Rapa Quavo Huncho kutokea Kundi la Migos amekataa kujibu kuhusiana na tuhuma za kundi lao hilo kuvunjika.
Siku ya Alhamisi (Mei, 19) zilisambaa tetesi kuwa kundi la Migos linalojumuisha wasanii watatu (Quavo, Offset na Take Off) limevunjika) baada ya Offset kuwa-unfollow Quavo na Take Off kwenye mtandao wa instagram.
Siku ya jana (Mei, 20) Take Off na Quavo waliachia ngoma yao mpya #HotelLobby ambapo Rapa Offset hajasikika katika ngoma hiyo kitu ambacho kikafanya watu wengi waendelee kuamini kuwa kundi hilo limevunjika.
Katika video iliyochukuliwa na Paparazzi moja huko Marekani, ilimuonyesha Quavo akikataa kuongelea swala la Kuvunjika kwa Kundi hilo mara baada ya kuulizwa huku akiendelea kuwaacha watu kwenye maswali mengi.
Post a Comment