Mshambuliaji wa Timu ya Geita Gold Anayemnyima Mayele wa YANGA Usingizi Kwa Kutupia Magoli Ataka Kucheza Uingereza

 


Mshambuliaji wa Timu ya Geita Gold ya mjini Geita amesema kuwa ndoto yake kubwa ni kuchezea timu zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) kwa kuwa ndio ligi yenye ushindani zaidi duniani.

Mpole amesema hayo katika mahojiano maalumu na HabariLeo ikiwa ni siku chache baada ya kutangazwa kuwa mchezaji wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa mwezi aprili.


“Natamani sana kucheza mpira Uingereza, kwa sababu ya staili ya uchezaji, navutiwa sana na hata mechi nyingi sana za ligi ya Uingereza huwa ninaziangalia, ni ligi yenye ushindani, ligi inayotazamwa sana duniani.

Ameongeza “Kuna vitu huwa naviangalia navifanyia kazi, wanavyocheza, kuna baadhi ya vitu ambavyo naona hata mimi naweza kufanya, ingawa siyo kwa asilimia kubwa wenzetu wameimarika zaidi, lakini kuna baadhi ya vitu nikiviangalia navifanyia kazi”



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post