Mwanamke maarufu jijini Mwanza aitwaye Swalha, aliyekuwa akijishughulisha na masuala ya urembo (make up artist) ameuawa kwa kupigwa na risasi na mumewe usiku wa kumkia Jumapili ya May 29. Tukio hilo limetokea nyumbani kwa wanandoa hao huko Buswelu huku chanzo kikielezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa mume wa Swalha anayejulikana kwa jina la Said alichukua uamuzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Amesema Swalha alienda kuangalia mpira na akachelewa kurejea nyumbani. Mumewe hakufurahishwa na kitendo cha mkewe kuchelewa kurudi nyumbani hivyo kukazuka ugomvi baina yao hali iliyopelekea mume wa Swalha kumfyatulia risasi.
Post a Comment