Mwimbaji nyota wa muziki wa Bongofleva, msanii @ommydimpoz amesema yeye hapendi kutembea na walinzi ama mabaunsa kama ilivyo kawaida ya wanamuziki wengine.
Dimpoz ameyasema hayo kwenye Leo Tena ya CloudsFm, ambapo alikuwa amekwenda kwa ajili ya kuutambulisha wimbo wake mpya na msanii Meja Kunta uitwao “Cheusi Cheupe”.
“Mimi nije na walinzi hapa studio kwani nyie mnapiga watu, labda nikienda kwenye hafla ambayo najua itakuwa na vurugu ndio naweza kwenda na walinzi.” alisema @ommydimpoz Ameongeza kwamba, anaamini kuna sehemu za kwenda na walinzi na nyingine za kwenda peke yake.
Kuhusu wimbo “Cheusi Cheupe” ambao wenye mahadhi ya Singeli, Dimpoz alisema kwamba Meja ndiye aliyekuwa na wazo la wimbo huo ila jina la kwanza alifikiria ni “Cheusi Mangara” naye akamshauri walibadilishe ili mabinti weupe wasihisi kutengwa.
“Ndani ya wimbo huo, hatuja shindanisha wanawake weupe na weusi ila kila mmoja amemsifia wake.” alisema Dimpoz. Alipoulizwa rangi anayopendelea kwa wanawake, Ommy Dimpoz alijibu kijanja swali hilo ambapo alisema, “Mimi napenda wanawake weupe japo weusi nawapenda pia ila sielewi kwanini napata weupe”.
Post a Comment