisi ambao hatuna matabaka tunakaa na kila mmoja. Wengi wanatumwa kwa mengi, Magroup mangapi yamevunjika wasanii wangapi wamepotea.

Mimi nimewahi kumsaidia mtu ambae hakua sawa nia yangu ilikua akae sawa akaangalie Familia na mimi yakinikuta siku sio lazima yeye yule ambae aliona yule akisaidika atanisaidia.

Sio unichukulie vyangu then ufanye Anasa ili useme chizi lile madawa yamemtawala na mibange. Why usichukue ukawapa familia yangu uwaambie amekua msanii kwa miaka mingi sana kwahiyo tunamsaidia sababu amewahi kutupa burudani na kutuelimisha. Wanangu waone faida ya kushinda Tuzo 5.

Baba mwanamziki na ana marafiki ambao amefanya nao kazi na wana sauti yake na Sura yake. Amechangia Sanaa na Nchi yake kwa kusafiri ndani na nje. Hana zuri Amefanya jamaani hata moja??? Tamaa inafanya unapanga mengi ya kumchafua kuliko ya kumjenga. Sasa chizi unachukua vyake vya nini? We mzima kwanini usidili na vyako tu?


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post